Sisi hatukupaswa kutoa msaada wa fedha Uturuki, tulitakiwa kutuma kikosi cha uokoaji

Sisi hatukupaswa kutoa msaada wa fedha Uturuki, tulitakiwa kutuma kikosi cha uokoaji

Kukosa akili ni kubaya sana. Bahati mbaya tuna Viongozi wengi ovyo
 
Msaada wetu kwa Uturuki umechelewa sana, tunaanza kucheza wakati mziki umeisha!

Sisi hatutakiwi kutoa msaada wa kifedha kwa wale jamaa, bali tulitakiwa kupeleka kikosi cha uokoaji kwenda kusaidia uokozi kwenye majengo yaliyoporomoka na kukalia watu.

Tulikuwa wapi kutoa msaada wa aina hii mapema? Mahitaji makubwa ya Uturuki haikuwa fedha, bali vikosi vya uokozi.
Kwani fedha za kwako? Msaada bado unahitajika licha ya kwamba tulichotoa ni mdogo sana.
 
Samia ni Kiongozi ,kwanza mswahili, alafu akapata Washauri wabovuuuuu kwelikweli, wengi wa Washauri wa Samia, ni walamba Asali.
Changamoto ya kuwaza kwa kutumia tumbo badala ya kichwa! Ukishakuwa chawa, huwezi kuwa na ushauri wa maana
 
Kwani fedha za kwako? Msaada bado unahitajika licha ya kwamba tulichotoa ni mdogo sana.
Hapo ndo unapokosea!
Hujui kwamba hizo ni kodi zetu?
Au hujui kwamba kila bidhaa unayoinunua Kuna kiasi cha kodi unalipia?
Hii nchi ina watu wa ajabu sijapata kuona!
 
Wewe una uzoefu gani wa kumzidi Rais Samia?

pengine tangu uzaliwe hujawahi kuongoza walau kikundi cha watu 10 hata kwny kuokota kuni lakini unajifanya mjuaji wa masuala ya kimataifa!
Acha uchawa, fanya kazi halali, utaonekana tu
 
Back
Top Bottom