Sisi Simba SC na wachambuzi uchwara tumemponza Fei Toto

Tatizo kubwa hawa wachezaji wetu huwa hawasomi mikataba yao na pia hiyo mikataba wakipewa wanafikiri kuwa ni kama barua za uchumba tu, hawasomi na kuelewa kuwa huo ni mkataba ambao una pande mbili.

Unapohitaji kuvunja mkataba lazima pande zote mkae mezani muelewane kuwa sasa tunavunja mkataba kwa sababu zifuatazo unazitaja mkikubaliana mkataba unaendelea msipokubaliana ndipo mnavunja mkataba. Sijawahi ona katika maisha yangu mkataba unavunjwa upande mmoja tu hasa ambayo iko chini ya FIFA.

Wachambuzi wa tanzania ni wachumia tumbo hakuna wanachokijua vichwani mwao,uchambuzi wao umejaa mapenzi ya timu na siyo uchambuzi wa kumwelimisha mchezaji. Namshukuru sana mzee Rage aliweka wazi na Feisal angekuwa na akili angemsikiliza huyu mzee na angefuata maelekezo yake.

Lakin akaendelea kuwasikiliza wanasheria uchwara na wachambuzi uchwara wamempoteza sasa.
 
Walipohukumu kesi ya Morrison mliona TFF wapo sahihi kwavile wafaidikaji ni Simba, ila kwavile kesi ya Feitoto imewapa Yanga ushindi mnaona kuwa TFF imejaa wahuni.
Unaandika vitu vya ajabu tu..!!

Kila siku mna kesi za kuhusu mikataba ya wachezaji na wadhamini, hii inawaonesha mlivyo weupe kwenye hayo mambo.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kweli wenye akili ni wawili tu.Mlifanya mpaka mkutano wa wazee wa Yanga mkiwalaumu Azam.Mkatishia kususia bidhaa za Azam, ujinga ulioje.
Sasa mmetapatapa mnaanza kuilaumu Simba.
Mnampa mshahara wa tarishi akagoma mnasingizia wengine wote isipokuwa ujinga wenu.

Kwani aliyesema ishu ya Simba ni nani?? Yanga kama timu au ni mleta mada JF..??
 
Kwa hiyo unakanusha anayedai mwenzako?At least kuna matumaini.Kuna wachache wanaanza kutumia akili lakini cha kuhuzunisha sio wengi!
 
Unaandika vitu vya ajabu tu..!!

Kila siku mna kesi za kuhusu mikataba ya wachezaji na wadhamini, hii inawaonesha mlivyo weupe kwenye hayo mambo.
Huyo mdhamini kachukua hatua gani kama Yanga ndiyo iliyokiuka taratibu za mkataba? Huyo Feisal wako si umshauri aende CAS na kama pesa hana basi mchangieni ili akapate haki yake ambayo mnahisi kaonewa.
 
Tarimba kwa ujinga wake amekuwa mpole kwasababu anajua mmebaki utopolo peke yenu mnaombeba, kama Simba tungekuwa.na udhamini wa Sports Pesa angewaburuza mahakamani na mngemlipa, ushabiki wake kwa utopolo unamponza.

Fei Toto sio boya kama Tarimba, barua zote mlizomuandikia kulia lia arudi kambini amezichoma moto, hataki mahaba ya kijinga na washamba msiojua kuheshimu mikataba, hata kuonesha kipengele alichokiuka kwenye mkataba mmeshindwa, Mwigulu anawabeba sana, mpeni Urais wa klabu.
 
TFF kwenye shauri la Feisal Salum wameboronga haswa ndio maana wameshindwa mpaka sasa kumjibu kuhusu ombi lake la kutaka hukumu ifanyiwe review.
Huwezi kuwa na Mwenyekiti wa kamati inayoamua jambo la kisheria na yeye sio mwanasheria!
Inawezekana Feisal kafanya kosa lakini asikilizwe kwa kufuata taratibu za kisheria ili haki itendeke. Kusema tu ni mchezaji wa Yanga bila kupitia anacholalamikia na huku akiamini mkataba umevunjika ni kumuonea.
Maamuzi yote yange base kwenye kanuni na vipengele vya mkataba.
 
Tarimba ni owner wa SP? maneno ya mzee Rage yataishi daima
 
Mpaka sasa hatusikii wachambuzi na vyombo vya habari vilivyokuwa vikizungumzia swala la FEI TOTO wakiwa wanamzungumzia tens saizi wapo kimya na huenda walisha sahau na siku zote vitu vya kuambiwa changanya na akili yako, Leo hii wenzake wapo Tunisia yeye yupo Dar na endapo angetumia hekima na busara hii michuano ingemfaa zaidi na angeonekana sehemu mbalimbali na klabu inayomhitaji ingekuja kuvunja mkataba na kumsajiri lakini mpaka sasa kimya.

Hata wale mashabiki,wachambuzi na media zilizokuwa zinamsapoti saizi wapo kimya mpaka sasa anapotea machoni mwa watu mpaka arudi atatumia nguvu kubwa rejesha jina lake machoni mwa watu . Namshauri arudi amalizane na Yanga achane na maneno ya watu.

Imeandikwa na Chirstopher Mlanda

Ameandika @deustanzania
Simba walihusikaje hapo
 
TFF kwenye shauri la Feisal Salum wameboronga haswa ndio maana wameshindwa mpaka sasa kumjibu kuhusu ombi lake la kutaka hukumu ifanyiwe review.
Huwezi kuwa na Mwenyekiti wa kamati inayoamua jambo la kisheria na yeye sio mwanasheria!
Inawezekana Feisal kafanya kosa lakini asikilizwe kwa kufuata taratibu za kisheria ili haki itendeke. Kusema tu ni mchezaji wa Yanga bila kupitia anacholalamikia na huku akiamini mkataba umevunjika ni kumuonea.
Maamuzi yote yange base kwenye kanuni na vipengele vya mkataba.
Hii case hata mjumbe wa nyumba 10 anaweza imaliza, mchezaji ana mkataba mpaka 2024 anataka kuondoka taratibu zina fahamika mbona hii ni case ya dakika 2 imeisha! unataka TFF wafanye nini?
 
Kama ni case ya dakika 2 inakuwaje mpaka sasa TFF wanashindwa kumpa review?Wanaficha nini?Wacha kuleta majibu rahisi kwenye masuala ya kisheria.
 
Walipohukumu kesi ya Morrison mliona TFF wapo sahihi kwavile wafaidikaji ni Simba, ila kwavile kesi ya Feitoto imewapa Yanga ushindi mnaona kuwa TFF imejaa wahuni.
Na walipohukumu hiyo hiyo ya Morrison mliona TFF ya hovyo kwasababu haikuwapa ushindi na mkaenda CAS

Ila kwasasa kwavile imewapa ushindi mnaona kamati imefanya haki kabsa kweli mkuki kwa nguruwe.
 
Tarimba kwa ujinga wake amekuwa mpole kwasababu anajua mmebaki utopolo peke yenu mnaombeba, kama Simba tungekuwa.na udhamini wa Sports Pesa angewaburuza mahakamani na mngemlipa, ushabiki wake kwa utopolo unamponza.

Fei Toto sio boya kama Tarimba, barua zote mlizomuandikia kulia lia arudi kambini amezichoma moto, hataki mahaba ya kijinga na washamba msiojua kuheshimu mikataba, hata kuonesha kipengele alichokiuka kwenye mkataba mmeshindwa, Mwigulu anawabeba sana, mpeni Urais wa klabu.

Kwani sportpesa ni ya Tarimba? Pole na endaleeni ku hamasisha watalii wa visit Tanzania bure..

Hiyo Feisal kaandikiwa barua kama uthibitisho wa hatua walizotekeleza. Nyie endeleeni kumpotosha kwa kumfanya ajione mwamba
 
Na walipohukumu hiyo hiyo ya Morrison mliona TFF ya hovyo kwasababu haikuwapa ushindi na mkaenda CAS

Ila kwasasa kwavile imewapa ushindi mnaona kamati imefanya haki kabsa kweli mkuki kwa nguruwe.
Yanga ilienda CAS kwavile waliona kama haki haikutendeka, hivyo hata Feisal anayo haki ya kwenda CAS kama hajaridhika na hukumu ya TFF
 
Basi tusubiri tuone kama ataenda CAS au atarudi kambini

Uzuri akirudi kambini na Injinia akasema wamuimbe tena Fei wale wale waliokuwa wanamtukana wataanza kumuimba bila hata kuombwa msamaha kwa lile walilokuwa wanahisi wamekosewa.
 
Kwamba umeshahau mlivyokuwa mnamdanganya eti Fei shikilia hapo hapo. Masimba Si mlijifanya wanasheria wake mkampa na vifungu vya mkataba vinavyoruhusu kurudisha milioni 112 na awe huru, mmeanza kujitoa sasa.

Huyu dogo aliambiwa Sana awe makini akaona raha kupost post insta sasa anajikuta anabaki peke yake waandishi wanachambua wimbo wa Diamond Zuwena sasa na masimba yako bize kutetea jezi zao
Mkuki kwa nguruwe eeh!? mlitufanyie kwa singano?
 
Mpaka sasa hatusikii wachambuzi na vyombo vya habari vilivyokuwa vikizungumzia swala la FEI TOTO wakiwa wanamzungumzia tens saizi wapo kimya na huenda walisha sahau na siku zote vitu vya kuambiwa changanya na akili yako, Leo hii wenzake wapo Tunisia yeye yupo Dar na endapo angetumia hekima na busara hii michuano ingemfaa zaidi na angeonekana sehemu mbalimbali na klabu inayomhitaji ingekuja kuvunja mkataba na kumsajiri lakini mpaka sasa kimya.

Hata wale mashabiki,wachambuzi na media zilizokuwa zinamsapoti saizi wapo kimya mpaka sasa anapotea machoni mwa watu mpaka arudi atatumia nguvu kubwa rejesha jina lake machoni mwa watu . Namshauri arudi amalizane na Yanga achane na maneno ya watu.

Imeandikwa na Chirstopher Mlanda

Ameandika @deustanzania
LIMWANAMKE LIKIRUDI KWAO USILIFUATE WALA KULITAFUTA

nimenukuu sehemu ila ni humuhumu jamvini.
 
Back
Top Bottom