Sisi tuliiga wapi kuwa na vyeo vyote viwili vya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais?

Waziri asiye na wizara kama George Mkuchika.
Siyo kweli, Mudavadi ni Mkuu wa Mawaziri japo katiba haimtambui ila Ruto ndiye kamwajiri.

Hii inaonyesha kwamba cheo cha Waziri Mkuu haswa kwa Afrika, bado kina umuhimu.
 
Kwenye nchi nyingi maarufu zenye mfumo wa Urais wenye nguvu ziko hivi
1. Marekani-Haina waziri mkuu, ina makamu wa Rais

2.Ufaransa-Haina makamu wa Rais, ina Waziri Mkuu

3. Africa Kusini- Haina waziri mkuu, ina makamu wa Rais

4.Kenya-Haina waziri mkuu, ina makamu wa Rais

5.Zambia- Haina waziri mkuu, ina makamu wa Rais

6.Ghana- Haina waziri mkuu, ina Makamu wa Rais.

7. Senegal- Haina makamu wa Rais, ina Waziri Mkuu

8.Botswana-Haina waziri mkuu, ina Makamu wa Rais

9. Brazil- Haina waziri mkuu, ina Makamu wa Rais

10. Korea Kusini- Haina makamu wa Rais, ina Waziri mkuu
Kwani lazima kuiga? Ni uvumbuzi Wetu tena yupo Hadi Naibu Waziri Mkuu
 
Siyo kweli, Mudavadi ni Mkuu wa Mawaziri japo katiba haimtambui ila Ruto ndiye kamwajiri.

Hii inaonyesha kwamba cheo cha Waziri Mkuu haswa kwa Afrika, bado kina umuhimu.
Mkuu wa mawaziri ni Rais
 
But vijana Kila siku wanalilia Ajira,Sasa ukifuta vyeo vya ukuu wa wilaya automatically takribani watu 1000 wanaKosea Ajira
Ajira zitaongezeka kama serikali itatumia pesa vizuri hasa kwa walio juu. Rais halipi kodi, anahudumiwa kila kitu, posho na mshahara anapata, makamu wa rais vivyo hivyo, waziri mkuu hivyo hivyo, marais wastaafu za Tanganyika na Zanzibar hivyo hivyo, kuna wabunge, majaji na spika na naibu wake wote hawalipi kodi na wanahudumiwa na serikali. Ni pesa nyingi mno ambazo zingetosha kuajiri maelfu ya vijana.
 
Vipo vyeo inatakiwa kufutwa
1 Makamu wa rais
2 Mkuu wa wilaya, huyu majuku yake atafanya mkurugenzi w
3 naibu waziri huyu kazi zake atafanya katibu wa wizara
Nchi hii inaongoza duniani kuwa na lundo la mavyeo yasiyo na tija. Kwa mfano kuanzia ngazi ya chini ya kata kuna katibu kata na katibu kata mtendaji, wilayani kuna mkuu wa wilaya, kuna DAS na mkurugenzi mtendaji wa wilaya, mkoani kuna mkuu wa mkoa na RAS. Taifani kuna Rais, makamu wa rais, waziri mkuu na sasa naibu waziri mkuu ambaye hata kwenye scheme of service hayupo. Sasa ukiangalia utitiri wote huo wa viongozi hakuna tija yoyote ya maana. Kama taifa tujitafakari. Pesa nyingi inatumika kiholela.
 
Ni gharama kubwa kwa walipa kodi na misafara isiyo na maana
 
Ajira zitaongezeka kama serikali itatumia pesa vizuri hasa kwa walio juu. Rais halipi kodi, anahudumiwa kila kitu, posho na mshahara anapata, makamu wa rais vivyo hivyo, waziri mkuu hivyo hivyo, marais wastaafu za Tanganyika na Zanzibar hivyo hivyo, kuna wabunge, majaji na spika na naibu wake wote hawalipi kodi na wanahudumiwa na serikali. Ni pesa nyingi mno ambazo zingetosha kuajiri maelfu ya vijana.
Una waambia watu walipe kodi huku wewe mshahara wako haukatwi kodi, sijui ni kuona watu ni wajinga
 
Siyo kweli, Mudavadi ni Mkuu wa Mawaziri japo katiba haimtambui ila Ruto ndiye kamwajiri.

Hii inaonyesha kwamba cheo cha Waziri Mkuu haswa kwa Afrika, bado kina umuhimu.
Hakuna umuhimu wowote, Majaliwa anasaidia nini zaidi ya kutuongezea gharama kubwa za matumizi na asipokuwepo nini kitakosekana?
 
Una waambia watu walipe kodi huku wewe mshahara wako haukatwi kodi, sijui ni kuona watu ni wajinga
Na mshahara na posho haununui hata kitunguu kimoja. Kila kitu bure na hapo hapo inasemwa wanaolipa kodi ni wachache kumbe ni watumiaji wachache ndio wanaoneemeka na kodi hizo.
 
Hakuna umuhimu wowote, Majaliwa anasaidia nini zaidi ya kutuongezea gharama kubwa za matumizi na asipokuwepo nini kitakosekana?

Mawaziri hawatasimamiwa.

Kama kuna Katibu Mkuu Kiongozi, na Makatibu Wakuu, hivyo hivyo uwepo wa Waziri Mkuu na Mawaziri inasadifu kiutawala.
 
Kwenye nchi nyingi maarufu zenye mfumo wa Urais wenye nguvu ziko hivi
1. Marekani-Haina waziri mkuu, ina makamu wa Rais

2.Ufaransa-Haina makamu wa Rais, ina Waziri Mkuu

3. Africa Kusini- Haina waziri mkuu, ina makamu wa Rais

4.Kenya-Haina waziri mkuu, ina makamu wa Rais

5.Zambia- Haina waziri mkuu, ina makamu wa Rais

6.Ghana- Haina waziri mkuu, ina Makamu wa Rais.

7. Senegal- Haina makamu wa Rais, ina Waziri Mkuu

8.Botswana-Haina waziri mkuu, ina Makamu wa Rais

9. Brazil- Haina waziri mkuu, ina Makamu wa Rais

10. Korea Kusini- Haina makamu wa Rais, ina Waziri mkuu
Just kuwaridhisha wa upande wa pili kwa cheo cha juu ! Then
Waziri Mkuu ndio Mtendaji Mkuu wa shughuli za Serikali za kila siku 😳 !

Lugha gongana ! 😅🙏👍
 
Ishu inaanzia kwenye muungano
Muungano wetu ni wa pekee,ndio umepelekea kuwe na hayo matakataka mengine
 
Mawaziri hawatasimamiwa.

Kama kuna Katibu Mkuu Kiongozi, na Makatibu Wakuu, hivyo hivyo uwepo wa Waziri Mkuu na Mawaziri inasadifu kiutawala.
Msimamizi wa mawaziri ni Rais, yeye ndiye anawachagua, anawapangia kazi na anayefukuza kazi. Hata waziri akitika kujiuzulu anapeleka barua moja kwa moja kwa Rais na sio kwa waziri mkuu.
 
Back
Top Bottom