Uchaguzi 2020 Sisi Watanzania tunakushukuru sana Tundu Lissu kwa kampeni zako za kiwango cha juu, Tunakutakia kila la heri, Mungu aendelee kukulinda

Nikiwa mmoja wa maripota wa Kampeni za Tundu Lissu humu JF na kwingineko kuanzia mwanzo hadi mwisho na kwa kadri ya umri nilionao na uzoefu wangu katika siasa za Tanzania na za kimataifa, Tundu Lissu amefanya kampeni za kiwango cha juu mno, huyu mtu hakuwa tu mgombea wa Urais bali alikuwa Mwalimu wa siasa na haki za Raia.

Elimu kali ya Uraia aliyoitoa kuanzia Zanzibar hadi Tanganyika haijawahi kutolewa na yeyote kuanzia wakoloni wala waliopo leo, amefichua mambo mazito mno yaliyofichwa kwa miaka mingi sana, kwa ujumla ni kwamba kwenye uchaguzi wa mwaka huu wananchi wa Tanzania wamepata faida kubwa mno na nina hakika sasa wananchi wengi sana wameelewa kinaga Ubagha namna nchi yao ilivyojaa makando kando ya aibu yanayolidhalilisha Taifa.

Kwa niaba ya Wananchi wa Tanzania wa ndani na nje ya nchi, natoa shukrani za dhati kwa Tundu Lissu kwa wema wake aliotutendea kwa kuamua kutushirikisha kwenye kila uozo uliofichwa kwa miaka mingi kwenye nchi hii, SPANA zilizopigwa hakuna yeyote katika wanaccm walio hai leo mwenye uwezo wa kujibu , kwa kifupi ni kama wanaccm wote wamevunjwa viuno.

Namuomba Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda Lissu kwa ajili ya Uhai wa Nchi yetu
Mkaambiwa muingie barabarani mkafanya usaliti, ndio maana ameamua kuondoka mapema
 
Lissu utakumbukwa nchi nzima ilicheza prakatatumba
 
Nikiwa mmoja wa maripota wa Kampeni za Tundu Lissu humu JF na kwingineko kuanzia mwanzo hadi mwisho na kwa kadri ya umri nilionao na uzoefu wangu katika siasa za Tanzania na za kimataifa, Tundu Lissu amefanya kampeni za kiwango cha juu mno, huyu mtu hakuwa tu mgombea wa Urais bali alikuwa Mwalimu wa siasa na haki za Raia.

Elimu kali ya Uraia aliyoitoa kuanzia Zanzibar hadi Tanganyika haijawahi kutolewa na yeyote kuanzia wakoloni wala waliopo leo, amefichua mambo mazito mno yaliyofichwa kwa miaka mingi sana, kwa ujumla ni kwamba kwenye uchaguzi wa mwaka huu wananchi wa Tanzania wamepata faida kubwa mno na nina hakika sasa wananchi wengi sana wameelewa kinaga Ubagha namna nchi yao ilivyojaa makando kando ya aibu yanayolidhalilisha Taifa.

Kwa niaba ya Wananchi wa Tanzania wa ndani na nje ya nchi, natoa shukrani za dhati kwa Tundu Lissu kwa wema wake aliotutendea kwa kuamua kutushirikisha kwenye kila uozo uliofichwa kwa miaka mingi kwenye nchi hii, SPANA zilizopigwa hakuna yeyote katika wanaccm walio hai leo mwenye uwezo wa kujibu , kwa kifupi ni kama wanaccm wote wamevunjwa viuno.

Namuomba Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda Lissu kwa ajili ya Uhai wa Nchi yetu

Pole sana. Jana nimeona msafara wake akisindikizwa kuelekea airport tayari kwa safari ya ubelgiji.

Huyu ndiye lisu aliyekuwa anatuamasisha tuingie barabarani baada ya uchaguzi angali yeye anatiketi mkononi🤷🏿‍♂️🤷🏿‍♂️

Mkuu mimi nakushauri uunde chama chako kama bado una interest na siasa. Achana na hizi za chadema
 
Back
Top Bottom