Sita wasomewa mashtaka ya mauaji ya Milembe Seleman aliyekuwa Afisa wa GGM, akiwemo aliyekuwa "mkewe"

Kukatisha uhai wa mtu ni kosa dhidi ya jamhuri.

Mahakama itimize wajibu wake muhimu
 
Kuna ulazima wa kupelekwa kwenye mahakama isiyo na uwezo kusikiliza kesi yao?

Si ni kupoteza muda? Ni halali kumsomea mtu mashtaka bila kumpa nafasi ya kujibu, hata kukana tu?
Kuna ulazima wa wewe kufika mahakamani na kujifunza maana ya hizo hatua. Hizo Mahakama za chini kazi yake ni kukusanya taarifa zote na kuzifaili kwenda Mahakama Kuu baada ya kuwa zimekamilika. Lengo ni kusaidia mahakama za juu kutokuwa na mlolongo mrefu wakati wa kusikilizwa kesi husika.

Kazi kubwa ya mshtakiwa hapo ni kuwafahamu mashahidi na vielelezo ili ajipange jinsi ya kukabiliana nao huko juu. Offcoz hii ni stage ya muhimu sana kwa mshtakiwa pengine kuliko anayeshtaki japo unaona kama anaonewa hivi kwa kuwa hapewi nafasi ya kujibu.
 
Kuna ulazima wa kupelekwa kwenye mahakama isiyo na uwezo kusikiliza kesi yao?

Si ni kupoteza muda? Ni halali kumsomea mtu mashtaka bila kumpa nafasi ya kujibu, hata kukana tu?

Ni utaratibu wa kisheria , ukisubiria committal proceedings kwenda mahakama kuu. Huo muda ofisi ya DPP inakuwa inaandaa ushahidi wa kutosha kuwafungulia kesi hao watuhumiwa.
 

Tuombee DPP apate ushahidi wa kufungua kesi mahakama kuu, isije ikatumika siasa kuiondoa hiyo kesi. Maana mpaka muda huu jalada lipo chapa kwenye ofisi ya DPP.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…