Sitaki niwe mnafiki; siasa za Vyama vya Upinzani zinatakiwa kubadilika kimtizamo kulingana na nyakati

Sitaki niwe mnafiki; siasa za Vyama vya Upinzani zinatakiwa kubadilika kimtizamo kulingana na nyakati

Upinzani wa Tanzania [emoji1241] ni upigania tumbo tu wala hawana jipya.
Chama kama Chadema kinapokusanya mashabiki na kuwahamasisha kwenda mahakamani Arusha kwenda kumzomea Sabaya kisa kumtuhumu alisimamia mbowe kukosa ubunge.Halafu Mbowe huyohuyo anaunda mtandao wa mwendesha mashtaka Kweka ambaye ni mkwe wake ,na kuhakikisha Sabaya anafungwa.

Zamu Inapomgeukia Mbowe na makomandoo wake, Chadema wote wanageukia huko na shughuli zao za chama zinasimama.wanasahau methali ya mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu.

Kisa mbowe ndie anazo akaunti zote za chama na bila yeye kusaini hata mishahara haitoki.
Bora wapigania tumbo kuliko wauaji, watekaji, wafirauni na wanafiki
 
Kuna vitu vingine sisi wengine tumeamua kukaa kimya. Kiukweli kabisa Tanzania, kwa huku bara, hatuna kabisa upinzani wa kweli na wa maana. Huu uliopo ni upinzani uchwala.

P
Mtoa hoja yuko sawa kabisa.
Hatuna vyama vyenye sera mbadala ili kushawishi umma kuwa vina nia ya kushika dola.

Wakati wa JK CDM walisifika kwa kuibua madudu yalikuwa serikalini hasa ufisadi ila hawakuwa na cha ziada nje ya kulaumu ufisadi. Huku mmoja wa viongozi akiwa bungeni alimtuhumu JK kuwa dhaifu

Alipoingia JPM akadhibiti ufisadi, wakaja na hoja mzee yule ni dikteta. Na hawakuwa hawakuwa na jipya.

Alipoapishwa Mama Samia kuwa Rais ilikuwa chereko kubwa sana kwao. Sasa hivi fungate limeisha.

China wana benevolence dictator na wahawana vyama vya upinzani ila wanasogea kimaendeleo kila kukicha.
Nchi za UAE, Bahrain, Oman, Saudia hawana kelele za demokrasia (japo wana uhitaji mkubwa kurekebisha kwenye haki za binadamu)
viwango vyao vya hali nzuri ya maisha ni bora kwa msingi wa kutumia rasilimali zao kujenga nchi zao.

ila bahati mbaya hata CCM kuna manyang'au wamo, watu wenye nia ya kutetea maslahi mapana ya wananchi huko nako wanapigwa vita.
Ni aibu kuwa taifa lenye wingi wa rasilimali kama Tanzania ila tunahangaika na masuala ya msingi, ikiwamo kutokuwa na uhakika wa kulima mazao msimu ambao mvua hazinyeshi kwa wakati huku tuna vyanzo vya maji kila pahala.

Bila shaka madam President atakuja na mkakati wa kujenga uchumi jumuishi ili Watanzania tuone neema ya kuishi kwenye nchi ya utele kama hii.
 
Tanzania bado hakuna chama pinzani ambacho Kiko serious ,hata hiki kinachojiita pinzani,hamna kitu ni njaa tu,wako biz na siasa za kutafuta ugali wa familia zao Basi.
 
Bora wapigania tumbo kuliko wauaji, watekaji, wafirauni na wanafiki
Mpigania tumbo anaweza fanya lolote sababu ya tamaa, ndio maana Mbowe alidiriki kumpuyanga Dk Slaa ili amuuzie chama Lowassa.

Wafirauni ni chadema na ndio maana Lissu alitetea ushoga live tena akiwa anapanda majukwaani na hata mbele ya Diaspora marekani na hata akihojiwa BBC.

Kwenye wauwaji Mbowe ni mmoja wao ndio maana alikuwa anao mpango wa kumuuwa Sabaya.
Na hatujasahau alivyomtumia Deus mallya kumuuwa Chacha Wangwe,na alipoenda Tarime msibani wananchi wakataka kumshambulia na aliokolewa na polisi kwa kumlaza chini ya pick up na kutoka nae nduki.
Mpaka wa leo mwambie akanyage Tarime kama atathubutu.
Tunajua mengi msiwe wepesi wa kuchonga midomo huku hamjui lolote.
 
Hivi hawa ndo braza Polepole alituambia kila mmoja ana V8 lake???
 
Kwahiyo unaona upinzani haufai kwasababu ukitoa hoja zako hawazikubali, kwani wewe ni nani mpaka kila hoja utakayotoa kwa wapinzani lazima ikubaliwe?

Tatizo lenu huwa mnalalamika wakati malalamiko yenu hata hayana sababu za msingi, hoja ya mtu kukubaliwa au kukataliwa ni jambo la kawaida kwenye demokrasia popote, naona huwa mnatumia mahaba ya "ukijani" wenu kulaumu upinzani ili mjifurahishe tu.

Muhimu kama unaona hoja yako ni ya maana sana na uliwapa halafu wakaikataa basi subiri vyama vyao vife uje kusema niliwaambia hawakunisikia, lakini uwaambie wakati ambao patakuwepo na usawa kwenye shughuli za vyama vya siasa Tanzania, sio kama ilivyo sasa wengine hawaruhusiwi kukutana ila mmoja anafanya atakavyo.
 
Naanza ku-declare interest Mimi ni Mwana Chama wa Chama Cha Mapinduzi kabisa ambaye sikupendezwa na jinsi Chama changu kilivyokuwa kikiyashughulikia Masuala mbali mbali Kwa Miaka kadhaa iliyopita na Mifano ipo.

Nikajikuta hasa kuna baadhi ya Mitizamo tunaendana kabisa na wenye sera mbadala ambao wanajulikana maarufu kama wapinzani,

Sikukubaliana na uminywaji wa Demokrasia si Kwa wapinzani tu bali hata kwa wanachama wa Chama chetu! Haikuishia hapo wakaanza hata kurekodiwa na kukagua hata meseji Kwa mtambo maalumu ambao kwa secret agreements ulinunuliwa kwa Mgongo wa Rwanda kuletwa nchini kipindi bado kagame hajamdhulumu Magufuli mambo kadhaa!

Tumelipigania hilo Kwa udi na Uvumba kabla yaa Kushinda vita Mungu akatushindia.

Sasa tukarudi kwenye msingi wa kuhoji yaliyo ya maana na mengine ya kupoteza Muda tukaachana nayo!

Nashangaa wapinzani wa Tanzania ukiwa na hoja mbadala yao wanaona we msaliti nawauliza ni wapi niliwai kutamka mimi ni mpinzani?

Katika masuala y’a Msingi lazima tukosoane, siku hizi Imekuwa kila kukicha mazungumzo kwenye Space huko twitter na action ni zero Imekuwa kama kikao cha soga!

Haijaisha topic moja na solution zake washadakia nyingine

Kinachoudhi zaidi Kuna Upotoshaji mwingi sana kwenye hoja za baadhi ya watu muhimu ndani ya Upinzani

Nimeangalia Sakata la Kesi ya Mbowe japo naamini siyo gaidi na hana uthubutu wa kufanya mambo y’a kigaidi ila wamekuwa ni wepesi Kumshambulia mtu yeyote anayeonekana kuwapa mawazo mbadala Au kuhoji jambo kuweka mambo sawa!

Tuanze ushahidi kutoka Tigo, wanasema Tigo hawakupaswa kutoa ushahidi, Seriously [emoji19]!

Someni Duty of Secrecy and exemption zake

Tusiwapotoshe wananchi wao wakaona Soln ni kuhamasisha kuvunja line, je na Voda wakitoa ushahidi na airtel mtahamia wapi?

Na Mashahidi wanaendelea kumiminika ama wa kutengenezwa Au wa kweli na wengine kuanzia week ijayo wanatoka Chama chake mtashangaa

Britanicca
Tabula Rassa
 
It's true, unajua hata CCM wanabadilika kila Utawala mpya unapoingia wao husoma upepo wa kiongozi aliyepo sasa upinzani lazima nao wajifunze kutembea na reli bila kuathiri malengo makuu ya vyama vyao.

Kwa maneno marahisi unasema wapinzani na wao wawe bendera fuata upepo kuendana na rais aliyeko kama ccm?
 
Hatukatai ila Basi Dawa mbadala ionekane kuleta Matumaini
Ndugu Kuna wakati mnanajisi maendeleo ya nchi yetu kwa makusudi kabisa,
Hoja ambayo ilikuwa inagombaniwa ni kwanini kampuni ya simu ya tigo kwenda kutoa ushahidi au kufanya uchunguzi au kutoa taarifa za mteja wake bila kufuata taratibu, kanuni na Sheria husika?

Je unaweza kutoa taarifa za mteja wako bila kuambiwa no kwanini hizo taarifa zinahitajika? Leo hii wewe ndugu Brita umekosana na jirani yako IGP then anaenda Tigo wampatie taarifa zako?
Ni kweli tuko serious na mada tunazozianzisha? tujitendee haki.
 
Kuna vitu vingine sisi wengine tumeamua kukaa kimya. Kiukweli kabisa Tanzania, kwa huku bara, hatuna kabisa upinzani wa kweli na wa maana. Huu uliopo ni upinzani uchwala.

P

Ni kweli kabisa upinzani huu ni uchwara, ila ili ccm imara ishinde ni lazima wizi wa kura ufanyike, ushenzi, ukatili na uhayawani. Sasa hapo unapimaje kuwa upinzani ni dhaifu, huku ccm imara haiwezi kushinda bila uhuni wa kitoto.
 
Hatukatai ila Basi Dawa mbadala ionekane kuleta Matumaini
Huko space unafuata nini? Mbona wapinzani hawafuatilii tena mijadala yenu huko bungeni, kwenye vipindi vya media ikiwemo radio, tv nk. Hivi majuzi kulikuwa na zoom meeting sijui ya mambo ya maendeleo, na rais alishiriki, umeona wapinzani wakitamani hata kushiriki?

Kulikuwa na mijadala huru kwenye vyuo, vipindi mbalimbali vya redio na runinga, huko kote mmezuia ili kuwe na mijadala iinayowafurahisha tu. Watu wenye mawazo mbadala wamejiongeza na kwenda sehemu nyingine kufanya mijadala yao maana hapa ndani mnataka msifiwe tu. Sasa hii mijadala ya kujisifia imekushinda, umeenda kurukia usiyoendana nayo. Nakushauri, baki kwa kutulia kwenye hii mijadala ya kusifia, sikiliza bunge maana ni la chama kimoja, huko utakutana na mijadala unayokubaliana nayo. Kinyume na hapo, kishauri chama chako kiachie mijadala kinzani hapa nchini kama ilivyokuwa, ili mpangue hoja kwa hoja.
 
Kwa ccm hii hapana!! Tunakoelekea nitachoma kadi badala ya kurudisha

Kwanini mumuonee mzee wa watu kisa siasa

Haitoshi mmeanza kumsema vibaya aliekirudisha chama relini

Endeleeni tu IPO siku.
 
Kuna maandishi umeyaruka either kwa makusudi au umeamua kutohusisha ubongo wako vizuri tu. Read between the lines nimeandika "bila kuathiri malengo makuu ya vyama vyao" waweza kuichambua hii statement kidogo utaelewa. Usitumie maneno marahisi kama ulivyosema dig in brother/sister.
Kwa maneno marahisi unasema wapinzani na wao wawe bendera fuata upepo kuendana na rais aliyeko kama ccm?
 
Kuna maandishi umeyaruka either kwa makusudi au umeamua kutohusisha ubongo wako vizuri tu. Read between the lines nimeandika "bila kuathiri malengo makuu ya vyama vyao" waweza kuichambua hii statement kidogo utaelewa. Usitumie maneno marahisi kama ulivyosema dig in brother/sister.

Ww ndio uko na making scheme nini?
 
Naanza ku-declare interest Mimi ni Mwana Chama wa Chama Cha Mapinduzi kabisa ambaye sikupendezwa na jinsi Chama changu kilivyokuwa kikiyashughulikia Masuala mbali mbali Kwa Miaka kadhaa iliyopita na Mifano ipo.

Nikajikuta hasa kuna baadhi ya Mitizamo tunaendana kabisa na wenye sera mbadala ambao wanajulikana maarufu kama wapinzani,

Sikukubaliana na uminywaji wa Demokrasia si Kwa wapinzani tu bali hata kwa wanachama wa Chama chetu! Haikuishia hapo wakaanza hata kurekodiwa na kukagua hata meseji Kwa mtambo maalumu ambao kwa secret agreements ulinunuliwa kwa Mgongo wa Rwanda kuletwa nchini kipindi bado kagame hajamdhulumu Magufuli mambo kadhaa!

Tumelipigania hilo Kwa udi na Uvumba kabla yaa Kushinda vita Mungu akatushindia.

Sasa tukarudi kwenye msingi wa kuhoji yaliyo ya maana na mengine ya kupoteza Muda tukaachana nayo!

Nashangaa wapinzani wa Tanzania ukiwa na hoja mbadala yao wanaona we msaliti nawauliza ni wapi niliwai kutamka mimi ni mpinzani?

Katika masuala y’a Msingi lazima tukosoane, siku hizi Imekuwa kila kukicha mazungumzo kwenye Space huko twitter na action ni zero Imekuwa kama kikao cha soga!

Haijaisha topic moja na solution zake washadakia nyingine

Kinachoudhi zaidi Kuna Upotoshaji mwingi sana kwenye hoja za baadhi ya watu muhimu ndani ya Upinzani

Nimeangalia Sakata la Kesi ya Mbowe japo naamini siyo gaidi na hana uthubutu wa kufanya mambo y’a kigaidi ila wamekuwa ni wepesi Kumshambulia mtu yeyote anayeonekana kuwapa mawazo mbadala Au kuhoji jambo kuweka mambo sawa!

Tuanze ushahidi kutoka Tigo, wanasema Tigo hawakupaswa kutoa ushahidi, Seriously 😒!

Someni Duty of Secrecy and exemption zake

Tusiwapotoshe wananchi wao wakaona Soln ni kuhamasisha kuvunja line, je na Voda wakitoa ushahidi na airtel mtahamia wapi?

Na Mashahidi wanaendelea kumiminika ama wa kutengenezwa Au wa kweli na wengine kuanzia week ijayo wanatoka Chama chake mtashangaa

Britanicca

Naona unatishia hapo paragraph ya mwisho kuwa kuna mashahidi toka mpaka kwenye chama chake. Acha mashahidi wa kwenye chama chake, achukuliwe mpaka mke wake na watoto wake wawe upande wa jamuhuri, lakini bado tunajua sio gaidi zaidi ya siasa chafu. Hayo mambo ya ushahidi wa siasa chafu tuliona wapinzani wote walionunuliwa na ccm wakisema maneno hayo hayo. Akina Lijualikali mpaka bungeni walilia na kutoa maelezo mliyoyotaka, na leo mmewapa vyeo kwa kazi yao.

Lakini pamoja na hizo siasa zote chafu dhidi ya Mbowe na cdm, ilibidi uchaguzi uvurugwe kwa kiwango kisichopata kuonekana, ili ccm watangazwe washindi kwa shuruti. So nothing new toka kwenye hao mashahidi wa kutengenezwa.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Wawatoe lupango wote waliowambakia kesi FEKI na kurudisha billions kama siyo trillions zikiwemo nyumba, viwanja, magari na pesa walizowapora Watanzania mbali mbali kila kona nchini

Futeni Kesi za uongo
 
Back
Top Bottom