Uchaguzi 2020 Sitampa kura yangu Dkt. Magufuli kwa sababu hii 'kubwa'

Yani nikimpigia kura Magufuli basi wakati narudi kutoka kituo cha kupigia kura nipate ajali NIFE! Sitathubutu hata nikishikiwa bunduki.
 
Naomba nimnukuu Wakili msomi Fatuma Karume anashangaa na kustaajabu watu ama wananchi wanapompigia magoti raisi ili hali wao ndio wanamuajiri kwa kumpigia kura yaani kumchagua atuongoze.
Fatuma yuko vizuri sana yule dada maana mazingira yaliyo mfikisha hapo alipo ni urais sasa ukimuona mtu kama huyo anakosoa urais basi huna budi kukubali mchango wake
 
Kama hamukuiong'oa CCM madarakani mwaka 2015 Mwaka huu jiandae kisaikolojia mtaishia kupata Kura za huruma tuuuuu
 
Wapiga dili mmevumilia mpaka mmeona mtoe povu. Mlizoea kuzichota, sasa hamna mwanya mnatapatapa.

Kura yako hiyo moja haiwezi kumnyima ushindi. Kwanza inaweza kuwa ni kati ya zile zinazoharibika.
Naona unaongea bila kuushirikusha ubongo wako, huyo mleta uzi nani asiye mjua kuwa ni mpigania chama na ni mmoja wa kiongozi ndani ya ccm.

Wewe na ujinga wako unamuona kama mgeni au mpinzani ndani ya chama?

Hata akiweza kuwashawishi watu 100 tu kutompigia kura mgombea wenu litakuwa ni pigo kwenu pia.

Jitahidi kutumia muda angalau akili zako zihusike kwenye maamuzi yako
 
Kura yako ingekuwa ni ya Turufu hii ingekuwa ni shocking news.
 
Akiandika ukweli ule mchungu ukawii kulaumu, napata wakati mgumu kujua wafuasi wa upinzani wanasimamia wapi linapokuja suala la maslahi mapana ya nchi na yenye tija kwa vizazi vijavyo
Ktk nchi hii bila kuwepo na mawazo mbadala ya wapinzani leo hii mgekuwa mnalipishwa hata kodi ya kichwa.

Bila waoinzania mgekuwa mnalazimishwa kwenda kuupokea mwenge kwa lazima.

Kuweni na shukrani basi hata kama hamna tabia za kushukuru
 
Hii pia ni sababu ya anguko la Magufuli, ile kujifanya bila yeye mambo hayaendi. Yaani anataka kujipa umungu angali yeye ni binadamu. Eti kwamba bila yeye mambo hayaendi.

Wananchi wajumbe tutaongea kwa sauti moja
Mungu awabariki sana wajumbe maaana nyinyi ndiyo wenye maamuzi ya kuinusuru nchi yetu.
 
Ubarikiwe sana mkuu huo ndiyo uamuzi wa kizalendo
 
Shida sana kada wa Chadema anapofanya maigizo kama kada wa CCM.
Wewe kweli ni mgeni hapa jf, kama leo hii unamwambia Mzee mwana kijiji kuwa ni cdm[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa hiyo utampigia nani? Membe au yule mwenye damu ya wakenya mwilini mwake?
 
Hata usipompigia kura bado watanzania wengine kwa wingi watampigia kura. Tupatupa wakati wa kwenda pale Lumumba kupewa fedha za bure umekwisha.
Mkuu Rais Magufuli ndio kiongozi pekee jasiri aliyetokea kutaka kuleta mabadiliko za kiuchumi sio waliomtangulia walibaki kupiga dili. Tufunge mikanda kwa hali hii ila ninauhakika Rais Magufuli atatuvusha kuelekea uchumi imara Africa Mashariki na Kati
 
Mkaonyeshe vitendo sio muandike tu

siku ya kupga kura mjifungie ndani mkichat
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…