- Thread starter
- #61
Kuna mtu kakalazimisha kusomaWe jamaa muongo unachukua uko story za vitabu unakuja na huku kutuadithia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna mtu kakalazimisha kusomaWe jamaa muongo unachukua uko story za vitabu unakuja na huku kutuadithia
Punguza uongo basKuna mtu kakalazimisha kusoma
Sawa dogoPunguza uongo bas
Una dharau za lejeleja dahSawa dogo
Kwa sababu tu sina njaa kama za akina ROBERT HERIEL nikilitakiwa niwaombe muchangie kachochoteIla imeanza kufurahisha bna, hongera sana mtunzi.
....Jingazz....SEHEMU YA 2
Nilimuambia yule boda atembee mwendo wa kuruka, nae hakuniangusha ndani ya dakika kumi tukawa tayari tuko nje ya lango la Bank.Nikazama mfukoni fast nikampa chake huyooo akasepa zake, kwenda kusaka vichwa vingine vya mwisho mwisho vya kufungia hesabu.
Nikatabasamu,tabasamu langu ambalo huwa natabasamu nikiwa na furaha ya kweli kutoka moyoni.
Nikawaza laiti kama huyu boda angejua mteja aliyemleta amekuja kuchota kiasi gani cha pesa, angebana pahali asubirie angalau kama anaweza pata kamgao japo kiduchu kuliko kujihangaisha kusaka buku buku ambazo hata akizipata atalazimika kuzigawana kama sio na boss wake basi atazigawana na mwenye kituo cha mafuta au mmiliki wa gereji & duka la spea za pikipiki
Nikaanza kufanya survey mazingira ya Bank kuangalia kama yako salama na yanaruhusu kupiga tukio lililonileta.Kwa sababu ilikuwa bado saa 3 usiku kulikuwa na wateja ambao walikuwa wakichukulia pesa kwenye ATM tena siku hiyo walikuwa wengi kidogo tofauti na siku zingine kwani mchana network ilishinda ikisumbua
Nikawaona police wawili wa kiume ambao nilijua ndio walinzi wa siku hiyo,nikaangalia sale zao zilizowabana kiasi cha kushindwa hata kurusha teke endapo itahitajika wafanye hivyo,nikaona jinsi walivyo eneo la wazi kabisa kiasi cha hata jambazi mwenye mishale anaweza kuwadondosha wote wawili ndani ya ½ dakika,nikatazama bunduki walizozibeba begani kama mabegi,nikaona jinsi wanavyowatolea macho watu wanaokuja kutoa pesa kwenye ATM huku wakijaribu kulazimisha mazoea na kufahamiana na baadhi yao ili wapatiwe kachochote, nikatabasamu tena kwa mara ya pili,tabasamu la dharau,eti hawa ndio leo wanalinda jengo la Bank,jengo lililohifadhi mamilioni kama sio mabillion ya pesa za watu.Kweli watanzania hatuko serious,unajaza pesa kwenye jengo chakavu kama hili halafu nje unawaweka matozi tena wawili tu wakulindie.Nchi yenye zaidi ya watu hai milioni 60 inakosa vijana majasiri,wenye misuri wanaoweza kulinda bank mpaka tunawaachia kazi hiyo matozi watufanyie
Nikaanza kuwaza namna nitakavyofungua milango ya Bank na kuzama ndani bila kushtukiwa na hawa police au wananchi wenye kiherehere waliobatizwa jina la kizuzu la raia wema,nikawaza namna nitakavyotoka na kutoweka na begi/mabegi ya hela bila kushtukiwa na yeyote
Nikaangalia odds za kufanikiwa kuingia na kutoka salama ziko 50/50.
Nikawaza tena, nikikamatwa itakuaje.
Je,nitapigwa na wananchi wenye hasira kali kisha kuchomwa moto kama wanavyofanyiwa hawa wezi wa simu,pochi & kuku waliobatizwa jina la vibaka
Nikawaza,je nitauwawa na hawa police halafu baadae waseme lilitunyooshea mkono tukafikiri ni bunduki, tukalimiminia risasi 30 kifuani kwa bahati mbaya limekufa wakati likikimbizwa kwa bodaboda hospitalini
Nikawaza,je nitapelekwa mahakamani ambako naweza kuchezea kifungo cha mpaka miaka 15 gerezani na kazi ngumu endapo nitapatikana na hatia.
Sijui nini kilitokea hili wazo la kukamatwa na kufungwa lilininyongonyeza sana tofauti na mawazo mengine.Nadhani lilininyongonyeza zaidi kwa sababu mazingira ya magereza ya Tanzania nayafahamu vyema.
Jela za Tanzania ni ½ ya jehanamu,sio salama kwa mtu kama mimi kupageuza makazi hata kwa ½ siku,nitateseka kama sio kupata taabu sana huku nikiwaachia wengine starehe za Dunia ambazo kila kukicha zinazidi kuongezeka.
Nikaanza kuwawaza wadada wazuri ambao kila siku wanazariwa kwaajili yetu sisi wanaume marijali,nikawaza kuhusu bia,k-vant & nyama choma za ng'ombe,mbuzi,kuku & nguruwe ambae kutokana na utamu wake amebatizwa majina rukuki kama kitimoto,mkuu wa meza,mbuzi katoliki nk nk
Nikawaza kuhusu kumbi & hoteli nzuri nzuri za kisasa za starehe zinazojengwa kila kukicha kwaajili ya vijana kama sisi kufanyia starehe zetu.
Nikawaza hivi vyote nitalazimika kuviacha endapo nitakamatwa na kupigwa mvua za kutosha gerezani kama alivyolazimika kuviacha msanii Nguza Viking & mwanae Papii Kocha baada ya kusainishwa mkataba wa kuishi jela maisha yao yote kutokana na kupatiwa kesi ya mchongo iliyosababishwa na kula wanavyokula wakubwa
#saliiima
Miaka kumi zaidi ya 15 iliyopita nilikaa gerezani kwa miezi michache lakini kwa taabu nilizozipata
niliona kama nimekaa miaka makumi matatu.
Eti leo ndio nirudi gerezani na kukaa zaidi ya miaka 10 kwa sababu ya tamaa ya pesa.Pesa kitu gani,pesa ambazo nimewashuhudia watu wakifa na kuziacha
pesa ambazo zilisababisha Yuda Isakariote ajitoe uhai mwenyewe baada ya kumfanyia usinichi msela wake wa kufa na kuzikana(Yesu mnazareti)
pesa ambazo serikali ikizihitaji inaweza kukukwapua tena kwa wewe mwenyewe kulazimisha makubaliano na DPP kama walivyofanyiwa SingaSinga wa IPTL na muhuni mmoja aliyeamua kuachana na jina alilopatiwa na wazazi wake kisha kujiita Mr kuku.
Pesa ambazo zinaweza kushuka thamani muda wowote na kurudia thamani yake halisi ya karatasi pindi imani ya watumiaji wake itakapoondoshwa kutokana na vikwazo kutoka kwa wakubwa wa Dunia kama ilivyozitokea nchi za Zimbabwe,Argentina & Venezuela.Pesa ambazo unaweza tapeliwa kirahisi kama walivyotapeliwa wale nyumbu wa Ontario walioahidiwa kupatiwa uwezo wa kudownload pesa namna ya wanavyoweza kudownload video & files nyingine mtandaoni.
Pesa,pesa ambazo unaweza kutapeliwa kwa kutumiwa sms fupi tu ya "ile pesa tuma kwenda namba 07****,jina litakuja Mabala Maburu"
Hapana siwezi kurudi gerezani kwa sababu ya tamaa ya pesa,tena pesa zenyewe za mchongo za kuchotwa na kuwekwa kwenye begi
Nikayakumbuka maisha yangu gerezani, mambo niliyoyaona kwa macho yangu mawili na kuyasikia kwa masikio yangu mawili makubwa.
Nikamkumbuka Nyamkina, mwanaume kibailojia lakini alikuwa anagawa tako kwa mfungwa yeyote mwenye kijizawadi cha kumpatia
nikakumbuka jinsi alivyokuwa akiturembulia macho yake makubwa sisi wanaume wenzie,nakiri kweli alikuwa amejaariwa macho mazuri makubwa meupe yanayotamanisha
Nikakumbuka jinsi alivyokuwa akizungukwa na watu kama malkia pindi akienda kuoga bafuni.Nikakumbuka siku moja alipoamka akiwa kajinyea kwani mishipa yake ya mkund*** ilikuwa imeregea sana kutokana na kuzidiwa na mzigo wa mikuyange ya kila namna iliyokuwa ikiingizwa humo kwa msaada wa kilainishi cha asiki(mate) na mabaharia wasiojali kitu
Nikakumbuka jinsi habari za vifo vya wafungwa waliohamishiwa kwenye gereza la kilimo zilivyokuwa zikiwafanya wafungwa kusali sana na wao wasije wakaamishiwa kwenye gereza la kilimo
Nikakumbuka story ya mjela jela maarufu ambae mwaka 1997 alimchinja na kumla paka kutokana na kuzidiwa njaa,njaa iliyosababishwa na bakuri/full moja ya ugali kuliwa na mijibaba mitano tena kwa kugombania
Nikamkumbuka mfungwa X aliyekuwa akifanya biashara ya chapati anazoziingiza gerezani kwa kuzificha kwenye gambuti
Nikamkumbuka rafiki yangu Deo aliyevunjika mkuu wakati akipigana na mfungwa mwenzake kugombania ndizi 2 mbivu
Nikakumbuka siku nilipopigwa rungu na daktari wa gereza baada ya kugoma kupokea dawa zilizokuwa zimeexpire alizokuwa amenipatia kama matibabu ya maralia iliyokuwa imenikaba vilivyo
Nikajiambia moyoni, hapana huwezi kurudi gerezani kiboya boya namna hii.
Nikazama mfukoni kuangalia kama zile funguo bado zimo,eeh zimo nikajipa ujasiri kuwa sitakamatwa wala kushtukiwa na mtu yeyote endapo nikiwa makini wakati wote wa hili zoezi la hatari la kuchota pesa za mchongo.
Nikajiambia kwa kujiamrisha "Lazima uzame bank kuchota pesa"
Itaendelea.....
🐒....Jingazz....
Ila imeanza kufurahisha bna, hongera sana mtunzi.
Babu kuingia kuingia Benk kuna funguo zaidi ya 3 zinakaa na watu tofautitofauti, koroga tena hii chai haijakorea sukari!!!Ilikuwa ni siku ya Jumanne tarehe 14 mwezi May mwaka 2019 nilipookota funguo bar zilizoachwa na bwana mmoja ambae alionekana kuzidiwa na pombe.
Yule bwana niligundua kuwa alikuwa ni manager wa bank kwani kuna wakati nilisikia akipiga simu na kutoa maelekezo fulani fulani kwa watu ambao nahisi walikuwa ni wafanyakazi wa chini yake.
Nilitaka nimuwahi nje nimpatie funguo zake lakini wazo lingine likaniambia acha ushamba hujaja mjini kuhesabu mijighorofa wala kupiga picha na kuziweka insta.
Fasta nikalipia kinywaji nilichokunywa,nikatoka nje nikaita boda huyooo moja kwa moja mpaka bank kuchukua hela, hela za kujichotea
Itaendelea. . . .
'Sehemu ya pili' Sitasahau siku nilipootea begi la hela Bank na kushindwa kuzitumia
Hahahah umefeli mpaka hapo na huu utoto usituletee huku peleka FacebookIlikuwa ni siku ya Jumanne tarehe 14 mwezi May mwaka 2019 nilipookota funguo bar zilizoachwa na bwana mmoja ambae alionekana kuzidiwa na pombe.
Yule bwana niligundua kuwa alikuwa ni manager wa bank kwani kuna wakati nilisikia akipiga simu na kutoa maelekezo fulani fulani kwa watu ambao nahisi walikuwa ni wafanyakazi wa chini yake.
Nilitaka nimuwahi nje nimpatie funguo zake lakini wazo lingine likaniambia acha ushamba hujaja mjini kuhesabu mijighorofa wala kupiga picha na kuziweka insta.
Fasta nikalipia kinywaji nilichokunywa,nikatoka nje nikaita boda huyooo moja kwa moja mpaka bank kuchukua hela, hela za kujichotea
Itaendelea. . . .
'Sehemu ya pili' Sitasahau siku nilipootea begi la hela Bank na kushindwa kuzitumia
Ngoja ifike mwisho ndio utajua kama hujuiHata bongo movie hawawezi kutunga utumbo huu
Ngoja nifuate sukari hapa dukani kwa mangi,wewe tulia na 😹hapo sebuleni kwa shemejiBabu kuingia kuingia Benk kuna funguo zaidi ya 3 zinakaa na watu tofautitofauti, koroga tena hii chai haijakorea sukari!!!
Usihofu najaribu kupunguza mambo mengine ili JF wasijenipiga lifeban plus kuniuza kwa mapolisi uchwaramkuu mi nasubiria hadi nione mwisho utakuwaje...