Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kipimo kikuu cha akili na ustaarabu wa binadamu yeyote yule ni namna anavyopangilia maeneo yake anayoishi na kufanya shughuli zake.
Haijalishi kama anajenga nyumba za kitajiri au za kimaskini ila namna gani alivyopima na kupangilia makazi yake ndicho kielelezo pekee kinachoweza kukwambia kuwa huyu binadamu ana akili sawa na amestaarabika kweli.
Nchi ya Tanzania imeharibiwa na watu wengi sana!
Ila tukisema leo tufanye uchambuzi hakuna watu waliochangia kuiharibu hii nchi na kuifanya kuwa ya hovyo kama Viongozi wa Serikali za Mitaa na Wizara ya Ardhi.
Kipimo kikuu cha uharibifu wa Tanzania ni namna ilivyojengwa hovyo na inavyozidi kujengwa hovyo bila mpangilio wowote ule.
Sababu kuu zilizopelekea hii nchi yetu kujengwa hovyo kwa uchafu bila mpangilio ni Wizara ya Ardhi na watu wanaoitwa Viongozi wa Serikali za Mitaa.
Wizara ya Ardhi kama Wizara ambayo ina jukumu la kupima na kupanga maeneo yote nchi hii na kuhakikisha wananchi wote wa nchi hii wanaishi katika maeneo yaliyopimwa na kupangwa vizuri haifanyi hilo jukumu lake la msingi kisawasawa. Badala yale Wizara hii imekuwa ikihangaika kila aiku kushughulikia migogoro ya ardhi ambayo ukitizama kama una akili nzuri migogoro hiyo inasababishwa na tatizo kuu la wao kutotimiza wajibu wao wa kupima na kupanga maeneo ya nchi hii.
Tukija kwa Viongozi wa Serikali za mitaa hawa ndo mashetani wanaofanikisha matokeo ya ujinga unaofanywa na Wizara ya Ardhi.
Hawa kwa miaka mingi ndo wamekuwa wakisimamia uuzaji na ugawaji wa maeneo bila kuzingatia uwepo wa barabara, maeneo ya wazi, pamoja na maeneo ya shughuli za kibinadamu.
Maeneo yote yaliyojengwa hovyo nchini Tanzania katika mikoa mbalimbali wanaosimamia uuuzwaji na ukatwaji holela wa viwanja kwenye maeneo hayo bila kuwaelekeza na kuwasimamia wananchi vizuri katika kuacha barababra za kupita magari na vyombo vya moto ni Viongozi wa Serikali za Mitaa.
Leo hii ukitembea mikoa ya Tanzania kama Mwanza, Arusha,Dar es Salaam, Mbeya, Manyara na kwingineko ni kama unapita katika jalala kwa namna makazi ya wananchi yalivyojengwa hovyo bila mpangilio.
Wizara ya Ardhi ambayo ingepaswa hata kutoa mwongozo wa ujengwaji wa nyumba na uuzwaji wa maeneo kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa kutokana na kushindwa kusimamia ipasavyo zoezi la upimaji na upangwaji wa nchi hii nayo imeshindwa kutoa huo mwongozo na kupelekea nchi yetu hii leo hii kuwa kama takataka.
Mbaya zaidi huwezi badilisha chochote kwenye haya kwa njia ya uchaguzi maana hapa Tanzania uchaguzi umeshahodhiwa na kikundi cha watu wachache ambacho ndicho kinateua watu wanaofanya haya. Hawajali umemchagua nani ila wanachagua wenyewe mtu wanayemtaka wao na hao wanaowachagua ndo wanafanya haya.
Mungu ananiona. Nisije tu kuwa Rais wa Nchi hii ila kuna uwezekano nikija kuwa Rais nikawafunga watu wote waliowahi kuwa Viongozi wa Serikali za Mitaa na Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi bila kusahau waliowahi kuwa Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Ardhi.
Lord denning
Qatar