Sitashiriki kamwe chaguzi yoyote nchini Tanzania kwa sababu ya Viongozi wa Serikali za Mitaa na Wizara ya Ardhi

Sitashiriki kamwe chaguzi yoyote nchini Tanzania kwa sababu ya Viongozi wa Serikali za Mitaa na Wizara ya Ardhi

Kila mtu na fikra zake kuna mwingine anafikiria akipata nafasi viongozi wote na wanachama wa CCM akina mwashambwa baadhi unawafirisi na kuwafunga wengine unawaua kabisa.
Hata mie naweza fanya hivyo
 
Mungu alishasema msipomuimbia yy mawe nayo yataimba, kwahyo tutapiga Kura ss kwa niaba yako
 
Mfano hai Nkuhungu broad acre Dodoma
Eneo lilikuwa limepangwa kwa ustadi Mkubwa sana
Mabadiliko yalitakiwa yafanywe kitaalam
Lakini kilichofanyika ni aibu ya aibu

Rushwa rushwa kutumia tume kibao za kuthibiti vibaka waliotengenezwa kisiasa kupitia wataalamu wezi wezi
Dodoma njia ya Iringa baada ya Stesheni ya SGR kuna uchafu umeibuka wa ujenzi holela hadi unatia aibu.

Ukija huku ihumwa, mtumba hadi uelekeo wa chamwino ni vituko vitupu.

Unajiuliza kama waliweza kupanga Ilazo na kisasa wameshindwaje kupanga chamwino na mtumba uelekeo wa ikulu unabaki unashangaa tu hupati majibu. Na hapo ni Dodoma jiji jipya ambalo Serikali walisema kila kitu kitakuwa sawa na litakuwa jiji la mfano.

Hii nchi tuna shida kubwa kuliko ile tunayofikiri tunayo kwa kweli. Matumizi ya akili ni jambo adimu sana na linaanzia kwenye Katiba mbovu inayowanyiwa wananchi kupata viongozi wanaowataka wao badala yake inawapa Viongozi waliochaguliwa na kikundi cha watu wachache
 
Kipimo kikuu cha akili na ustaarabu wa binadamu yeyote yule ni namna anavyopangilia maeneo yake anayoishi na kufanya shughuli zake.

Haijalishi kama anajenga nyumba za kitajiri au za kimaskini ila namna gani alivyopima na kupangilia makazi yake ndicho kielelezo pekee kinachoweza kukwambia kuwa huyu binadamu ana akili sawa na amestaarabika kweli.

Nchi ya Tanzania imeharibiwa na watu wengi sana!

Ila tukisema leo tufanye uchambuzi hakuna watu waliochangia kuiharibu hii nchi na kuifanya kuwa ya hovyo kama Viongozi wa Serikali za Mitaa na Wizara ya Ardhi.

Kipimo kikuu cha uharibifu wa Tanzania ni namna ilivyojengwa hovyo na inavyozidi kujengwa hovyo bila mpangilio wowote ule.

Sababu kuu zilizopelekea hii nchi yetu kujengwa hovyo kwa uchafu bila mpangilio ni Wizara ya Ardhi na watu wanaoitwa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Wizara ya Ardhi kama Wizara ambayo ina jukumu la kupima na kupanga maeneo yotw nchi hii na kuhakikisha wananchi wote wa nchi hii wanaishi katika maeneo yaliyopimwa na kupangwa vizuri haifanyi hilo jukumu lake la msingi kisawasawa. Badala yale Wizara hii imekuwa ikihangaika kila aiku kushughulikia migogoro ya ardhi ambayo ukitizama kama una akili nzuri migogoro hiyo inasababishwa na tatizo kuu la wao kutotimiza wajibu wao wa kupima na kupanga maeneo ya nchi hii.

Tukija kwa Viongozi wa Serikali za mitaa hawa ndo mashetani wanaofanikisha matokeo ya ujinga unaofanywa na Wizara ya Ardhi.

Hawa kwa miaka mingi ndo wamekuwa wakisimamia uuzaji na ugawaji wa maeneo bila kuzingatia uwepo wa barabara, maeneo ya wazi, pamoja na maeneo ya shughuli za kibinadamu.

Maeneo yote yaliyojengwa hovyo nchini Tanzania katika mikoa mbalimbali wanaosimamia uuuzwaji na ukatwaji holela wa viwanja kwenye maeneo hayo bila kuwaelekeza na kuwasimamia wananchi vizuri katika kuacha barababra za kupita magali na vyombo vya moto ni Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Leo hii ukitembea mikoa ya Tanzania kama Mwanza, Arusha,Dar es Salaam, Mbeya, Manyara na kwingineko ni kama unapita katika jalala kwa namna makazi ya wananchi yalivyojengwa hovyo bila mpangilio.

Wizara ya Ardhi ambayo ingepaswa hata kutoa mwongozo wa ujengwaji wa nyumba na uuzwaji wa maeneo kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa kutokana na kushindwa kusimamia ipasavyo zoezi la upimaji na upangwaji wa nchi hii nayo imeshindwa kutoa huo mwongozo na kupelekea nchi yetu hii leo hii kuwa kama takataka.

Mungu ananiona. Nisije tu kuwa Rais wa Nchi hii ila kuna uwezekano nikija kuwa Rais nikawafunga watu wote waliowahi kuwa Viongozi wa Serikali za Mitaa na Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi bila kusahau waliowahi kuwa Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Ardhi.

Lord denning

Qatar
Ukisusia uchaguzi tatizo litakua limeisha?
 
Mkuu, ukiamka, tutakupa elimu ya haya mambo, wizara ardhi imegatua sana, ukiona uharibifu, basi wanafanya washkaji zako hapo mtaani
Unipe elimu gani mkuu wangu?

Kipi cha maana kinachofanywa na hao Wizara ya Ardhi? Zaidi ya kula posho tu na kuhalalisha ujenzi holela usio na mpangilio kila siku?

Kielelezo kuwa nchi hii hatuna Wizara ya Ardhi ni maeneo mapya hapo Jiji kuu la Biashara Dar es Salaam.

Kama wangekuwa wanajua walifanya makosa huko nyuma basi wangewela nguvu kwenye maeneo mapya hapo Dar es Salaam kwa kusimamia yapangwe na kujengwa kwa mpabgilio. Ila nenda kimara, mbezi, Kinyerezi, kibamba, mapwepande, Pugu, Chanika, Kigamboni uone Jiji linavyozidi kuwa uchafu kwa ujenzi holela na wa hovyo!
 
Ukisusia uchaguzi tatizo litakua limeisha?
Huwezi kuondoa uchafu uliopo nchi hii kwa njia ya uchaguzi. Labda watokee wenye akili huko TISS waseme basi kuwabeba CCM kwenye chaguzi
 
Huwezi kuondoa uchafu uliopo nchi hii kwa njia ya uchaguzi. Labda watokee wenye akili huko TISS waseme basi kuwabeba CCM kwenye chaguzi
Siku watanzania tukiamka usingizini,na kuacha upumbavu tutajipata tuko huru. Shida tumekua taifa la kulalamika tu bila kuchukua hatua.
 
Well said mkuu, kungekuwa hakuna limitation ya like ninge gonga like 1000.

Ukipita mitaani tena maeneo ya karibu kabisa na mijimikuu yetu alafu ukafanya tathmini ya jinsi watu walivyo Jenga kiholela unaweza kusema ni mji wa majuha.

Viongozi wa mitaa na wizara ya ardhi hawajui majukumuyao ya msingi na kwabahati mbaya sana sijui huu ushenzi na ujinga utaishia lini, hii nchi ni maudhi kila mahali.

Rushwa, ujinga,kujuana,ubinafsi na uwoga ndio chanzo cha haya yote.
 
Nilishawahi andika uzi humu. Kwa ufupi kwa namna nchi yetu ilivyojengwa hovyo hovyo ni kama hatujawahi kuwa na Wizara ya Ardhi nchini.

Tanzania ni kielelezo namba moja cha ujuha wa mtu mweusi
 
One of the penalties of refusing to participate in politics is that,
You will end up being governed by your inferiors.
 
One of the penalties of refusing to participate in politics is that,
You will end up being governed by your inferiors.
Nchi hii tuombe tu mazeeta ya JW na TISS yaje kuamka kutoka usingiz wa pono na kupata akili. Hapo ndo pona ya Watanzania itakapofika.

Otherwise kila mtu abaki na masimamo wake!
 
Hoja kubwa.ni kuzorota kwa uapatikanaji.wa.maji. ujenzi wa.hovyo.wa.mwendokasi unaoleta.maafa.ya.ajali kila.siku.badala ya.kupanua. barabara wao.wanaziminya
 
CCM ana njia mbili tu za kuondoka Madarakani!
1. Maandamano yatakayoitishwa na Viongozi wa Dini.

2. Mapinduzi ya Kijeshi au siku TISS akiamua basi hawabebi tena kwenye sanduku la Kura.

Vinginevyo haya yote tunayoita uchaguzi ni maigizo ya mtu mweusi kwenye sanduku la kura!
Kwa hiyo kwa upande wako umehitimisha kuwa wananchi hawawezi kufanya lolote bila ya hizo dini, jeshi au hao "usalama" wa CCM?
Hilo la viongozi wa dini kusimamia kazi hiyo sijui wazo hilo umelitoa wapi?
Jeshi wenyewe wamedhibitiwa na CCM hao hao; viongozi wao wote ni CCM!

Kinacho kosekana kwa muda mrefu, ni kiongozi; ndiyo nasema kiongozi mmoja tu anaye eleweka na wananchi, basi. Akipatikana kiongozi huyo, wananchi wenyewe wataimaliza kazi upesi sana; na mahali pa kuanzia; sababu ikiwa ni uchafuzi wa uchaguzi kama hivi inavyo fanyika sasa.
 
Magufuli ni rais bora wa karne ya 21, nimeliona hili baada ya kutembelea SGR na bwawa la umeme
Da kweli umeona ukatamka. Ungeishi enzi za Hitler yule ungemuita mtukufu mana alijenga zaidi ya hayo uliojionea kwa Magufuri, umejaliwa kwa macho ya kuona hivi
 
Kwa hiyo kwa upande wako umehitimisha kuwa wananchi hawawezi kufanya lolote bila ya hizo dini, jeshi au hao "usalama" wa CCM?
Hilo la viongozi wa dini kusimamia kazi hiyo sijui wazo hilo umelitoa wapi?
Jeshi wenyewe wamedhibitiwa na CCM hao hao; viongozi wao wote ni CCM!

Kinacho kosekana kwa muda mrefu, ni kiongozi; ndiyo nasema kiongozi mmoja tu anaye eleweka na wananchi, basi. Akipatikana kiongozi huyo, wananchi wenyewe wataimaliza kazi upesi sana; na mahali pa kuanzia; sababu ikiwa ni uchafuzi wa uchaguzi kama hivi inavyo fanyika sasa.
Hapana! Wananchi wa nchi hii ni mandezi sana. Mwanga umeanza kuonekana kwa Viongozi wa dini na hawa ndo watu wanaoweza kusema tuandamane na wananchi wakawafuata nyuma.

Kuhusu Jeshi na TISS hawa ni watu ambao wana nguvu ila bado wanaogelea kwenye bwawa la ujinga hawajajua maana ya nguvu zao ndo mana wanasiasa wanachezea kama vi toy.

Nguvu ya CCM ni vyombo vya dola na siku vyombo vya dola vikisema NO hicho chama ni wepesi zaidi ya toilet paper.

Kwenye nchi ambazo wanasiasa wana nidhamu kweli kwa Wananchi, vyombo vya ulinzi vilishaamua kujitenga na ujinga na upoyoyo wa wanasiasa
 
Hapana! Wananchi wa nchi hii ni mandezi sana. Mwanga umeanza kuonekana kwa Viongozi wa dini na hawa ndo watu wanaoweza kusema tuandamane na wananchi wakawafuata nyuma.
Sijasoma hayo mengine huko chini umeeleza nini, lakini hili la "viongozi wa dini" ni dhahiri kabisa kuwa hiyo kazi hawawezi kuifanya wala kuisimamia ifanyike.
Kwanza hao ni nani; maaskofu Katoliki? Hawa wanachoweza kufanya ni kukemea tu na kuonya, basi! Kwanza wewe hata huoni hao viongozi wengine wa dini walivyo tulia, na wengine wakiwapinga moja kwa moja hao maaskofu? Na siyo ajabu, hata huko miongoni mwa maaskofu wenyewe kuna wanao thamini zaidi zawadi (rushwa) zinazo tolewa kwao na Samia mwenyewe; kwamba hawawezi kuwa na sauti moja kupinga CCM.

"Wananchi wa nchi hii ni mandezi sana"? Unawalaumu wasio stahili lawama hapa.
 
Kuhusu Jeshi na TISS hawa ni watu ambao wana nguvu ila bado wanaogelea kwenye bwawa la ujinga hawajajua maana ya nguvu zao ndo mana wanasiasa wanachezea kama vi toy.
Kwani wewe unadhani CCM hawajui jinsi ya kuwaweka walipo? Tatizo ni la kupigania maslahi binafsi kila mahali. Kuna siku na wakati kutajitokeza kundi linalo jali maslahi ya taifa hili zaidi. Sasa hilo hatujui litatokea lini.
Inawezekana ikatokea kama ilivyo fanyika kule Gabon karibuni wakati Omar Bongo akifanya yale yale yanayo fanywa na Samia na CCM yake sasa hivi.
 
Back
Top Bottom