Sitawafundisha tena; Ukitaka mapenzi yasikusumbue tafuta mwanamke anayemiliki pesa yake mwenyewe(anayeweza kujilisha na kujitunza)

Hpa unatupiga na kitu kizito. Mwanamke akishakuwa free financially anamdharau mwanaume. Hivyo kuteswa na mapenzi hakuepukiki.

Mwanaume ukitaka mapenzi yasikutese, tafuta mwanamke anayekupenda.
SITAWAFUNDISHA TENA; UKITAKA MAPENZI YASIKUSUMBUE TAFUTA MWANAMKE ANAYEMILIKI PESA YAKE MWENYEWE (ANAYEWEZA KUJILISHA NA KUJITUNZA)

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Elewa, mwanamke Anayemiliki pesa zake mwenyewe alafu akakukubalia uwe Mchumba au mpenzi wake huyo kuna uwezekano wa asilimia 90% anakupenda.

Hii ni tofauti na hawa ambao ni tegemezi.

Usiuamini upendo wa mtu tegemezi, na aliyemaskini.

Vijana wengi wanafanya makosa makubwa kujitoa kwa wanawake tegemezi. Ni kosa kubwa kufanya hivyo.

Mwanamke anayeweza kujilisha, kujivalisha, kujitunza huyo akitafuta mwanaume hutafuta mwanaume kwelikweli kwaajili ya kuwa Mke na huyo mwanaume kuwa Mume.
Hakunaga Unafiki hapo.

Lakini hawa tegemezi, njaanjaa, wanaofikiri kuwa mwanamke ni kilema, au Tiketi ya kuwa ombaomba hao usiwaweke kwenye hesabu. Watakuumiza. Wengi wao ni wanafiki.
Wengi wao mahusiano ni ajira Rasmi.
Wengi wao huwachukulia wanaume kama Misukule yako.

Usitegemee pesa za Mwanamke. Lakini hiyo haimaanishi huyo mwanamke asiwe na pesa yaani asiwe anafanya Kazi.

Mhudumie Mkeo au mwanamke lakini naye anapaswa kujihudumia kwa sehemu. Sio umhudumie kwa kila kitu.
Utakuja kupigwa vibaya wewe.

Usitoe vyote kwa pamoja. Yaani moyo na nguvu kwa mwanamke.
Toa kimoja uache kimoja.

Mfano, Kama utatoa pesa Basi usimpe Moyo wako. Hiyo tunaita kumfanya mwanamke Malaya. Yaani unanunua huduma yake.

Kama utatoa Moyo wako Basi usimpe Nguvu zako(Pesa), hiyo tunaita kupima nguvu ya mawimbo ya bahari.

Ni kosa utoe Moyo wako wote kisha utoe na pesa. Hiyo tunasema kugeuzwa mtumwa na msukule WA Mwanamke.

Haya nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Huko ni kuwa mtumwa wa ngono kwa huyo mwanamke na majibu yake kwako ni lazima mwanaume ujifanye fala haswa!
Wanaume walio kwenye mausiano na wanawake wenye hela watazuga na furaha za njee tu lakini ndani wanavyoishi anakuwa Kama houseboy tu na Hana sauti!
Umeongea ukweli mtupu mkuu
Wanawake wanaojiweza kiuchumi hapana kwa kweli👐
 
Usitoe vyote kwa pamoja. Yaani moyo na nguvu kwa mwanamke.
Toa kimoja uache kimoja.

Mfano, Kama utatoa pesa Basi usimpe Moyo wako. Hiyo tunaita kumfanya mwanamke Malaya. Yaani unanunua huduma yake.

Kama utatoa Moyo wako Basi usimpe Nguvu zako(Pesa), hiyo tunaita kupima nguvu ya mawimbo ya bahari.

Nimeondoka na hii
Hii ngoja niifanyie lamination itakuja kunifaa baadae
 
Hilo ni wazo zuri ila usianze kulalamika siku ambazo atakwambia ana kwenda safari zake za binafsi nje ya nchi - usitoe macho kama unatumbuliwa jipu - si anajiweza.
Mwanamke huru (mwemye kipato chake) ana gharama zake sheikh.

Wacha mie nikae na huyu wa kwangu akitaka kwenda kwa dadake nampeleka ama nampa nauli ya bajaji au boda, akitaka kwenda saloon ananiomba hela na kama nina muda namsindikiza hana makuu - mzigo napewa muda wowote nikijiskia.
 
Umeongea ukweli mtupu mkuu
Wanawake wanaojiweza kiuchumi hapana kwa kweli👐
Na inaumiza sana aweza hata kukutukana mbele za watoto!
Na watoto wanajua kabisa mama ndiye mwenye hela,
Ebu fikiria watoto wamekuwa na hawakueshimu inavyouma!
Lakini pia watoto wa kike wanaokulia mazingira hayo huwa na Dharau sana kwa wanaume!
 
SITAWAFUNDISHA TENA; UKITAKA MAPENZI YASIKUSUMBUE TAFUTA MWANAMKE ANAYEMILIKI PESA YAKE MWENYEWE (ANAYEWEZA KUJILISHA NA KUJITUNZA)

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Elewa, mwanamke Anayemiliki pesa zake mwenyewe alafu akakukubalia uwe Mchumba au mpenzi wake huyo kuna uwezekano wa asilimia 90% anakupenda.

Hii ni tofauti na hawa ambao ni tegemezi.

Usiuamini upendo wa mtu tegemezi, na aliyemaskini.

Vijana wengi wanafanya makosa makubwa kujitoa kwa wanawake tegemezi. Ni kosa kubwa kufanya hivyo.

Mwanamke anayeweza kujilisha, kujivalisha, kujitunza huyo akitafuta mwanaume hutafuta mwanaume kwelikweli kwaajili ya kuwa Mke na huyo mwanaume kuwa Mume.
Hakunaga Unafiki hapo.

Lakini hawa tegemezi, njaanjaa, wanaofikiri kuwa mwanamke ni kilema, au Tiketi ya kuwa ombaomba hao usiwaweke kwenye hesabu. Watakuumiza. Wengi wao ni wanafiki.
Wengi wao mahusiano ni ajira Rasmi.
Wengi wao huwachukulia wanaume kama Misukule yako.

Usitegemee pesa za Mwanamke. Lakini hiyo haimaanishi huyo mwanamke asiwe na pesa yaani asiwe anafanya Kazi.

Mhudumie Mkeo au mwanamke lakini naye anapaswa kujihudumia kwa sehemu. Sio umhudumie kwa kila kitu.
Utakuja kupigwa vibaya wewe.

Usitoe vyote kwa pamoja. Yaani moyo na nguvu kwa mwanamke.
Toa kimoja uache kimoja.

Mfano, Kama utatoa pesa Basi usimpe Moyo wako. Hiyo tunaita kumfanya mwanamke Malaya. Yaani unanunua huduma yake.

Kama utatoa Moyo wako Basi usimpe Nguvu zako(Pesa), hiyo tunaita kupima nguvu ya mawimbo ya bahari.

Ni kosa utoe Moyo wako wote kisha utoe na pesa. Hiyo tunasema kugeuzwa mtumwa na msukule WA Mwanamke.

Haya nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Oya dokta una siti yako mbinuni
 
Hilo ni wazo zuri ila usianze kulalamika siku ambazo atakwambia ana kwenda safari zake za binafsi nje ya nchi - usitoe macho kama unatumbuliwa jipu - si anajiweza.
Mwanamke huru (mwemye kipato chake) ana gharama zake sheikh.

Wacha mie nikae na huyu huyu akitaka kwenda kwa dadake nampeleka ama nampa nauli ya bajaji au boda.

Sasa yeye akienda kazini hofu yako ni nini Mkuu?

Wanawake wasiojiweza ni wanafiki kwa kiwango cha juu kabisa.
 
Unatongozaje job seeker, yani hata hela vocha anakosa, no way
Bora niendelee kuonekana nina ubaguzi
 
Mwanaume halisi atakiwa yeye awe ndio provider
kutegemea kipato cha mwanamke ndio inapunguza

uanaume tunakuwa na wanaume nyororo kwenye jamii
anayetukanwa na kupigwa na mke wake kisa eti anataka
kusaidiwa majukumu.
 
Back
Top Bottom