Sitosahau mara yangu ya kwanza kuingia Barbershop

Sitosahau mara yangu ya kwanza kuingia Barbershop

Katika maisha kila mtu anakuwa na matukio ambayo siyo rahisi kuyasahau hata akumbwe na changamoto ya namna gani.

Leo na mimi nimeamua ku share na nyinyi Wana JF tukio hili ambalo sio la kutisha Bali Ni la kawaida tu Ila naimani linafunzo ndani yake, moja kwa moja tuanze Sasa..

Wakati huo nilikua nimepangiwa chuo Mbeya pia hii ilikua ni Mara yangu ya kwanza kwenda mbeya ijapokua sikupenda kabisa kwenda mbeya lakini Post zilivyotoka ikaonesha nimepangiwa MZUMBE mbeya.

Sasa si unajua life la First year ( Hapa ndipo story ilipo ) huwaga kunakuwaga na matukio mengi sana, Kuna kuuziwa dhahabu fake ingawa niliwakwepa Hawa jamaa, kupewa hela fake, kutolewa nywele mdomoni n.k Sasa vituko vinakuwaga vingi hasa kwa wale wenzangu na mimi wanaotokea bush Yaani vijijini Hawa ndio hukutwa na Mikasa ya hatari zaidi.

Zilipita sikuchache baada ya kuanza masomo Sasa nywele zangu zilikua zimekua hivyo nikaamua kutafuta saloon ili nikanyoe, katika kutafutatafuta nikaona saloon moja iliandikwa barbershop Basi na Mimi bila hiyana nikaingia mle ndani moja kwa moja. Nakumbuka wakati nimeingia mle ndani kidogo nianguke Ile saloon kwa nje ilikua nzuri Sana Ila kwa ndani ilikua nzuri zaidi Yaani malumalu zake zilikua ni nzuri kidogo niteleze (hahaaaa ushamba huu jameni).

Mle ndani kulikua na vinyozi wawili ambapo kwa wakati huo wote walikua wakiwahudumia wateja wengine. Sasa mmoja akaniona wakati huo me bado nimesimama nashangaa shangaa mle ndani yule kinyozi mmoja akanichangamkia "Dogo kaa hapo" aliniambia huku akinionyesha sehem ya kukaa.

Nikajiona mjinga kwa kushangaa shangaa mle ndani nikahisi huenda jamaa aliniona Kama wakuja sijui, Basi nikakaa kwenye sofa. Mle ndani kulikua na masofa ya kuwatosha watu watatu yalikua mawili. Sasa Ile kukaa daaaah Yaani lile sofa lilikua Ni laini hatari ukikaa linabonyea flani hivi afu ukiinuka linakua Kama Lina ku push hivi Yaani kama linakuja juu. Basi nikawa nazidi kushangaa shangaa tu

Wakati huo wote mfukoni nilikua na buku jero tu ambaapo nilipanga buku ya kunyolea na jero ya nauli kurudi Hadi chuo. Bhana bhana si nikajua eti wananyoa kwa buku. Na Mimi hata sikushtuka tu mazingira ya Ile saloon kua hapa sio level zangu aaah. Sasa baada ya muda kidogo Kama dakika Kumi hivi Kuna jamaa akaja na gari ilikua ni V8. niliweza kumuona kupitia vioo vilivyopo mlangoni pale saloon vile vioo vilikua ni tinted me namuona wa nje Ila wa nje hanioni Mimi. Sasa nikawa naishangaa lile gari ili nione atakaeshuka nikaona akashuka jamaa mmoja hivi alikua na madevu kama ya Rick Ross madevu yake jamaa yalikua yanang'aa weusi nafikiri ni kutokana na matunzo aliyokua anayapatia, yule jamaa akaingia Hadi mle ndani nikaona wale majamaa wanamchangamkia hapo ndio nikajua kua yule jamaa ni mwenyeji pale Basi me nikamsalimia akaitikia salamu yangu afu akakaa karibu yangu.

Sasa hapo ndio nikasikia vizuri harufu ya marashi yake yalikua yananukia vizuri sanaa. Sasa hapo ndio nikaanza kushtuka kua hapa nilipoingia sio level zangu, Machale ndio yakaanza kunicheza kua hapa hapawezi kua kunyoa buku. Nikawa na discuss na halmashauri ya kichwa changu naanzaje kuondoka hapa ili wasinishtukie.

Baada ya kufikiria kwa mda kidogo nikaona bhana eeh me ngoja niamke niende tuu Sasa Ile nimenyanyuka niondoke jamaa mmoja akawa amemaliza kunyoa tayari kwa kinyozi mmoja Tena ndio yule kinyozi aliyopo upande wangu kwaiyo wakati Mimi nimenyanyuka niondoke yule kinyozi akajua ndio najiandaa ili nipande kwenye kiti.

"Dogo inaonekana una haraka Sana eeh" aliongea yule kinyozi huku akisafisha kile kiti alichotoka yule mteja mwingine. Hapana brooh Ila nimeona niondoke tu ntakuja Tena baadae kunyoa. Niliamua kudanganya ili niondoke, hapa ilikua baada ya kushtuka kua hapa sio pa buku hapa. Sasa yule kinyozi baada ya kuona vile nataka kuondoka yeye hakujua kua Sina hela Ila nahisi alikua anajua kua nataka nimfanyie janja nisepe mazima.

Wakati huo tunaongea yule mteja aliyekua ananyolewa alikua tayari ameshatoka kwenye kiti. Sasa nikabaki Mimi na yule kinyozi tunaongea wakati huo Kwenye sofa pale kulikua na yule brooh mwenye madevu amekaa, Sasa wakati tunaongea yule jamaa mwenye madevu akasema "Dogo si ukae unyolewe watu tupo tunasubiri hapa ujue oy Emma em mnyoe huyo dogo Basi" aliongea bonge na ndio hapo nikajua kua yule jamaa kinyozi anaitwa emma.

Nikaona hapa nimekamatika nikaamua kujitoa muhanga ikabidi nimuulize yule kinyozi " samahani broo lakini hapa kunyoa kwani ni shilingi ngapi ??. "Haaa!! kumbe dogo ujanja wote huo alafu unaogopa bei ya kunyolea hapa ndio maana unataka kuondoka sio " aliongea yule kinyozi. Nikamwambia hapana brooh Ila nahitaji tu kutambua bei ya kunyoa Ni shilingi ngapi?

Wakati namuuliza hivyo nilikua bado sijakaa kwenye kiti Cha kunyolea nilikua nimesimama yunaangaliana na kinyozi yule "Emma". Nikamwambia broo Mimi Nina hela .... kabla hata sijamaliza yule Big akajibu dogo em kaa unyolewe bhana kwani unaogopa Nini mbona hapa kunyoa ni bei ya kawaida sana.

Nikatulia afu nikamwangilia yule bnrooh Emma nae akasema yeah dogo we kaa tu kwenye kiti hapa kunyoa ni bei ya kawaida sana. Kila nikitaka kukaa naona nafsi inagoma kabisa naona Kama "inaniambia wewe kima hapa kunyoa sio buku hapa ukinyoa kitakacho kukuta usimlilie Mungu", Nikamuuliza yule broo Emma Tena brooh me naomba nijue bei tu Ni shilingi ngapi ya kunyoa jamaa akanijibu tenah kua nisiwe na hofu bei yao ni rafiki tu me nisiwe na wasiwasi nikae tu ninyolewe. "Kwani wewe dogo Ni wawapi wewe au Ni mnyasa" Yule big aliongea hivo, aisee nikamwangilia yule jamaa afu nikajisemea Yaani Mimi Atalanta ambae home naonekana Mimi ndio mjanja Leo hii naambiwa eti me mnyasa..?? Daah nikaona isiwe kesi nikakaa kwenye kiti kidume ili ninyolewe pasipo hata kujiuliza tenah Mara mbilimbili.

Aisee yule jamaa alivyokua ananinyoa ndio alikua anazidi kunivuruga kabisa yaan, kwanza aliniuliza nikunyoe style gani..?. Nikafikiria kidogo kwa wakati huo me nilishazoea nikienda saloon ni kunyolewa tu Sasa hapa eti naulizwa ninyolewe style gani duuuh makubwa haya, afadhari ningekua najua hata jina la style hata moja bas ningemwambia lakini kwa wakati huo sikuijua yoyote Ile.

Nikabaki namkodolea mimacho tu jamaa akaniuliza tenah oy dogo unataka nikunyoe style gani..?. Nikawa najiuliza tenah moyoni nikasema hapa unaweza kuta kila style na bei yake Sasa nikianza kumwambia aninyoe mtindo wowote anaweza ninyoa style ya bei kubwa afu nikashindwa kulipa, nikamwambia kwa kujiamini kaabisa ninyoe style ya bei ndogo kuliko zote. Khaaaa!

Yule big akasema wewe dogo vipi mbona unatuletea vituko hapa Sasa ndio style gani hiyo, yule kinyozi akamwabia oy tulia mkubwa ngoja nimweleshe dogo inaonekana ni mgeni hapa mjini. Basi yule kinyozi akaniambia kua nitaje style yoyote Ile ataninyoa kwa gharama Ile Ile. me nikamwambia kua nilijua kila style inabei yake akaniambia hapana style zote Ni bei moja tu. Nikamwambia bas ninyoe unayoona wew Ni nzuri, Niseme ukweli tu Yaani kwa siku ile Kama yule Big mwenye madevu ndio angekua ni kinyozi nahisi angenitimua pale pale tenah na makofi juu maana jamaa alikua ana Ni mind hatar. Kinyozi Akaanza kuninyoa sasa huwezi amini naweza sema huenda Ile ndio saloon niliyotumia mda mrefu kunyolewa nilitumia Kama dakika 1
20- 30 kunyolewa tu.

Aisee jamaa alivyonimaliza Ile kujicheki kwenye kioo daah nilipendeza hatariii nikasema kweli majamaa wanajua kunyoa.

Sasa nilipotoka kwenye kiti Cha kunyolea nikawa najipukuta pukuta nywele kichwani na mikono yule kinyozi akaniambia oy dogo usijipukute utajichafua hapo bado hujamaliza.

Sikumuelewa anamaanisha nini alivyosema vile kua sijamaliza nikajua alikua nanitania sababu Hadi nanyolewa yule Big alikua akinitania Sana mule saloon. Me nikamjibu yule kinyozi "aah hapa mbona haina shida brooh nishamaliza hapa alaf...." Sikumaliza hata kuongea nikamsikia yule kinyozi mwingine anamuita mdada mmoja alikua nje "wee asha wewe afu mbona unajisahau Sana au haujaona wateja humu ndani afu we unakaa kaa nje tu " Sasa me nikajiuliza huyu asha anakuja kufanya nini tena nikajiongeza nikasema aah huenda atakua anakuja kufanya usafi labda. wakati huo nilikua najipukuta huku najiangalia kwenye kioo hapo.

Sasa Ile niangalie mlangoni ili nimuone asha mwenyew, khaa mama yangu nikabaki nimeganda Tena namuangalia tu alikua mdada mmoja mzuri mweupee pee sio mnene Sana Ila anashepu nzuri yakuvutia, wakati bado namshangaa yule Asha nikaona Kama upande wa pili Kuna mtu ananiangalia si unajua Kama mtu anakuangalia sana unaweza hisi tu kua Kuna mtu anakuangalia kwa muda mrefu, nilipogeuza shingo niangalie Nani anae niangalia huyo Basi nakakutanisha macho na yule big afu akasema "kua makini dogo mjini hapa".

Nikabaki najichekesha tu nikahisi mkono wangu umeshikwa na mkono laini aisee kidogo nipige ukelele Sasa Ile niangalie Nani aliyenishika mweee mwee mweee si nikaona Asha ndio kanishika mkono akasema ndio wewe ?? Kama kawaida yangu nikabaki nimeduwaa tena Sasa hapa najibu nini Mimi. Nikamuangalia Emma sikumwabia chochote Ila Ile angalia yangu tu alishajua kipi namaanisha. Yule kinyozi akaniambia dogo mfate huyo Dada nend nae humo "akionesha kichumba kingine kilichopo mlemle ndani" atakuosha hizo nywele.

Nikaona mmh hapa Leo nimeyakanyaga hapa naona kabisa nimeyakanyaga kiufupi Leo nitajibeba, Nikamwambia kinyozi brooh me kuhusu kujiosha ntaenda kujiosha hata hosteli we usijari. Akasema Dogo najua utakua unawazia kuhusu bei Ila kwa sisi hapa tunafanya bei moja Yaani mteja akinyoa tu nilazima aende huko kwenye hicho chumba ili asafishwe bei ya huko Ni hii hii ya kunyolea Hapa.

Hiyo huduma ya huko ni ya ziada tu hata Kama usipoenda huko Ila bei Ni Ile Ile moja tu kwaiyo Bora uende tu. Nikajisemea haya makubwa Sasa, Ikabidi nimfate yule dada anaeitwa Asha ambae alienda kwenye kile chumba kingine. Nilivyoingia mle ndani nikaona kulikua na kiti Ila sio Cha plastic na Wala sio Cha mbao sijui kipoje kipoje kile kiti pia kulikua na kitanda.

Basi nikaambiwa nikae pale kwenye kile kiti nikakaa kidume kutoka moro.Yule mdada Asha akakiminya kile....

Mwendelezo: Sitosahau mara yangu ya kwanza kuingia Barbershop
Naweka kambi
JamiiForums458960362.jpg
 
MUENDELEZO
yule mdada Asha akakiminya wapi sijui kile kiti kikawa kinalala Basi kinarudi nyuma taratiiibu "Yaani Kama kina lala hivi" Mara baada ya muda kidogo kikakaa sawa Ila kwa dizain ya kulala hivohivo. Wakati nikiwa bado nipo kwenye kile kiti nikaona Asha akafungua koki ya maji pale pale pembeni kulikua na Kama ka sink hivi kadogo alipofungua Ile koki ya kwanza nikahisi Yale maji yaliyotoka yalikua ni ya motomto nilihisi hivyo kwasababu alijiosha mikono yake afu wakati wa kujifuta ndio yakanirukia kidogo baada ya hapo akafungua koki nyingine tenah hapo yakatoka ya baridi nayo pia niliyahisi kwa stail Ile Ile akafungua tenah koki ya tatu hapo sikuona kilichotoka sababu mawazo yangu yakarudi tenah kufikiria bei tu Yaani kichwa kikawa kinawaka Moto kwa kuwaza bei ya pale Sasa ukijumlisha na Asha alipokua akafungua zile koki Yaani ndio akawa ananitoa kwenye reli kabisa.

Baada ya muda Asha akaniuliza kua natumia Sabuni au rosheni gani..?? aah mtihani mwingine huuu kwangu me home nishazoea Sabuni ninayotumia Ni TAKASA "kipindi kile zilikuwepo sijui Kam bado zipo Hadi saiz" Tena na yenyewe sio kwamba hiyo Ni spesho kwa kuogea aah hapana Kama nataka kwenda kuoga nabeba ntakayoiona unakuta Sabuni hiyo hiyo Ni yakuogea tena hiyo hiyo ya kuoshea vyombo Sasa hapa eti naulizwa unatumia Sabuni gani nijibu nini Sasa.Nikamwambia em tuone Sabuni ulizonazo hapa Basi nikaangalia sikuona hata TAKASA yangu Wala inayoendana na TAKASA haikuwepo pale, ilibaki kidogo nimuulize kua Kama anasabuni ya magadi nikaona mmh hapa ntaonekana mshamba Zaidi. Ikabidi nimwambie we nipake yoyote Ile ambayo haitoi vipele. Akachukua Sabuni gani sijui Ile me siifaham akanza kunipaka aisee yule mdada anamikono milaini nyieee sijapata ona Basi na ushamba wangu huu naoshwa usoni na kichwani lakini chaajabu kichwa chini kikawa kinahangaika Yaani sikuile ilikua ni tabu tupu. Jamani jamani Kuna wadada wanajua kuongea yule mdada "Asha" alikua anaongea taratiiibu Ila kadri ninavyoisikia sauti yake nilikua nazidi kusisimka daah nyie acheni tu, Chaajabu Sasa ukiniuliza alikua anaongea nini sikumbukk hata kimoja Ila napenda tu kusikia vyenye alivyokua anaongea. Akawa anachukua sijui vitu gani Mara ajipake mkononi afu anipake usoni Mara anifute na kitambaa lain, akawa ananipaka hiki ananisafisha. Kusema ukweli sikutamani nitoke kwenye kile chumba kwa wakati huu nilikua najiona Kama nipo kwenye ulimwengu mwingine kabisa yaan nilikua nasikia raha tu kua na yule mdada mule ndani.

Baada ya muda kidogo nikaona ngoja nimuulize Asha bei ya kunyoa hapa Ni shingapi. samahani sister hivi bei ya kunyoa hapa Ni shilingi ngapi kwani..?? Yule mdada akawa Kama ananishangaa hivi baada ya kunijibu akaniambia kwani hawajakwambia bro ni shingapi. Nikamwambia hapana hawajaniambia akasema usijar bei ya hapa Ni ya kawaida sana. Sasa nikawa nimechoshwa na majibu yao Yale nikawa nimetulia tu.Nikawa nimemaliza kunyolewa Sasa nikaanza kujifikiria kuhusu bei akili ikawa inaniambia kabisa kua hapa piga ua garagaza hapawezi kua pa buku. Nikamfata kinyozi mmoja "Emma" sababu niliona kidogo yeye ndio Kama nimezoeana nae kwa muda ule mfupi. Yule broo Emma alivyoniona tu nimetoka kunyoa akaniulize dogo umeonaje huduma. Nikamjibu huduma ni nzuri tu brooh, wakati naongea nae hapo pia alikua anamnyoa mtu mwingine yule Big alikua kwenye kiti kingine akinyolewa na yule jamaa mwingine. Nikaona hapa ili kujua bei nisiulize kwa sauti kubwa nisije haribu Basi nikamsogelea yule brooh Emma karibu afu nikamuulize sorry brooh gharama yake ni kiasi gani. Emma akanijibu dogo gharama yake siyo kubwa Ni teni tu. aisee nilitoa macho achaa Nikamuuliza Tena taratibu "umesema shingapi broo" safari hii hakujibu yeye akajibu yule big "dogo si umeshaambiwa ten au hujui kiingereza okay bei yake ni Elfu kumi nimekufafanulia Sasa". Nikashangaa huyu Big vipi nae me naongea na Emma afu yeye ananijibu. Nikaona isiwe kesi nikamwambia Emma "brooh naomba tuongee maramoja tafadhari" yule Big akajibu tena muongee nini dogo we TOA hela Kama huna acha viatu hivyo aisee nilijuta kwenda pale mbona. Nikabaki najiwazia moyoni Sasa hapa hata Kama nikaomba anipunguzie bei kutoka elfu kumi Hadi buku hivi atanielewa kweli..??. Nikaona hapa lazima niache kitu hapa usikute atasema niache viatu kweli Ila daah na Mimi kwanini niliingia hapa Sasa.

Ninachoshukuru Mungu yule Emma alikua anaonekana ni mcheshi Sana afu alikua akitabasamu tu muda wote wakati naongea nae Sasa nikaona hapahapa ndio pa kujichukulia point. Nikamwambia Tena taratibu "broo samahani naomba nipunguzie bei bas" akanigeukia afu akaniambia dogo bei ya kunyoa ndio hiyo hiyo hua hatupunguzi ndio maana tukaamua kuweka bei ndogo hivyo. Moyoni nikawa najisemea elfu kumi ni bei ndogo kweli..?? Yaani hela ambayo Mimi natumia kwenye msos siku tatu kwa bajeti yangu afu wao wanasema eti ni ndogo, Nikasema daah bora ningenyoa na wembe tu Hostel . Emma akaniuliza kwani wewe unashingapi nikaganda nafikiria maana nilikua naogopa hata kutaja hela niliyonayo nikabaki namuangalia tu kwa sura ya huruma. Dogo usitie huruma mjini hapa hakuna wa kumdekea aliongea Big, alikua ananiona kupitia kioo Cha mbele Cha mle saloon. Emma Akasema Basi subiri hapo nimmalizie kumtoa huyu afu tutaongea nikaona hapa saloon inaonekana kunakuwaga na watu wengi hapa unaweza kuta katoka huyu akaja mwingine nikaona Bora niwe muwazi tu. Nikamwambia samahani brooh Mimi ninahela ndogo nilikua sijui bei yake kweli tena. akaniambia usijari dogo hela ndogo Ni shilingi ngapi hiyo kwani elfu Tano au, daah nikabaki namkodolea mimacho tu afu nikatikisa kichwa kukataa hiyo hela aliyoitaja yeye. akasema Sasa una kiasigani dogo nikamwambia nina buku. Buku !!! aisee yule Big alishangaa nyieee akasema Emma huyu dogo anakufanyia masihara bhana haiwezekani afu we dogo kwani Ni wa wapi wew nikamwambia me natokea morogoro akasema morogoro mbona wajanja afu we inaonekana mshamba mshamba wewe Ni wa morogoro kweli wewe.

Nikajisemea tena moyoni eeh Mungu nisaidie nisionekane tapeli tu me nitoke salama hapa. Hamna broo sema me natokea ndani ndani kidogo nikaamua kumjibu hivyo. Ndani ndani wapi huko nae akaniuliza nikamwambia natokea Euga akasema duuh huko nako ni morogoro nikamjibu ndio. Emma malizana na mtu wako bhana akasema yule Big. Me nikajua ananilipia alivyokua ananiuliza maswali vile Sasa et nae anamwambia tenah Emma amalizane na Mimi daah . Naomba nisaidie brooh nikaamua kuanzisha Tena mazungumzo Sasa Mimi nakusaidijae hapo mdogo wangu labda angalau Kama ungekua na elfu Tano Mimi ningekuelewa Sasa wewe dogo una buku hata Kama wewe ungekua Mimi ungefanyaje hapo eeh afu kingine dogo humu siko peke yangu nipo na wenzangu nao pia tunagawana pesa Sasa vipi Kama Mimi nilichukua hiyo buku yako wao watanielewa ?

Nikaona kweli kabisa jamaa kaongea sawa lakini na Mimi hiyo 10k Sina nikafikiria nikamgeukia yule Big nikamwambia broo naomba nisaidie samahani Mimi nilikua sijui bei ya hapa Ila Kama ningekua naijua nisinge hata Sogea. Yule Big akanikata jicho afu akaniambia dogo mbona msumbufu wewe afu mbeya umekuja kwa Nani yako kwanza tuanzie hapo nikamjibu nimekuja chuo kusoma. Yaani mitoto mwingine Ni mipumbafu kabisa Sasa wewe msomi mzima ulifikiri bei ya kunyoa hapa Ni buku ivi kweli !! wewe lipa tu ili sikunyingine ujifunze nikamwambia samahani brooh nimejifunza tayar nilikua siifaham kweli Tena yule Big akaniangalia afu akasema sikunyingine usirudie tena utatolewa kizuri Mbeya imebadilika sikuhizi sawa, nikamwambia sawa shukrani brooh nashukuru sana. Sasa unashukuru Nini akaniambia yule big nikamjibu nashukuru unanilipia akasema haaa wew dogo Nani kasema nakulipia dogo vipi wewe. Nikaona Sasa hapa naumbuka mtu mzima nikarudi kukaa kwenye sofa pale safari hii sikuona hata Kama lile sofa Ni laini niliona hakauna tofauti yoyote Kati ya sofa na benchi la kawaida na hii Ni sababu ya mawazo niliyonayo .

wakati nimekaa pale nafikilia nikaona yule Big akaniambia dogo nenda kasome ntakulipia Daah Kama sikusikia vizuri nikamuangalia Tena yule big. Unashangaa Nini dogo wewe nenda me ntakulipia aisee nilimshukuru Sana yule Big siku hiyo.

Tangu siku hiyo sijawah kurudi Tena pale saloon Kuna kipindi nilitaka niende hata niwape hai hasa hasa yule kinyozi Emma lakini sikufanya hivyo.
Tumeipenda Wallah
JamiiForums-1374833720.jpg
 
Pole sana kuna muda unaweza dhalilika kinomaa...na mm kuna siku nilipanda daladala kumbe nimedondosha kipochi kidogoo kilikua na nauli..nilijua kipo kwny mkoba mkubwa..wee nimekaa siti ya mbele na mkaka bahati nzuri nilimsalimia wkt nimeingia sasa konda anaanza kudai nauli siti ya mbele kuangalia sina tafuta mifuko ya pochi yotee sioni kipochi hakipoo nikatoa machoo...konda na yy badala aende nyuma kakazana dada nauli..nikasema isiwe tabu kudhalilika mara moja na watu wenyewe hawanijui ngoja nimuombe huyu kaka jirani nauli nikamwambia bro sioni nauli..basi hata hajajiuliza akanipa nikampa konda..duuh yani usimcheke mtu kisa amedhalilika ipo siku na ww yanaweza kukukuta..
 
Khahahahah!
Kuna siku nikawa nimedaka kamkwanja flani hivi kadoogodogo.

Nikajisemea,kabla hakajaisha,ngoja na Mimi nikaoshe nyota.

Nikatungua kadent & katshet kamtoko
Mimi huyo🏃 Barbashop haiwezikani napita tu.

Nikazama ndichi,ebhanae kidogo kidogo nirudi nyuma nikajikaza kiume,maana nilikuta Sura kadhaa nzuri kinouma.
Nywele zangu Kama kawaida hazina mlolongo mzuri.

Karibisha yenyewe nikasema,ewaaaaaa hapahapa.

Mademu waliokuwa wawili vinyozi wawili,wateja Kama watatu.so more ndani kukawa c haba.

Store nyingi,na wakawa vinyoz wanawatania wale mademu mpaka nikasema,day Kuna watu wanafanya kazi mazingira mazuri,FURU rsha.

Zamu ikafika YANGU,mashine za kunyolea haziumiz hata kidogo,tofauti na kile pa siku zote unakutana na mashine utafikiri imetolewa JIKONI
,Nikamaliza,sikuwa na wasiwasi,nikaulizwa mekapu ipi nahitaji,nikasema iliyo quarity.
Sasa ebhanaeeeee!demu mkali ndo slikuwa anafanya hayo yote.
Si nilisema quarity,hee acha aanze kufinya uso wangu.

Aibu ya mwaka,uso wangu ulikuw unatoa vitu vyeupe Kama MAFINYO loh3!
Nikashtuka,in maana nimeoza au!.
Mbona sielewi elewi,kucheki watu mle ndani wanafatilia show inayoendelea kwangu.
Naiman vilivyotoka usoni kwangu vingejaa mfuniko wa chupa ya maji Kilimanjaro.

Nikapelekwa room ingine,kule hudma Kama kawa ya viwango,room ile ilikuwa kubwa kinyama.
Baadae ile pisi mautani Kama you're,kumbe bhana MDA wote msemaji was RUVU SHOOTING slikuwa amesimama Dede kwa ajili ya mahojiano.
Kulingana na Dada yule alivyokuwa akinishikashika,akaniambia,Kuna huduma extral Kama ntahitaji lakini.maana nilifanyiwa mpaka massage ya nusu mwili.

Alikuwa akifika karibu na kwa msemaji was Ruvushooting anakuwa Kama amejisahau anagusa kiutaalam.

Nikamwambia fresh,akasema day ni elfu 20000. Huduma ya extral.nikasema fresh.

Maana nilitaka nipewe huduma zote za pale.

Daaaaaaaah,duniani Raha Sana bhana.
Nikapiga bori Kama feisal shot la nje ya 18.
Wow.
Nilivotoka mule ndani,nikajisemea mmepata hell YANGU kubwa,Ila nami nimeinjoi.
Baada ya hapo,nilala njaa Kama siku 3 mpaka 4.
 
Khahahahah!
Kuna siku nikawa nimedaka kamkwanja flani hivi kadoogodogo.

Nikajisemea,kabla hakajaisha,ngoja na Mimi nikaoshe nyota.

Nikatungua kadent & katshet kamtoko
Mimi huyo🏃 Barbashop haiwezikani napita tu.

Nikazama ndichi,ebhanae kidogo kidogo nirudi nyuma nikajikaza kiume,maana nilikuta Sura kadhaa nzuri kinouma.
Nywele zangu Kama kawaida hazina mlolongo mzuri.

Karibisha yenyewe nikasema,ewaaaaaa hapahapa.

Mademu waliokuwa wawili vinyozi wawili,wateja Kama watatu.so more ndani kukawa c haba.

Store nyingi,na wakawa vinyoz wanawatania wale mademu mpaka nikasema,day Kuna watu wanafanya kazi mazingira mazuri,FURU rsha.

Zamu ikafika YANGU,mashine za kunyolea haziumiz hata kidogo,tofauti na kile pa siku zote unakutana na mashine utafikiri imetolewa JIKONI
,Nikamaliza,sikuwa na wasiwasi,nikaulizwa mekapu ipi nahitaji,nikasema iliyo quarity.
Sasa ebhanaeeeee!demu mkali ndo slikuwa anafanya hayo yote.
Si nilisema quarity,hee acha aanze kufinya uso wangu.

Aibu ya mwaka,uso wangu ulikuw unatoa vitu vyeupe Kama MAFINYO loh3!
Nikashtuka,in maana nimeoza au!.
Mbona sielewi elewi,kucheki watu mle ndani wanafatilia show inayoendelea kwangu.
Naiman vilivyotoka usoni kwangu vingejaa mfuniko wa chupa ya maji Kilimanjaro.

Nikapelekwa room ingine,kule hudma Kama kawa ya viwango,room ile ilikuwa kubwa kinyama.
Baadae ile pisi mautani Kama you're,kumbe bhana MDA wote msemaji was RUVU SHOOTING slikuwa amesimama Dede kwa ajili ya mahojiano.
Kulingana na Dada yule alivyokuwa akinishikashika,akaniambia,Kuna huduma extral Kama ntahitaji lakini.maana nilifanyiwa mpaka massage ya nusu mwili.

Alikuwa akifika karibu na kwa msemaji was Ruvushooting anakuwa Kama amejisahau anagusa kiutaalam.

Nikamwambia fresh,akasema day ni elfu 20000. Huduma ya extral.nikasema fresh.

Maana nilitaka nipewe huduma zote za pale.

Daaaaaaaah,duniani Raha Sana bhana.
Nikapiga bori Kama feisal shot la nje ya 18.
Wow.
Nilivotoka mule ndani,nikajisemea mmepata hell YANGU kubwa,Ila nami nimeinjoi.
Baada ya hapo,nilala njaa Kama siku 3 mpaka 4.
Aibu ya mwaka,uso wangu ulikuw unatoa vitu vyeupe Kama MAFINYO loh3!
Nikashtuka,in maana nimeoza au!.
Mbona sielewi elewi,kucheki watu mle ndani wanafatilia show inayoendelea kwangu.
Naiman vilivyotoka usoni kwangu vingejaa mfuniko wa chupa ya maji Kilimanjaro.
hahaha sura yako ikawa I natoka MAFINYO mjinga kweli wewe

Jamaa shu ni mshaka Glenn Mamaya
 
Pole sana kuna muda unaweza dhalilika kinomaa...na mm kuna siku nilipanda daladala kumbe nimedondosha kipochi kidogoo kilikua na nauli..nilijua kipo kwny mkoba mkubwa..wee nimekaa siti ya mbele na mkaka bahati nzuri nilimsalimia wkt nimeingia sasa konda anaanza kudai nauli siti ya mbele kuangalia sina tafuta mifuko ya pochi yotee sioni kipochi hakipoo nikatoa machoo...konda na yy badala aende nyuma kakazana dada nauli..nikasema isiwe tabu kudhalilika mara moja na watu wenyewe hawanijui ngoja nimuombe huyu kaka jirani nauli nikamwambia bro sioni nauli..basi hata hajajiuliza akanipa nikampa konda..duuh yani usimcheke mtu kisa amedhalilika ipo siku na ww yanaweza kukukuta..
bro aliyekupa nauli ulimpa number😀
 
Back
Top Bottom