Sitosahau mara yangu ya kwanza kuingia Barbershop

MUENDELEZO
yule mdada Asha akakiminya wapi sijui kile kiti kikawa kinalala Basi kinarudi nyuma taratiiibu "Yaani Kama kina lala hivi" Mara baada ya muda kidogo kikakaa sawa Ila kwa dizain ya kulala hivohivo. Wakati nikiwa bado nipo kwenye kile kiti nikaona Asha akafungua koki ya maji pale pale pembeni kulikua na Kama ka sink hivi kadogo alipofungua Ile koki ya kwanza nikahisi Yale maji yaliyotoka yalikua ni ya motomto nilihisi hivyo kwasababu alijiosha mikono yake afu wakati wa kujifuta ndio yakanirukia kidogo baada ya hapo akafungua koki nyingine tenah hapo yakatoka ya baridi nayo pia niliyahisi kwa stail Ile Ile akafungua tenah koki ya tatu hapo sikuona kilichotoka sababu mawazo yangu yakarudi tenah kufikiria bei tu Yaani kichwa kikawa kinawaka Moto kwa kuwaza bei ya pale Sasa ukijumlisha na Asha alipokua akafungua zile koki Yaani ndio akawa ananitoa kwenye reli kabisa.

Baada ya muda Asha akaniuliza kua natumia Sabuni au rosheni gani..?? aah mtihani mwingine huuu kwangu me home nishazoea Sabuni ninayotumia Ni TAKASA "kipindi kile zilikuwepo sijui Kam bado zipo Hadi saiz" Tena na yenyewe sio kwamba hiyo Ni spesho kwa kuogea aah hapana Kama nataka kwenda kuoga nabeba ntakayoiona unakuta Sabuni hiyo hiyo Ni yakuogea tena hiyo hiyo ya kuoshea vyombo Sasa hapa eti naulizwa unatumia Sabuni gani nijibu nini Sasa.Nikamwambia em tuone Sabuni ulizonazo hapa Basi nikaangalia sikuona hata TAKASA yangu Wala inayoendana na TAKASA haikuwepo pale, ilibaki kidogo nimuulize kua Kama anasabuni ya magadi nikaona mmh hapa ntaonekana mshamba Zaidi. Ikabidi nimwambie we nipake yoyote Ile ambayo haitoi vipele. Akachukua Sabuni gani sijui Ile me siifaham akanza kunipaka aisee yule mdada anamikono milaini nyieee sijapata ona Basi na ushamba wangu huu naoshwa usoni na kichwani lakini chaajabu kichwa chini kikawa kinahangaika Yaani sikuile ilikua ni tabu tupu. Jamani jamani Kuna wadada wanajua kuongea yule mdada "Asha" alikua anaongea taratiiibu Ila kadri ninavyoisikia sauti yake nilikua nazidi kusisimka daah nyie acheni tu, Chaajabu Sasa ukiniuliza alikua anaongea nini sikumbukk hata kimoja Ila napenda tu kusikia vyenye alivyokua anaongea. Akawa anachukua sijui vitu gani Mara ajipake mkononi afu anipake usoni Mara anifute na kitambaa lain, akawa ananipaka hiki ananisafisha. Kusema ukweli sikutamani nitoke kwenye kile chumba kwa wakati huu nilikua najiona Kama nipo kwenye ulimwengu mwingine kabisa yaan nilikua nasikia raha tu kua na yule mdada mule ndani.

Baada ya muda kidogo nikaona ngoja nimuulize Asha bei ya kunyoa hapa Ni shingapi. samahani sister hivi bei ya kunyoa hapa Ni shilingi ngapi kwani..?? Yule mdada akawa Kama ananishangaa hivi baada ya kunijibu akaniambia kwani hawajakwambia bro ni shingapi. Nikamwambia hapana hawajaniambia akasema usijar bei ya hapa Ni ya kawaida sana. Sasa nikawa nimechoshwa na majibu yao Yale nikawa nimetulia tu.Nikawa nimemaliza kunyolewa Sasa nikaanza kujifikiria kuhusu bei akili ikawa inaniambia kabisa kua hapa piga ua garagaza hapawezi kua pa buku. Nikamfata kinyozi mmoja "Emma" sababu niliona kidogo yeye ndio Kama nimezoeana nae kwa muda ule mfupi. Yule broo Emma alivyoniona tu nimetoka kunyoa akaniulize dogo umeonaje huduma. Nikamjibu huduma ni nzuri tu brooh, wakati naongea nae hapo pia alikua anamnyoa mtu mwingine yule Big alikua kwenye kiti kingine akinyolewa na yule jamaa mwingine. Nikaona hapa ili kujua bei nisiulize kwa sauti kubwa nisije haribu Basi nikamsogelea yule brooh Emma karibu afu nikamuulize sorry brooh gharama yake ni kiasi gani. Emma akanijibu dogo gharama yake siyo kubwa Ni teni tu. aisee nilitoa macho achaa Nikamuuliza Tena taratibu "umesema shingapi broo" safari hii hakujibu yeye akajibu yule big "dogo si umeshaambiwa ten au hujui kiingereza okay bei yake ni Elfu kumi nimekufafanulia Sasa". Nikashangaa huyu Big vipi nae me naongea na Emma afu yeye ananijibu. Nikaona isiwe kesi nikamwambia Emma "brooh naomba tuongee maramoja tafadhari" yule Big akajibu tena muongee nini dogo we TOA hela Kama huna acha viatu hivyo aisee nilijuta kwenda pale mbona. Nikabaki najiwazia moyoni Sasa hapa hata Kama nikaomba anipunguzie bei kutoka elfu kumi Hadi buku hivi atanielewa kweli..??. Nikaona hapa lazima niache kitu hapa usikute atasema niache viatu kweli Ila daah na Mimi kwanini niliingia hapa Sasa.

Ninachoshukuru Mungu yule Emma alikua anaonekana ni mcheshi Sana afu alikua akitabasamu tu muda wote wakati naongea nae Sasa nikaona hapahapa ndio pa kujichukulia point. Nikamwambia Tena taratibu "broo samahani naomba nipunguzie bei bas" akanigeukia afu akaniambia dogo bei ya kunyoa ndio hiyo hiyo hua hatupunguzi ndio maana tukaamua kuweka bei ndogo hivyo. Moyoni nikawa najisemea elfu kumi ni bei ndogo kweli..?? Yaani hela ambayo Mimi natumia kwenye msos siku tatu kwa bajeti yangu afu wao wanasema eti ni ndogo, Nikasema daah bora ningenyoa na wembe tu Hostel . Emma akaniuliza kwani wewe unashingapi nikaganda nafikiria maana nilikua naogopa hata kutaja hela niliyonayo nikabaki namuangalia tu kwa sura ya huruma. Dogo usitie huruma mjini hapa hakuna wa kumdekea aliongea Big, alikua ananiona kupitia kioo Cha mbele Cha mle saloon. Emma Akasema Basi subiri hapo nimmalizie kumtoa huyu afu tutaongea nikaona hapa saloon inaonekana kunakuwaga na watu wengi hapa unaweza kuta katoka huyu akaja mwingine nikaona Bora niwe muwazi tu. Nikamwambia samahani brooh Mimi ninahela ndogo nilikua sijui bei yake kweli tena. akaniambia usijari dogo hela ndogo Ni shilingi ngapi hiyo kwani elfu Tano au, daah nikabaki namkodolea mimacho tu afu nikatikisa kichwa kukataa hiyo hela aliyoitaja yeye. akasema Sasa una kiasigani dogo nikamwambia nina buku. Buku !!! aisee yule Big alishangaa nyieee akasema Emma huyu dogo anakufanyia masihara bhana haiwezekani afu we dogo kwani Ni wa wapi wew nikamwambia me natokea morogoro akasema morogoro mbona wajanja afu we inaonekana mshamba mshamba wewe Ni wa morogoro kweli wewe.

Nikajisemea tena moyoni eeh Mungu nisaidie nisionekane tapeli tu me nitoke salama hapa. Hamna broo sema me natokea ndani ndani kidogo nikaamua kumjibu hivyo. Ndani ndani wapi huko nae akaniuliza nikamwambia natokea Euga akasema duuh huko nako ni morogoro nikamjibu ndio. Emma malizana na mtu wako bhana akasema yule Big. Me nikajua ananilipia alivyokua ananiuliza maswali vile Sasa et nae anamwambia tenah Emma amalizane na Mimi daah . Naomba nisaidie brooh nikaamua kuanzisha Tena mazungumzo Sasa Mimi nakusaidijae hapo mdogo wangu labda angalau Kama ungekua na elfu Tano Mimi ningekuelewa Sasa wewe dogo una buku hata Kama wewe ungekua Mimi ungefanyaje hapo eeh afu kingine dogo humu siko peke yangu nipo na wenzangu nao pia tunagawana pesa Sasa vipi Kama Mimi nilichukua hiyo buku yako wao watanielewa ?

Nikaona kweli kabisa jamaa kaongea sawa lakini na Mimi hiyo 10k Sina nikafikiria nikamgeukia yule Big nikamwambia broo naomba nisaidie samahani Mimi nilikua sijui bei ya hapa Ila Kama ningekua naijua nisinge hata Sogea. Yule Big akanikata jicho afu akaniambia dogo mbona msumbufu wewe afu mbeya umekuja kwa Nani yako kwanza tuanzie hapo nikamjibu nimekuja chuo kusoma. Yaani mitoto mwingine Ni mipumbafu kabisa Sasa wewe msomi mzima ulifikiri bei ya kunyoa hapa Ni buku ivi kweli !! wewe lipa tu ili sikunyingine ujifunze nikamwambia samahani brooh nimejifunza tayar nilikua siifaham kweli Tena yule Big akaniangalia afu akasema sikunyingine usirudie tena utatolewa kizuri Mbeya imebadilika sikuhizi sawa, nikamwambia sawa shukrani brooh nashukuru sana. Sasa unashukuru Nini akaniambia yule big nikamjibu nashukuru unanilipia akasema haaa wew dogo Nani kasema nakulipia dogo vipi wewe. Nikaona Sasa hapa naumbuka mtu mzima nikarudi kukaa kwenye sofa pale safari hii sikuona hata Kama lile sofa Ni laini niliona hakauna tofauti yoyote Kati ya sofa na benchi la kawaida na hii Ni sababu ya mawazo niliyonayo .

wakati nimekaa pale nafikilia nikaona yule Big akaniambia dogo nenda kasome ntakulipia Daah Kama sikusikia vizuri nikamuangalia Tena yule big. Unashangaa Nini dogo wewe nenda me ntakulipia aisee nilimshukuru Sana yule Big siku hiyo.

Tangu siku hiyo sijawah kurudi Tena pale saloon Kuna kipindi nilitaka niende hata niwape hai hasa hasa yule kinyozi Emma lakini sikufanya hivyo.
 
Unanikumbusha miaka ya 2012 tulivamia mlimani City kwenye restaurant moja vyakula bei juu sana, jamaa angu kwa jeuri anauliza MENU ZIKO WAPI? menu zikaletwa tena kila mtu ya kwake, mfukoni kila mtu ana 2.5k buku 2 msosi nauli jero. Kukagua menu kitu cha bei rahisi juisi glas 1 ni 2000😢😢😢🤔 wali mkavu 6000,itoshe tu kusema tulikimbia kwa aibu na jeuri ya ndugu yote
 
Umenifurahisha.Umenikumbusha mara ya kwanza kutumia tea bag tena hotelini .Kata kamba kwenye kikombe nikakatoboa na meno nikamimina kwenye kikombe.Wenyeji wangu wakabaki wamepigwa na butwaa.Ushamba mzigo.
 
Ulikosea ungeenda tena tena ungeenda kunyoa kwa bei yai ya 10,000.

Kuinyesha wewe sio mnyonge kihivho ni vile hukujua bei na hukutembea na hela ya kutosha.
 
Umenifurahisha.Umenikumbusha mara ya kwanza kutumia tea bag tena hotelini .Kata kamba kwenye kikombe nikakatoboa na meno nikamimina kwenye kikombe.Wenyeji wangu wakabaki wamepigwa na butwaa.Ushamba mzigo.
Kuna vitu ukiwa ugenini na hujui cha kufanya jifunze kutegea unaangalia kwanza wenzio wanafanyaje?
 
Umenikumbusha hapo Kebbys hotel sijui ni mwenge tumeenda kwaajili ya 4u movement ya lowassa mimi na kiherehere nimewahi kutoka UD wadau hawajafika nikaona ngoja nikacheki mechi ya yanga na mgambo jkt wakati huo ya akina malimi busungu,Si nikaaguza cocacola mfukoni nina buku nikajua kama kiaani mia sita bas hapa buku yule dada kuja eti buku mbili jero aiseeeee nipo hotelin ntafanyaje sasa.
Chap chap nikampigia mdogo wangu wa kike kijijin kuomboleza akanisave buku 5 ile nataka nikatoe chini pale nashangaa mshikaji wetu Vian akaclear bill.siku ile ningeumbuka mpaka leo hata nikiingia bar huwa nauliza kwanza castler lager sh ngap ndo naagiza
 
Kabisa mkuu kuuliza sio ujinga🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom