Sitosahau nilivyokoswa na risasi nikiwa baa

Ilikua 2009 nikiwa Congo Eneo la Goma pembeni ya ilipojengwa ihusi hotel palikua na kiwanja kimoja hivi, tumeanza kupiga maji na akina Bisima, mara paaa waasi hao hapa, haikua na jinsi humo kulikua na staff wa UN kibao, wafanyabiashara na waganga njaa kama sisi, ubishi ubishi wakanikata panga mguu wa kushoto hadi mfupa nikausikia hadi leo nina kovu kubwa sana , jamaa aliekua rafiki yake bisima aliitwa Daniel alipigwa risasi ya kifuani alianguka namuona kabisa akafia pale pale, wale wajeshi waliokua nje kuwalinda mabosi wao walitokomea, nilikuja kuzinduka nakujielewa vizuri nipo upande wa rwanda dispensary, sitosahau tukio lile kwani lilibadilisha maisha yangu jumla na kuniacha na maumivu makubwa sana
 
Hii story namashaka nayo maana tukio nalojua mimi lilitokea art gallery pale braza mani mmoja anajifanya wa mjini jamaa wakaingia kumtafuta na machine
 
Kuna kijamaa kinaitwa Hans mtanashati kitakuja hapa kusema hii

Chai
 
pole sana kaka
 
Duh waas waliua tu wakasepa?awakuiba.?
 
Hii story namashaka nayo maana tukio nalojua mimi lilitokea art gallery pale braza mani mmoja anajifanya wa mjini jamaa wakaingia kumtafuta na machine
Tofauti sana na hii naifahamu hio tukio kabla mawella store kufunguliwa wala juliana bar & hotel haijawika kiivyo
 
Siku nyingine usikimbilie kaunta hilo ni eneo lengwa wakati wa ujambazi kimbilia chooni kama ukiona kulala chini ni hatari zaidi.
Cha msingi fuata amri yao, ukisha amrisha lala chini wewe lala, kitendo cha kikimbia hata uende chooni, wao wanajua unaenda kujipanga, wakikuona lazima wakuwashe.
 
Pole
Hongera
Hii ndio ukiskia paaah!
 
Kuna dada mmoja wa kisukuma aliuawa kwa shaba mjini masasi aliacha kazi benk akawa wakala wa bia wazee wa kazi wakamuotea kuwa ana cash ndani ile wamefika wamemuambia atoe pesa akaleta ubishi akpigwa shaba na mzigo ukachukuliwa
 
Pole sana mkuu, ulikua unawabishia nini? Walikuomba uwape mali ukakataa? Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…