Ilikua 2009 nikiwa Congo Eneo la Goma pembeni ya ilipojengwa ihusi hotel palikua na kiwanja kimoja hivi, tumeanza kupiga maji na akina Bisima, mara paaa waasi hao hapa, haikua na jinsi humo kulikua na staff wa UN kibao, wafanyabiashara na waganga njaa kama sisi, ubishi ubishi wakanikata panga mguu wa kushoto hadi mfupa nikausikia hadi leo nina kovu kubwa sana , jamaa aliekua rafiki yake bisima aliitwa Daniel alipigwa risasi ya kifuani alianguka namuona kabisa akafia pale pale, wale wajeshi waliokua nje kuwalinda mabosi wao walitokomea, nilikuja kuzinduka nakujielewa vizuri nipo upande wa rwanda dispensary, sitosahau tukio lile kwani lilibadilisha maisha yangu jumla na kuniacha na maumivu makubwa sana