Nakumbuka niliondoka kijijini kwetu kwenda mjini kusoma tuition likizo ya mwezi wa sita kipindi hicho niko kidato cha nne. Nilikaa mjini muda wa mwezi mzima. Ile siku narudi niko njiani kwa miguu mida ya jioni nilikutana na manzi nilikuwa namzimikia balaa. Akiwa bado mbali nilijiapiza siku hiyo lazima kieleweke maana nilishamfatilia hapo kabla lakini holaa! Tulipokutana nikamuomba asimame! Hakutaka, ikabidi nimlazimishe kusimama. Manzi alipandisha mori, mwanzo nilijua masihara, alinikwida akanirushia konde moja hapo ndo akili ilinikaa sawa. Ikabidi nijitetee. Nilimpa konde moja imeshiba, ilitua usawa wa kifua juu kidogo ya matiti, Dogo alienda chini bila kupenda pamoja na kuwa alikuwa ameshachana shati langu nikabakiwa na singred tu. Zilifuatia lawama kwenye familia japo baadae yaliisha.