Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Ku
Tembea uone Ndugu yangu...kuna sehemu nilifika nikakabidhiwa nyumba full kwa sh. 3000.....nikae kwa miezi mitatu...hiyo elfu tatu nilimpa balozi alienionyesha hiyo nyumba niishi....vijijini hizo nyumba ni nyingi sana tu...
Kuna kipindi tulienda kupiga kazi Songwe kwenye mgodi wa SHANTA gold mining
Tulipokuwa tunaelekea kuna kijiji tulipita makaburi yalikuwa ni mengi sana tukawauliza wenyeji kulikoni hapa.,.,

Wenyeji wakatuambia msiguse huku kuna moto atar.,... Na makaburi yote hayo mnayoyaona wengi wao ni umeme umewondoa kwa hyo kuweni makini...
 
Polen sana ndugu
 
HIV sio ugonjwa.
Halafu UKIMWI wa old model ulikuwa hatari ule kwa sababu ya kutokuwepo kwa dawa za kupunguza makali ya virusi. Nowdays kuna TLD, kuwatambua ni ngumu
 
HIV kule unapishana nayo kama binadamu
 
Pole sana mkuu.
 
Katika harakati zangu za kutafuta maisha, kuna siku nilikuwa SONGEA, nikafika mida ya jioni kama saa 12 hivi, nikachukua chumba lodge iliyokaribu na stendi.

Nikiwa room naweka vitu vyangu sawa ili nitoke, nikaona mfuko wa watsani ukiwa na vitu ndani umefungwa na kuwekwa kwenye uwazi uliopo baina ya kitanda na ukuta.

Nikauchukua nikaufungu, ndani nikakuta kikopo kidogo chenye vidonge nadhani vilikuwa kama vya kijivu hivi vikubwa kubwa kidogo. Pia nikakuta na karatasi inayoonesha muhusika alikuwa anahama hospitali ya kuchukulia ARV iliyopo DSM na kuanza kuchukulia dawa hospitali iliyopo songea. Nikakuta na night dress na hela kidgo kama 8000 hivi. Nikarudisha vile vitu halafu nikaufunga na kuweka pembeni nikiazimia nikitoka nikaupeleke mapokezi.

Baada ya dakika kadhaa mlango wangu ukagongwa niliposema karibu tu akaingia mdada moja kwa moja...dada alikuwa mzuri maashallah kajistiri vizuri na baibui pamoja na mtandio saafi. Akaenda moja kwa moja kwenye ukingo wa kitanda, nikamuona kashtuka baada ya kuona furushi lake halipo. Nikamwambia mzigo wako huu hapa chini ya meza nilipanga nikauwasilishe mapokezi. Akashukuru shukuru pale then akaondoka.

Nilipotoka mapokezi nikaulizia ilikuwaje mkanipa chumba ambacho mtu bado yupo? Wakasema HAPANA huyo dada alikuja na mtu wake wakalipia showtime na alipotoka tukakiweka sawa chumba. Nikauliza mnamjua yule dada? Wakasema eenh tunamjua vipi broo ulikuwa unamtaka uvushe nae usiku, ana bei nzuri tu....nikasema daaah WASHENZI HAWA WANANIDALALIA UKIMWI.

ANYWAY watu wameungua ndugu zangu, wameungua haswaaaa, TUENDELEE KUJILINDA.
 
Ni kweli ugonjwa anapanga mungu ila najitahidi kutembea na oral quick ili nimpime kabla ya game kwasababu kuna siku nilitaka kuyatimba.
 
Mafinga kuzuri mkuu, mambo mengine ni hivo kama ilivo asee...
 
Sema huu uzi unaogopesha saana, ila AFYA inapaswa kulindwa kwa namna yoyote ile. UKIMWI upo na unaua. Cha kushangaza siku hizi kampeni za kuelimisha kuhusu huu ugonjwa zimepotelea kusiko julikana
 
Tychob shida nini mkuu.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸš¬πŸš¬

Kufufua nyuzi kama hizi huo ni uchawi kama uchawi mwingine mkuu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sema huu uzi unaogopesha saana, ila inapaswa kulindwa kwa namna yoyote ile. UKIMWI upo na unaua. Cha kushangaza siku hizi kampeni za kuelimisha kuhusu huu ugonjwa zimepotelea kusiko julikana
saivi hakufi mtu maana kuna dawa unameza unakaa sawa unanenepa na kupendeza kabisa hadi hauwezi kumjua mwenye nao
 
Shida kwenye ndoa, wanaume sio waaaminifu kabisa wakiona Msichana ametulia hawakumbuki kabisa kondomu
Wee nani alikudanganya wanandoa wakicheat wanatumia condom 🀣🀣🀣🀣
Kataa ndoa kama wapenda afya yako. Msituone sie wajinga hatutaki kuoa mnasema vijana wa hovyo 🀣🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…