Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

hii dunia bana,unaweza pia ukabaki njia kuu ila wife akamtamani handsomeboy wa mtaani kwenu unakuja kuambukizwa hujui.

ila jamani kuna midada imeumbika aiseee
Waangalie tu mkuu,usiwatamani utakuja kunishukuru,shughuli yenyewe huwa haizidi hata nusu saa lakini majuto yake ni mabaya sana,usione watu wanajinyonga hata haachi ujumbe wengine unakuta ni mawazo,tena ukute una mke na watoto halafu umejiingiza kwenye huo upuuzi kwasababu ya tamaa,wanawake wenyewe siku hizi kila baada ya mita 10 kuna mwingine mzuri kuliko uliempita,utatembea na wangapi......
 
Kuna time napataga tamaa ya kuchepuka lkn nikifikilia ngwengwe najikuta mood yote inakata, hasa nikikumbuka watoto wangu bado wadogo! Nisha cancel promise kibao wakati tushapangana vzr tu na demu.
Mkuu huo ugonjwa kwa % kubwa huletwa na married couple hususani wanawake wenye tamaa ya pesa na ngono za nje kwa kisingizio cha kulizishwa, pia mchunge mkeo ukiona dalili zozote za kuchepuka usimsamehe achana nae immediately.
 
Mwanangu natetemeka hapa, naogopa mzee maana nami nishauguza na kuzika ndugu si chini ya wanne kwa huu ugonjwa...
Nikikumbuka zamani nilikua makini saana hata nikaamua kuoa mapema na kua muamifu ila ndoa ilipovunjika nimeingiwa na roho ya uhuni balaa tena mbaya zaidi siwezi kutumia mpira....
Naogopa kesho yangu namuomba Mungu anasaidie hii roho ya umalaya initoke maana nikijikaza wiki mpaka natetemeka nahisi homa na akili inavurugika sijui n nini hata... enhh Mola nisaidie....😥😥😥😥
 
Una mapepo.Nenda mwenyewe kanisa la EAGT mtaa uliopo.Kama unasali Moravian,Anglican,Batist hat Roma huwa kuna ibada ya waliokoka Jumapili inaitwa felloship/Newlife Church Christ.Fanya hivi waombe waliokoka wakuonyeshe wanapoabudu wakitoka kanisani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…