Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Na hawa mademu huku kama hawataki nataka na milio fulani kutaka izame yote.Hali ya ukimwi kwa sasa ni mbaya zaidi.TABIA YA KUKUINGILIANA KINYUME NA MAUMBILE NDO KABISA.UKIONA DEMU ANAFANYIWA VITU VIKUBWA UJUE ANATOA MDUARA NAJISI. Watch out
 
Sijui Bukoba nao wasemeje! Hilo gonjwa lisikie tu.
Huu Uzi unasisimua sanaa mm sitaki kuandika mengi....ila ukimwi wa 90's umetafuna wengi...

Watu wali ishia kusema wamerogwa na wengine baada ya kuupata waliamua kufa kishujaaa....

Kuna watu ukiwatizama Kwa kipimo Cha macho huwezi kuwa dhania....

Huu Uzi unatembea Kwa Kasi sanaa na I bet ni Uzi bora wa mwezi may (Uzi Bora wa mwezi may 2023)
 
Naandika uzi huu huku nikiwakumbuka wengi waliokufa na gonjwa la hatari la UKIMWI kule kwetu Iringa Mafinga kwenye misitu mbao mji wa biashara mji wenye viwanda vidogo vidogo vingi vya mbao mji wa majani ya Chaibora.

Mimi nilizaliwa mwaka 1990 DSM, baadae mwaka 1995 tukahamia mafinga mjini kikazi Mafinga ikiwa bado changa sana, mwaka 1997 nikiwa na miaka saba ndo nilipoanza kusikia hii term UKIMWI.

Mama yangu alikuwa anafanya kazi hospital ya Mafinga kama nurse pale sasa mara nyingi alikuwa anakuja na viperurushi navisoma nashangaa UKIMWI ni nini.

Jamani huu ugonjwa kama hujaoana mgonjwa UKIMWI anavyokufa huwezi elewa pia utaendelea kupiga kavu, lazima ushuhudie kama week mgonjwa kabla haja kata roho ndo utajua why HIV is king of all diseases hakuna kama HIV maana linaalika magonjwa yote. HIV/AIDS NI MFALME WA MAGONJWA sio utani.

Nisipoteze muda kifo cha kwanza nilihushudia jirani yetu alikuwa mwalimu alianza mume alikonda mwaka 1997, maskini afu walikuwa na watoto mapacha waliachwa bila wazazi asee jamaa alikonda kiasi hata mimi mtoto mdogo enzi hizo niliogopa na watu walikuwa hawataki kumgusa kabisa.

Kifo cha pili ba mkubwa wangu huyo yeye hakuchukua hata round alikuwa mlevi na UKIMIW wa enzi hizo ni miezi mitatu tunazika.

Haya sasa baada hapo tukahama mtaa tukamia mtaa mpya mtaa wa mikosi mkosi mkubwa hadi naandika uzi kwa uchungu mkubwa ni tulihamia ule mtaa mwaka 2003 hadi ninavyoongea 80% ya ule mtaa wamekufa na AIDS ule mtaa jamani wafanya wa Serikali walijenga sana nyumba maana serikali ilipima na kuwaanzia kwa bei nzuri wafanyakazi wengi wakahamia huko na kujenga majumba kumbe wamehamia mtaa mtoa roho mtaa na majanga yake.

Tulianza jirani mwanajeshi huyo tunafika akavuta ila mke wake hadi leo yupo anakula ARV, kanali yule tulizika tukiwa tumehamia ule mtaa week tu.

Upande mwingine alikuwa ni hakimu yule aliishi ishi akaja na kuvuta mama wa watu alikuwa na roho nzuri nahisi sijui nae UKIMWI alitoa wapi.

Kule idara ya maji dada mmoja mchaga alikuwa mtaani kwetu nae hivi she was beautiful japo nilikuwa mdogo huyo alikufa hata mtoto hakuacha alicha nyumba tu.

Kuna jirani yetu yeye pamoja na mke wameeacha mtoto wao mvuta bangi nao hivi huyu alikuwa fundi wa magari alijenga bonge la jumba mke alikuwa mzuri sana.

Pia upande wa juu kwa mbele mwanajeshi mmoja yeye na mke walikuwaga na baa walipishana tu miaka ule mtaa jamani sina hamu HIV iliwapiga fasta ikaacha watoto wakijilea.

Kuna mwamba pia pale kitaa alikuwa usalama wa taifa yeye ndo alikufa yeye na mdogo wake, huyo ni hivi mdogo wake alikula mke wa kaka yake nae akapata kaka yake anavyokufa akamwambia kama uliniabia mke wangu tutaonana very soon walikuwa wote watatu na mke juu wakaacha nyumba na katoto kachanga sijui kako wapi.

Haya dada mmoja mzuri sana alikuwa alijenga kijumba chake kipya kabisa akifanya kazi halmashauri nae kufika tu mafinga uzuri ulimponza tukazika akapenda hela za mpasua mbao mmoja tajiri miaka hiyo sijui yuko wapi alikuwa mweupe handsome alikuwa akiindesha shangingi miaka hiyo.

Wadau mtaaa ni mkubwa mno ule 80% ya zile nyumba zimejengwa wajenzi wake HIV iliwabeba.

Kila siku tukawa tunazika majirani tukijua kwetu salama 2012 babangu nae sijui alitoa wapi ila nilifuatialia nasikia alipata miaka ya 90 nae tukazika, sikuwa na mahusiano mazuri na dingi hivyo hata msiba niliona normal tu nikamuuliza maza akasema si unajua mimi na baba ako tuliachana mmi mzima.

Basi miaka ikaenda hadi mwaka 2018 nilikuwa nimetoka zangu China nikaenda Iringa kumpa hi maza, mara kuingia chumbani nakuta ARV kasahau kitandani asee nililia sana nikamuuliza akaniambia samahani niliwaficha wanangu nikambatia kwa uchungu mkubwa sana siku kesho yake nikarudi Dar nikisema why why mama angu nurse nae anaondoka.

2020 akaanza kuumwa kumbe nae aliishia nao kimya kimya toka miaka 2000 mwanzoni, 2021 kuiukweli HIV/AIDS hapa ilionesha uwezo wake ilimua mama yangu kikatili mno siwezi simulia.

Basi wadau nasema kutoka moyo ule mtaa wetu 80% nyumba zimebaki za urithi tu siwezi taja mtaa ila una jina la herufi tu, kama uko mafinga utakuwa umeshaujua ni kwa kishua sana.

Research niliyofanya why UKIMWI uliua sana mafinga ni padogo pia na walio kufa sana ni wafanyakazi serikali ilikuwa ikileta wafanyakazi miaka ile ya 90 wanaambukizana sana bila kujua so wafanyakazi wengi mafinga miaka 90 kuna 2000 mwanzoni walikufa na HIV wengi ni wageni kutoka mikoa mingine including my mom.

Kuna makaburi yanaitwa MET 50% half ya marehemu pale watu wa UKIMWI wa miaka 90.

RIP To those beautiful souls, nimesimulia machache sana kuhusu mafinga na HIV, ni mengi mno nimeacha na niliyoshuhudia toka 1996.

Nilihama sijawahi kanyaga tena hata nyumba tuliuza kwa hasira maana majirani wote wamekufa now naishi Dar kama business man.

Huwa sipigi demu bila kupima pia mtumiaji mzuri wa condom.

Uzi wa leo asubuhi asanteni ila Mafinga never forget japo napapenda sana. Familia ilihamia kikazi mji ule kumbe tulienda mazikoni, kuweni makini na Mafinga wafanyakazi mnaoenda hapo, bahati yenu kumetulia ila miaka ile asee hapana.
Mama yako huwezi jua labda aliipata HIV kutokana na kazi yake, Nurse yupo kwenye high risk ya kupata HIV
 
Its true,na inasemekana kuwa hawa wanaotumia dawa ukienda kupima na rapid test wadudu hawaonekani,yaani nikiwaza hapo nasema wacha tu nibaki njia kuu maana nimeshapoteza marafiki na ndungu wengi sana,nakumbuka katika jamaa waliotangulia kuna aliyefikia mpaka kutoka funza kwenye mwili ni kama alikuwa anaoza,aisee hii kitu ni hatari sana,HIV is real...
Nilimzika mama yangu akitoa funza aisee [emoji24]
 
Ngoma ipo na inawaunguza watu ndani kwa ndani, kilichopo ni ARV ndo mficha maradhi, wapo watoto walizaliwa na ukimwi ila wana afya njema kwa hisani ya vidonge, wapiga kavukavu kazi mnayo. kiwanda kingine kinachozalisha ukimwi ni madada poa, hawa wana dau la kavukavu na dau la kondom, ajabu mtu anaongeza dua ili apige kavu kumbe ndo ananunua ukimwi, na haka kamtindo ka anal sex ndo balaa maana friction ni kubwa unapata fresh HIV, utani mwingine ni hawa wanaojipima, kumezuka biashara ya kitembea na vipimo, mnapima ndo mnapiga game, well and good but sio 100% guarantee, ndo maana hili jambo linafanyika hospital, kuna ishu ya utunzaji wa kifaa unaoweza kuadhiri ufanisi wa kipimo, pia kuna expire date sidhan kama wanaangalia, cha ziada kuna kitu kinaitwa "window period" yaan kipind kati ya kupata maambukizi mpaka mda wa ugonjwa kuonekana kwenye kipimo, zamani ilikuwa miezi 3, ila sikuhz ni mwezi mmoja, sasa kama dem kapata ngoma wiki iliyopita, kuna uwezekano ukimpima asome negative lakini ukila kavu unapata ngoma, ndo maana hata hospital ukipima unaambiwa rudi baada ya muda kurudia vipimo, somo ni kuwa majibu ya kujipima sio ya kutegemea 100%, bora mkapime hospital mpate na ushauri wa kitaalamu.
Hivyo bado suluhisho la ukimwi ni zilezile sentensi 3, ..... 1. jiepushe kabisa na ngono.. 2. kuwa na mpenzi mmoja na wote muwe waaminifu 3. tumia kondom ,
kondom itumike kwa usahihi na itunzwe vizuri, kuna watu wanatembea na condom kwenye wallet mwishowe zinapoteza ubora, pia kuna mafuta yakikutana na condom yanazidhoofisha inapasuka katikati ya show... kwahyo wale wazee wa vilainishi tumieni vilainishi ambavyo ni water based na sio oil based..
Is water-based lubricant best for condoms?

"
Water-based or silicone lube are always safe to use with any kind of condom. Don't use anything that has oil in it, like lotion, vaseline, or oil-based lubes with latex condoms. Oil can damage latex condoms and make them break"

unakuta mtu anakomaa na mafuta ya nazi ndo kilainishi, hapo kondom itachanika na utaenda na maji, kanunue tu KY firauni wewe

""Coconut oil cannot be used with latex condoms because it can break down the latex and cause the condom to break," explained Dr. Landry. Only water- and silicone-based lubricants can be used with latex condoms without risking breakage, said Dr. Landry""

so wazee wa kazi tujilinde na tuwalinde wenza wetu, point sio wivu au kuchapiwa bali point ni kutoleteana magonjwa nyumbani, ndo maana nawaelewa wanaotoa adhabu kali pale wanapofumania, we umetulia zako uko busy na kaz kumbe kuna kijana anaruka na wife, kamata kijana chomoa viungo, aende akamtumikie muumba wake.
"UKIMWI UNAUA, HAUNA KINGA WALA DAWA'
 
Asante mtoa mada kwa kutukumbusha.
Yawezekana huu uzi ukaokoa afya ya mtu.
Kwangu huu ndio uzi bora JF wa 2023.❤️
Hakuna kitu naogopa kupoteza kama afya yangu.
Wapendwa UKIMWI bado upo na unatesa sana msidanganyike na ARV .
 
Mama yako huwezi jua labda aliipata HIV kutokana na kazi yake, Nurse yupo kwenye high risk ya kupata HIV
Nikiwa kama mdau wa afya MWANDAMIZI (senior)

Kuna jamaa alikuja dar so Arvs zake zikaisha so akaniomba am 4 real nimchukulie za kusukuma siku mpaka atakapo Rudi mkoani kwake.......

Nikamcheki mshikaji wangu Y nikamwambia anichukulie akanambia nipo ofsn njoo uchukue.........
Ni dokta kijana alikua ana muhudumia mmama mmoja ni mteja etu nyumbani.....
Kwa bahati mbaya Ile sindano aliyo mchoma mama yule ikamchoma na yeye....
Nikakuta na yeye anazitumia zile dozi....
Niliwaza sana siku iyo..
 
Back
Top Bottom