Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Its true,na inasemekana kuwa hawa wanaotumia dawa ukienda kupima na rapid test wadudu hawaonekani,yaani nikiwaza hapo nasema wacha tu nibaki njia kuu maana nimeshapoteza marafiki na ndungu wengi sana,nakumbuka katika jamaa waliotangulia kuna aliyefikia mpaka kutoka funza kwenye mwili ni kama alikuwa anaoza,aisee hii kitu ni hatari sana,HIV is real...
Na shida unabaki high way mwenzako anachochora
 
Duh!!!
HIV kill Mimi nilishuhudia Kwa Uncle wangu alikuwa na Bonge la mwili kama wangu yani uncle alikuwa na kitambi kama Yule marehemu Komba siku alipoanza kuumwa 2016 hiyo aisee uncle alikonda sana mpaka nilikuwa na huwezo wa kumbeba peke yangu.
SHETANI NI MS*NG* SANA YANI AMEWEKA MCHANGA KWENYE ASALI [emoji22]
Mseveni wa Uganaga alishasema hiv !!


Despite knowing the address of HIV /AIDS we still like going there and easily get killed ….



Licha ya kujua kuwa kwenye kma na Mb’o kuna ukimwi bado tunapenda kwenda kule na matokeo yake tunauliwa kiraisi
 
Naandika uzi huu huku nikiwakumbuka wengi waliokufa na gonjwa la hatari la UKIMWI kule kwetu Iringa Mafinga kwenye misitu mbao mji wa biashara mji wenye viwanda vidogo vidogo vingi vya mbao mji wa majani ya Chaibora.

Mimi nilizaliwa mwaka 1990 DSM, baadae mwaka 1995 tukahamia mafinga mjini kikazi Mafinga ikiwa bado changa sana, mwaka 1997 nikiwa na miaka saba ndo nilipoanza kusikia hii term UKIMWI.

Mama yangu alikuwa anafanya kazi hospital ya Mafinga kama nurse pale sasa mara nyingi alikuwa anakuja na viperurushi navisoma nashangaa UKIMWI ni nini.

Jamani huu ugonjwa kama hujaoana mgonjwa UKIMWI anavyokufa huwezi elewa pia utaendelea kupiga kavu, lazima ushuhudie kama week mgonjwa kabla haja kata roho ndo utajua why HIV is king of all diseases hakuna kama HIV maana linaalika magonjwa yote. HIV/AIDS NI MFALME WA MAGONJWA sio utani.

Nisipoteze muda kifo cha kwanza nilihushudia jirani yetu alikuwa mwalimu alianza mume alikonda mwaka 1997, maskini afu walikuwa na watoto mapacha waliachwa bila wazazi asee jamaa alikonda kiasi hata mimi mtoto mdogo enzi hizo niliogopa na watu walikuwa hawataki kumgusa kabisa.

Kifo cha pili ba mkubwa wangu huyo yeye hakuchukua hata round alikuwa mlevi na UKIMIW wa enzi hizo ni miezi mitatu tunazika.

Haya sasa baada hapo tukahama mtaa tukamia mtaa mpya mtaa wa mikosi mkosi mkubwa hadi naandika uzi kwa uchungu mkubwa ni tulihamia ule mtaa mwaka 2003 hadi ninavyoongea 80% ya ule mtaa wamekufa na AIDS ule mtaa jamani wafanya wa Serikali walijenga sana nyumba maana serikali ilipima na kuwaanzia kwa bei nzuri wafanyakazi wengi wakahamia huko na kujenga majumba kumbe wamehamia mtaa mtoa roho mtaa na majanga yake.

Tulianza jirani mwanajeshi huyo tunafika akavuta ila mke wake hadi leo yupo anakula ARV, kanali yule tulizika tukiwa tumehamia ule mtaa week tu.

Upande mwingine alikuwa ni hakimu yule aliishi ishi akaja na kuvuta mama wa watu alikuwa na roho nzuri nahisi sijui nae UKIMWI alitoa wapi.

Kule idara ya maji dada mmoja mchaga alikuwa mtaani kwetu nae hivi she was beautiful japo nilikuwa mdogo huyo alikufa hata mtoto hakuacha alicha nyumba tu.

Kuna jirani yetu yeye pamoja na mke wameeacha mtoto wao mvuta bangi nao hivi huyu alikuwa fundi wa magari alijenga bonge la jumba mke alikuwa mzuri sana.

Pia upande wa juu kwa mbele mwanajeshi mmoja yeye na mke walikuwaga na baa walipishana tu miaka ule mtaa jamani sina hamu HIV iliwapiga fasta ikaacha watoto wakijilea.

Kuna mwamba pia pale kitaa alikuwa usalama wa taifa yeye ndo alikufa yeye na mdogo wake, huyo ni hivi mdogo wake alikula mke wa kaka yake nae akapata kaka yake anavyokufa akamwambia kama uliniabia mke wangu tutaonana very soon walikuwa wote watatu na mke juu wakaacha nyumba na katoto kachanga sijui kako wapi.

Haya dada mmoja mzuri sana alikuwa alijenga kijumba chake kipya kabisa akifanya kazi halmashauri nae kufika tu mafinga uzuri ulimponza tukazika akapenda hela za mpasua mbao mmoja tajiri miaka hiyo sijui yuko wapi alikuwa mweupe handsome alikuwa akiindesha shangingi miaka hiyo.

Wadau mtaaa ni mkubwa mno ule 80% ya zile nyumba zimejengwa wajenzi wake HIV iliwabeba.

Kila siku tukawa tunazika majirani tukijua kwetu salama 2012 babangu nae sijui alitoa wapi ila nilifuatialia nasikia alipata miaka ya 90 nae tukazika, sikuwa na mahusiano mazuri na dingi hivyo hata msiba niliona normal tu nikamuuliza maza akasema si unajua mimi na baba ako tuliachana mmi mzima.

Basi miaka ikaenda hadi mwaka 2018 nilikuwa nimetoka zangu China nikaenda Iringa kumpa hi maza, mara kuingia chumbani nakuta ARV kasahau kitandani asee nililia sana nikamuuliza akaniambia samahani niliwaficha wanangu nikambatia kwa uchungu mkubwa sana siku kesho yake nikarudi Dar nikisema why why mama angu nurse nae anaondoka.

2020 akaanza kuumwa kumbe nae aliishia nao kimya kimya toka miaka 2000 mwanzoni, 2021 kuiukweli HIV/AIDS hapa ilionesha uwezo wake ilimua mama yangu kikatili mno siwezi simulia.

Basi wadau nasema kutoka moyo ule mtaa wetu 80% nyumba zimebaki za urithi tu siwezi taja mtaa ila una jina la herufi tu, kama uko mafinga utakuwa umeshaujua ni kwa kishua sana.

Research niliyofanya why UKIMWI uliua sana mafinga ni padogo pia na walio kufa sana ni wafanyakazi serikali ilikuwa ikileta wafanyakazi miaka ile ya 90 wanaambukizana sana bila kujua so wafanyakazi wengi mafinga miaka 90 kuna 2000 mwanzoni walikufa na HIV wengi ni wageni kutoka mikoa mingine including my mom.

Kuna makaburi yanaitwa MET 50% half ya marehemu pale watu wa UKIMWI wa miaka 90.

RIP To those beautiful souls, nimesimulia machache sana kuhusu mafinga na HIV, ni mengi mno nimeacha na niliyoshuhudia toka 1996.

Nilihama sijawahi kanyaga tena hata nyumba tuliuza kwa hasira maana majirani wote wamekufa now naishi Dar kama business man.

Huwa sipigi demu bila kupima pia mtumiaji mzuri wa condom.

Uzi wa leo asubuhi asanteni ila Mafinga never forget japo napapenda sana. Familia ilihamia kikazi mji ule kumbe tulienda mazikoni, kuweni makini na Mafinga wafanyakazi mnaoenda hapo, bahati yenu kumetulia ila miaka ile asee hapana.
Hujawahi muona mgonjwa wa aggressive cancer
Si bora ukimwi unaweza ishi hata miaka 20 aggressive cancer ndani ya miezi kinakua ni kipindi cha mateso makali sana mgonjwa ni analia mda wote au anaugumia maumivu mda wote
 
Wewe neenda kwenye wadi ya saratani ndo utajua ukimwi ni cha mtoto na inaua watu wazima na consciousness yao kwa % kubwa, kule cancer inaua watoto wadogo wazee vijana, masikini wenye pesa kila aina ya mtu. Ukimwi ni hatari ila is over rated kwasbb ni ajira kwa mashirika mengi na misaada kwa serikali zetu........je wa jua kwamba Malaria inaua watu hapa Africa Tanzania ikiwemo kuliko HIV? kila baada ya dakika 3 kuna mtu anakufa kwa Malaria hususani watoto walioko chini ya 5yrs infants......mtu anauwezo wakuishi na ukimwi kwa zaidi ya miaka 30, kinacho ua wa Tanzania ni umasikini ulio kithiri kupata chakula sahihi na dawa kwa wakati ila sio HIV
Exactly
Cancer hapana aisee bora ukimwi
 
Nilivyo ona neno Mafinga Iringa, nimeishia hapo kusoma...
Nyanda za juu kusini hasa hasa Iringa, ukimwi upo kila nyumba kila mtaa, si jambo la kushangaza...
Sababu 1. Imani potofu kuhusu tohara; hivyo jamii kubwa haijapata tohara na kisayansi mtu govi ni rahisi kupata michubuko na maambukiz ya UKIMWI wakat wa kujamiana
Pia Iringa Ina muingiliano sana madereva wa malori wa Nchi za nje wanapenda kulala iringa plus biashara za mazao zinaleta sana wageni pia hii imechagia sana all in all aliyeleta ARV ajengewe sanamu
 
Back
Top Bottom