Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Naandika uzi huu huku nikiwakumbuka wengi waliokufa na gonjwa la hatari la UKIMWI kule kwetu Iringa Mafinga kwenye misitu mbao mji wa biashara mji wenye viwanda vidogo vidogo vingi vya mbao mji wa majani ya Chaibora.

Mimi nilizaliwa mwaka 1990 DSM, baadae mwaka 1995 tukahamia mafinga mjini kikazi Mafinga ikiwa bado changa sana, mwaka 1997 nikiwa na miaka saba ndo nilipoanza kusikia hii term UKIMWI.

Mama yangu alikuwa anafanya kazi hospital ya Mafinga kama nurse pale sasa mara nyingi alikuwa anakuja na viperurushi navisoma nashangaa UKIMWI ni nini.

Jamani huu ugonjwa kama hujaoana mgonjwa UKIMWI anavyokufa huwezi elewa pia utaendelea kupiga kavu, lazima ushuhudie kama week mgonjwa kabla haja kata roho ndo utajua why HIV is king of all diseases hakuna kama HIV maana linaalika magonjwa yote. HIV/AIDS NI MFALME WA MAGONJWA sio utani.

Nisipoteze muda kifo cha kwanza nilihushudia jirani yetu alikuwa mwalimu alianza mume alikonda mwaka 1997, maskini afu walikuwa na watoto mapacha waliachwa bila wazazi asee jamaa alikonda kiasi hata mimi mtoto mdogo enzi hizo niliogopa na watu walikuwa hawataki kumgusa kabisa.

Kifo cha pili ba mkubwa wangu huyo yeye hakuchukua hata round alikuwa mlevi na UKIMIW wa enzi hizo ni miezi mitatu tunazika.

Haya sasa baada hapo tukahama mtaa tukamia mtaa mpya mtaa wa mikosi mkosi mkubwa hadi naandika uzi kwa uchungu mkubwa ni tulihamia ule mtaa mwaka 2003 hadi ninavyoongea 80% ya ule mtaa wamekufa na AIDS ule mtaa jamani wafanya wa Serikali walijenga sana nyumba maana serikali ilipima na kuwaanzia kwa bei nzuri wafanyakazi wengi wakahamia huko na kujenga majumba kumbe wamehamia mtaa mtoa roho mtaa na majanga yake.

Tulianza jirani mwanajeshi huyo tunafika akavuta ila mke wake hadi leo yupo anakula ARV, kanali yule tulizika tukiwa tumehamia ule mtaa week tu.

Upande mwingine alikuwa ni hakimu yule aliishi ishi akaja na kuvuta mama wa watu alikuwa na roho nzuri nahisi sijui nae UKIMWI alitoa wapi.

Kule idara ya maji dada mmoja mchaga alikuwa mtaani kwetu nae hivi she was beautiful japo nilikuwa mdogo huyo alikufa hata mtoto hakuacha alicha nyumba tu.

Kuna jirani yetu yeye pamoja na mke wameeacha mtoto wao mvuta bangi nao hivi huyu alikuwa fundi wa magari alijenga bonge la jumba mke alikuwa mzuri sana.

Pia upande wa juu kwa mbele mwanajeshi mmoja yeye na mke walikuwaga na baa walipishana tu miaka ule mtaa jamani sina hamu HIV iliwapiga fasta ikaacha watoto wakijilea.

Kuna mwamba pia pale kitaa alikuwa usalama wa taifa yeye ndo alikufa yeye na mdogo wake, huyo ni hivi mdogo wake alikula mke wa kaka yake nae akapata kaka yake anavyokufa akamwambia kama uliniabia mke wangu tutaonana very soon walikuwa wote watatu na mke juu wakaacha nyumba na katoto kachanga sijui kako wapi.

Haya dada mmoja mzuri sana alikuwa alijenga kijumba chake kipya kabisa akifanya kazi halmashauri nae kufika tu mafinga uzuri ulimponza tukazika akapenda hela za mpasua mbao mmoja tajiri miaka hiyo sijui yuko wapi alikuwa mweupe handsome alikuwa akiindesha shangingi miaka hiyo.

Wadau mtaaa ni mkubwa mno ule 80% ya zile nyumba zimejengwa wajenzi wake HIV iliwabeba.

Kila siku tukawa tunazika majirani tukijua kwetu salama 2012 babangu nae sijui alitoa wapi ila nilifuatialia nasikia alipata miaka ya 90 nae tukazika, sikuwa na mahusiano mazuri na dingi hivyo hata msiba niliona normal tu nikamuuliza maza akasema si unajua mimi na baba ako tuliachana mmi mzima.

Basi miaka ikaenda hadi mwaka 2018 nilikuwa nimetoka zangu China nikaenda Iringa kumpa hi maza, mara kuingia chumbani nakuta ARV kasahau kitandani asee nililia sana nikamuuliza akaniambia samahani niliwaficha wanangu nikambatia kwa uchungu mkubwa sana siku kesho yake nikarudi Dar nikisema why why mama angu nurse nae anaondoka.

2020 akaanza kuumwa kumbe nae aliishia nao kimya kimya toka miaka 2000 mwanzoni, 2021 kuiukweli HIV/AIDS hapa ilionesha uwezo wake ilimua mama yangu kikatili mno siwezi simulia.

Basi wadau nasema kutoka moyo ule mtaa wetu 80% nyumba zimebaki za urithi tu siwezi taja mtaa ila una jina la herufi tu, kama uko mafinga utakuwa umeshaujua ni kwa kishua sana.

Research niliyofanya why UKIMWI uliua sana mafinga ni padogo pia na walio kufa sana ni wafanyakazi serikali ilikuwa ikileta wafanyakazi miaka ile ya 90 wanaambukizana sana bila kujua so wafanyakazi wengi mafinga miaka 90 kuna 2000 mwanzoni walikufa na HIV wengi ni wageni kutoka mikoa mingine including my mom.

Kuna makaburi yanaitwa MET 50% half ya marehemu pale watu wa UKIMWI wa miaka 90.

RIP To those beautiful souls, nimesimulia machache sana kuhusu mafinga na HIV, ni mengi mno nimeacha na niliyoshuhudia toka 1996.

Nilihama sijawahi kanyaga tena hata nyumba tuliuza kwa hasira maana majirani wote wamekufa now naishi Dar kama business man.

Huwa sipigi demu bila kupima pia mtumiaji mzuri wa condom.

Uzi wa leo asubuhi asanteni ila Mafinga never forget japo napapenda sana. Familia ilihamia kikazi mji ule kumbe tulienda mazikoni, kuweni makini na Mafinga wafanyakazi mnaoenda hapo, bahati yenu kumetulia ila miaka ile asee hapana.
Siku hizi ARV inasaidia sana , ule UKIMWI wa Sofia haupo tena. Wanakufa watu na vitambi vyao bila vipele wala kuharisha na maambukizi kwa watumia dawa ni kidogo sana.

Tatizo la HIV unaweza ukatulia wewe na kuwa makini sana lkn mwezi wako akakuletea ndani ya nyumba hasa mkioana Malaya na waongo waongo 😭😭😭
 
Huu ugonjwa haukuwa na mchezo na tumepoteza watu wengi sana, kwa sasa ni jambo la kushukuru mungu maana hizi ARV ukila vizuri na ukajiangalia vizuri kiafya unaweza kusihi maisha ya kawaida kabisa mpaka ukawa mzee bila matatizo, sio death sentence kama miaka ile, kwa sasa mambo ya pressure, kisukari, cancer ni hatari kuliko hata ukimwi, binadamu hatuko salama tunashambuliwa kila kona
 
Familia ilihamia kikazi mji ule kumbe tulienda mazikoni, kuweni makini na Mafinga wafanyakazi mnaoenda hapo, bahati yenu kumetulia ila miaka ile asee hapana.
Asante kwa ushauri mujarabu mkuu. BTW kumbuka unaweza kuvaa kondomu ukafa lakini ukapiga kavu uka survive. Kuvaa kondomu sio guarantee ya kutoambukizwa.
 
Iringa ni home na umezungumza ukwel japo Mafinga hapo mbona pa kirembo sana..
2010 February baada ya kumaliza kidato cha sita nilipata kazi kwenye volunteering program flan ilikua inajulikana kama student partnership worldwide (SPW) now days wanajiita RESTLESS DEVELOPMENT hii organization ilikua inajihusisha na mambo hizo za UKIMWI na Peer education.

Nilifanya kazi sana Njombe, Ludewa na Makete..zaid zaid Ludewa na Vijiji vyake..Lugarawa..Masimbwe...Itundu... n.k.

Aisee kule ukimwi ulikua UNAOUNA KWA MACHO HIVIIIII yan huhitaji kipimo wala nini.Watoto wadogoo vijana watu wazima kwa wazee jinsia zote ukimwi ulikua unafagia sanaaaaa..

Nashkuru Mungu those days nilikua sijaanza kuchakata bado.
E bwana ukimwi ni noma sana.
Those days elimu rika ilikua adimu sana na kwakwel moja ya vitu najivunia nilifanya kwenye maisha yangu ya u teeneger basi ni mojawapo.

Tulikua tunapiga sana semina.
Mnaandaa matamasha ya muziki kutoa elimu nakumbuka sana pande za ULAYAS secondary pale Mlangali Ludewa...Anzisha sana maktaba za kujisomea kutengeneza HIV Awareness kwa vijana ... ligi la soka ambazo zilikua zinaambatana na Semina na upimaji wa HIV ..

Ukimwi umetafuta sana nyanda za juu kusini magharib.Sanaaa yani.
Kilimo cha chai na miti kama kichocheo cha maambukizi..
IKUMBUKWE maeneo hayo yalikua maarufu sana kutoa ma house girl.Wakija Dar wanaukwaa ukimwi wakianza kuumwa wanarudishwa Huku vijijin wazaz wasio na elimu ya kuwahudumia wanaambukizwa..plus pisi imetoka mjini vijana wa village nao wanapambana japo waonje ...Imooooo..
Dah ukimwi ni nyokoo sanaaaa.

But now days angalau hali ime stablize..

Nakumbuka pale Mlangali nilishakutana na li shangazi Nurse limoja hakyanan lile lilikua linataka nili gonge kila mitego aliniwekea haikunasa maana akili yangu kipinzi hiko badoo hata mbususu sizijui so nikawa hata sielewi yule mama anataka nini 😄😄😄😄..

All in all AIDS Kills.
Tatizo mojawapo kwasasa watu tumesusa Kampeni za kuijengea jamii HIV AWARENES sawa kuna mitandao siku hiz ndio ila hili la kila mtu kujifunza kibinafs ni hatar sana maa internet is full of wrong information.

TUJILINDE..TUJIKINGE
Katika kitu namshukuru Mungu nlikuwa well grounded kwenye elimu ya jinsia na mahusiano! Kulikuwa na programs nyingi zilikuwa funded na wajapan kupitia world vision Tanzania, mwaka 2009 nkiwa darasa la tatu nlishapelekwa kwenye semina tunaandaa ngonjera na Kazi mbali mbali Sanaa ambapo tar December 1 ndo inakuaga maadhimisho yake.

Pia tulikua tunaenda semina za wiki Moja au mbili kuhus mambo ya watoto na tar 16/6 tulikua tunashiriki maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika.

Haya yote yalitamatika nlipomaliza elimu ya msingi 2013 though vilinijenga Sana kua na fikra pana
 
Nimejikuta nakuonea huruma sana mkuu.Kitendo cha mkeo kuwa na trip daily ina leta confussion sana.Mara nying hata stability ya family huwa inakua at jeopardy sana

Nafikiria nimwambie kazi na ndoa/watoto ipi bora?
Haiwezekani kwa mwezi tunaonana kwa siku 7 tu imefikia hatua watoto wamemzoea dada wa kazi
 
Sasa niukwae mara ngapi jamani sixteen years and counting hamna arv wala nini siri ni mazoezi chakula na kitokuoa maana ukiwa na mke unaongeza uharaka wa kulifikia kaburi lako [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] oh plus maji kwa wingi pia
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Dah so sad kuna jamaa yetu hapa mtaani juzi aliamua kujinyonga kisa ana Ukimwi😭.
Ni ugonjwa hatari sana unahitaji maombi na umakini wa hali ya juu kuuepuka... Ukishaupata unapoteza ramani ya maisha kabisa...... Inauma na isikitisha ni gonjwa linalogusa kila familia kwa sasa.

Rip my beloved bro!.
 
Mkuu huo ugonjwa kwa % kubwa huletwa na married couple hususani wanawake wenye tamaa ya pesa na ngono za nje kwa kisingizio cha kulizishwa, pia mchunge mkeo ukiona dalili zozote za kuchepuka usimsamehe achana nae immediately.
Hiyo iko wazi kama ya mbuzi, nishamwambia nikikudaka ni no sorry
 
Wewe neenda kwenye wadi ya saratani ndo utajua ukimwi ni cha mtoto na inaua watu wazima na consciousness yao kwa % kubwa, kule cancer inaua watoto wadogo wazee vijana, masikini wenye pesa kila aina ya mtu. Ukimwi ni hatari ila is over rated kwasbb ni ajira kwa mashirika mengi na misaada kwa serikali zetu........je wa jua kwamba Malaria inaua watu hapa Africa Tanzania ikiwemo kuliko HIV? kila baada ya dakika 3 kuna mtu anakufa kwa Malaria hususani watoto walioko chini ya 5yrs infants......mtu anauwezo wakuishi na ukimwi kwa zaidi ya miaka 30, kinacho ua wa Tanzania ni umasikini ulio kithiri kupata chakula sahihi na dawa kwa wakati ila sio HIV
Hapa ndo mwengi hawana uelewa wa Nini maana ya HIV. Huu si ugonjwa ni upungufu wa Kinga hivyo magonjwa yote yatakufata Kinga ikipungua
 
Back
Top Bottom