Hii issue nikikua early 90s hasa hasa hii miaka miwili 1998/2000 nakumbuka kusikiliza kwenye taarifa ya habari RTD (TBC ya sasa) kwamba moja ya wilaya za Tanzania kuzungushiwa utepe mwekundu kutokana na kuongoza kwa vifo vilivyotokana na HIV/AIDS,nahisi ni hii hii Mafinga.
Pole sana hauko peke yako,hakuna Tanzania hii aliyekwepa hili zimwi iwe ni kwa wajomba,shangazi,baba wadogo etc mimi niliwahi zika mpaka babu yangu mdogo 2007 na mwanae alizikwa 1997 kisababishi kikiwa huu huu UKIMWI na mzee alikuwa na jeuri yule aliambiwa atumie ARVs akakataa akasema kama alivyokuwa anafurahia utamu anataka kuuona uchungu nao unafananaje,alikufa mzee aged 70.