Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Its true,na inasemekana kuwa hawa wanaotumia dawa ukienda kupima na rapid test wadudu hawaonekani,yaani nikiwaza hapo nasema wacha tu nibaki njia kuu maana nimeshapoteza marafiki na ndungu wengi sana,nakumbuka katika jamaa waliotangulia kuna aliyefikia mpaka kutoka funza kwenye mwili ni kama alikuwa anaoza,aisee hii kitu ni hatari sana,HIV is real...
Akiwa anatumia dawa vizur hupati
 
Wewe umeongea kitu cha msingi ambacho watu wengi hawakielewi.

Wanadhani eti virusi vinapitia ktk michubuko ya uume kwa nje tu. Wakati kumbe virusi vinapita kwenye ngozi laini ya ndani ya tundu la uume (Epithelium cells). Hizo cells ndo zina receptors nyingi za wadudu wa HIV kuliko hata lingozi la nje
Nakataa. Kirusi hakitembei bila media sasa yale maji maji ya ukeni yanasafirije kwenda huko? Halafu maji maji ya ukeni kama mwanamke anatumia dozi basi yanakuwa na maambikizi very rare. Bila michubuko no HIV transmission ndiyo maana tulihimizwa jando ili kuimarisha ngozi ya uume isipate michubuko kirahisi wakati wa tendo halali. Yani kama ukifanya mapenzi unachubuka basi jitafakari sana!
 
Hii issue nikikua early 90s hasa hasa hii miaka miwili 1998/2000 nakumbuka kusikiliza kwenye taarifa ya habari RTD (TBC ya sasa) kwamba moja ya wilaya za Tanzania kuzungushiwa utepe mwekundu kutokana na kuongoza kwa vifo vilivyotokana na HIV/AIDS,nahisi ni hii hii Mafinga.

Pole sana hauko peke yako,hakuna Tanzania hii aliyekwepa hili zimwi iwe ni kwa wajomba,shangazi,baba wadogo etc mimi niliwahi zika mpaka babu yangu mdogo 2007 na mwanae alizikwa 1997 kisababishi kikiwa huu huu  UKIMWI na mzee alikuwa na jeuri yule aliambiwa atumie ARVs akakataa akasema kama alivyokuwa anafurahia utamu anataka kuuona uchungu nao unafananaje,alikufa mzee aged 70.
Hukuwahi kuisikia Makete wewe. Niliwahi kwenda Makete miaka ya 2000 nikiwa mdogo makaburi niliyokuwa nayaona kwenye familia karibu nichizike! Unakuta familia imetandaza mkeka makaburi zaidi ya 10 na ni nyumba kwa nyumba. Achilia mbali hao wagonjwa waliojilaza nje kwenye vizulia kimguu na kipaja ukiangalia unaweza kukimbia. Aisee nyie acheni huu UKIMWI ukae tu kama ulivyo miaka hii. Vinginevyo!!!
 
Chifu ukimwi hauna mfanano. Huu ugonjwa acha kabisa. Ugonjwa ambao mume anakula arv mkewe hajui au mke anakula arv mumewe hajui na hapo unakuta wanaendelea kuzaa!Wazazi wanakula arv watoto hawajui.

Kwenye mazishi cv ya ugonjwa wa marehem inabadilishwa. Ukitaka kujua jiulize hapa kuna comment 400+ kuna wachangiaji wangapi wamekiri kuwa na shida hii na ujiulize je ni kweli hamna mwenye shida hiyo? acha kabisa Ukimwi baba lao aisee.
 
Chifu ukimwi hauna mfanano. Huu ugonjwa acha kabisa. Ugonjwa ambao mume anakula arv mkewe hajui au mke anakula arv mumewe hajui na hapo unakuta wanaendelea kuzaa!Wazazi wanakula arv watoto hawajui.

Kwenye mazishi cv ya ugonjwa wa marehem inabadilishwa. Ukitaka kujua jiulize hapa kuna comment 400+ kuna wachangiaji wangapi wamekiri kuwa na shida hii na ujiulize je ni kweli hamna mwenye shida hiyo? acha kabisa Ukimwi baba lao aisee.
Ndugu yangu mzabzab ndiye pekee amekiri wazi, anastahili tuzo huyu mwamba. Sie wengine zaidi ya porojo hatuna la kuongeza 😅😅😅 japo mimi status yangu kweli siijui, sijui lini nitapata ujasiri wa kutoboa kidole.
 
Ndugu yangu mzabzab ndiye pekee amekiri wazi, anastahili tuzo huyu mwamba. Sie wengine zaidi ya porojo hatuna la kuongeza 😅😅😅 japo mimi status yangu kweli siijui, sijui lini nitapata ujasiri wa kutoboa kidole.
Ah wee unapima ya nini kujitakia stress thu. Tulia zako ipo siku isoyojulikana utapata kujua status yako.
 
Sasa niukwae mara ngapi jamani sixteen years and counting hamna arv wala nini siri ni mazoezi chakula na kitokuoa maana ukiwa na mke unaongeza uharaka wa kulifikia kaburi lako 🤣🤣🤣🤣 oh plus maji kwa wingi pia
Itafikia mahali dawa haitazuilika.... Hlf nyie msiotumia dawa ndiyo mnaoendeleza kusambaa kwa maambukizi
 
nimesoma thread hii comment moja hadi nyingine, nimejikuta napata kiwewe sana cos umegusa familia yangu kwa kiasi kikubwa
1999 nilimpoteza mjomba alikuwa handsome aise mimi nilikuwa mdogo ila nilikuwa natamani niwe handsome kama uncle alikuwa deleva wa askofu huko njombe, alio mke wa kwanza akafariki bila yakupata mtoto akaoa mke wapili wakapata watoto 2 (ke na me)
Mjomba alikuwa kiwembe akamwambukiza mke, mtoto wa kwanza negative mtoo wapili ikasoma postive

Akafariki yeye 1999 akafata mke 2001 na wa mwisho akafata mtoto 2007, mjomba angu mwingine nae aliumwa TB akapona 1999 hadi 2001 akapona kabisa na hakuwa na UKIMWI sijui nini kika mkumba 2008 akaenda kuoa mtu ana UKIMWI baada ya muda tukampoteza tena alikuwa anajua kabisa ila tamaa zilimzidia cos mwanamke alikuwa cheap na huyu mjomba alikaa miaka 10 kwa maelezo yake yeye bila kugusa mama alimchukua apozee tu kupima + akaamua kuoa kabisa

Hadi mimi mwenyewe nilijihisi ninao cos wazazi wangu wote wamefariki na mimi ni last born baada ya kufuatilia sana kilichowaua wazazi wangu nikagundua ni TB sio UKIMWI kwenda kupima nikajikuta nipo fresh
Nilikuwa naogopa UKIMWI sana na sikuwahi kusa Ke hadi nilipo oa na Mungu mwema saivi ni baba wa watoto watatu na wana afya njema kabisa
 
😳😳😳🤔 Leo hii?
ceet.PNG
 
imagine upo unajipima magetoni halafu shaaaaaaaa mistari miwili,

yaaaan twaaa mistari miwili

yaaani taaaa mistari miwili

unajaribu kipimo kingine mara chaaaaa mistari miwili

unachanganyikiwa unaanza kupiga kelele ghafla unasikia wife anakwambia "MUME WANGU KARIBU CHAKULA"
Ni hatari...! Nasoma comments watu wanaandika utoto...eti ukimwi Ni ugonjwa wa kawaida nawashangaa Sana..
Kuna mtu namjua ana ukimwi lakini mke hana ukimwi..na wanaishi nyumba moja..wana watoto..sijui wanaishijeishije..na Mimi siku za mbele nitaeleza kisa chao..(Ni story ya huzuni maana huyu jamaa alitembea na mtoto wa mbunge akiwa Ni mlinzi wao..alimuambuza ili gonjwa binti innocent kaibisa)
 
Back
Top Bottom