Siungi mkono watu Kumchukia Diamond kisa aliipigia kampeni CCM

Kuhamasishana ili watu wasimpgie kura mtu kutokana na itikadi yake ya kisiasa huo ni uadui. Hauna tofauti na magu alivyokuwa anawaweka ndani wapinzani. Na huenda kama wangekuwa na madaraka nao wangefanya kama magu
Siasa sio uadui, kuwa na itikadi tofauti sio uadui, ila siasa ikitumika vibaya kama alivyokuwa anaitumia Magufuli ndio uadui.
 
Wako huru kumsapoti yeyote kama wewe ulivyo huru kumsapoti diamond, halafu kama ni wanaharakati wa kisiasa wako sahihi kwanini unataka wamsapoti aliyeungana na watesi wao CCM kuwateka, kuwaua, kuwanyanyasa na kuwabeza kwa nyimbo zake?
Ukweli mchungu huu. Wakae kwa kutulia.
 
Acha upuuzi ,Domo hata akipigiwa kura na waTZ hawezi kutoboa mbele ya wanaijeria,msitafute kichaka cha kujifichia.

Pili atakula alipopeleka mboga ,mwambieni pole pole na shaka zulu wahamasishe wana ccm wampigie kura.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukienda na matusi yako anakublock nenda kwa hoja.
Hakuna matusi wala nini, ukimpinga kwa hoja anaanza kutafuta maisha yako binafsi ili kukudharirisha, akikukosa anakublock, yule ni kichaa
 
Hata chadema wasipompigia domo hawezi kushinda.

Hao chadema kama kweli wana nguvu ya kumpandisha msanii waanze kumpandisha sugu,roma na wengineo wanaowasapoti..


Msanii yupi anayesapoti chadema ana trend? Siasa za wapinzani ni za ovyo
 

Apelekae mboga alikopeleka ni sahihi kukumbushwa kwa vitendo wapi akaendelee kula. Hilo haliwezi kuwa na mjadala.

Habari ndiyo hiyo.
 
Kwani huyo domokaya ana haha nini? Si juzi tu kakutana na Shaka Pandu si angemuambia awahimize wafuasi wa ccm wampigie kura? Ndo atajua hajui sasa, ba atakula alikopeleka mboga.

Nwei hawezi kushinda mbele ya Burna boy na Wizkidayo. Poleeh yake sana, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hakuna matusi wala nini, ukimpinga kwa hoja anaanza kutafuta maisha yako binafsi ili kukudharirisha, akikukosa anakublock, yule ni kichaa
Comment yako tu hii inakuonyesha ulivyo mtu wa matusi.
 
Sisi tumeamua tunampigia burns boy

Tusipangiane aisee[emoji57]
 
Kwani nani amekutaka kuunga mkono, kila mmoja ashinde match zake
 
Ukitazama hii movement imekaa ki HUSDA na sio kiweledi na siasa inatumika kama mlango wa kupitishia husda hizo kumpigia mtu kura ni hiyari lakini inapotumika nguvu kubwa kuhalalisha hilo inazua maswali mengi kwenye jamii......inawezekana wanaofanya hayo wana ajenda zao nyuma ya pazia.

Muda utatuambia.
 
Comment yako tu hii inakuonyesha ulivyo mtu wa matusi.
Hivi wewe Kuna mtu mwenye maneno machafu kama Kigogo? badala ya kupambana na Nick wa pili analeta Habari za mkewe za nini? yule ni kichaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…