Siungi mkono watu Kumchukia Diamond kisa aliipigia kampeni CCM

Na mimi wa 26 mkuu[emoji23][emoji23] na naenda kuwa balozi kuongeza chain. Ni bana boi tuu hakuna mwingine
 
Mimi Sina tatizo na watu kutompigia kura Diamond huo ni Uhuru wao, ambacho mimi napinga ni kujaribu kumshutumu Diamond kwa kuwa tu ni ccm, wakati kuwa ccm sio kosa, ni jambo la uchaguzi binafsi, kama Simba au Yanga
 
Ebu tuambie Diamond hajakemea, haya Nani kakemea hapa Bongo kwenye jambo lolote linalo lalamikiwa na upinzani
Ishu sio kukemea ni bora angekaa kimya tu!... sasa ilifikia kipindi watu wanalalamika kuhusu uonevu wa serikali yeye anatunga wimbo kuitetea serikali! Hiyo haikuwa sawa na sa iv ndio analipa price yake asilalamike.
 
Heeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee kwani mwanamziki anaeitaka brand yake alikuwa na ulazima gani wa kuhangaika na kampeni? viva Joh Makini huu upuuzi huwa huutaki.

kura kwa Burn Boy anatosha
Kila la kheri, ila kampeni kama kawaida
 
Mungu mkubwa mnaweza shangaa mondi akashinda, sema watanzania ni watu wa ajabu simba ikicheza ta tamu za nje ikifungwa mashabiki wa yanga wanafurahi, saizi mondi akishindwa mashabiki wa kondeboy watafurahi huwa hatuaangalia utaifa wetu kwanza
 
Tena hao BET ingependeza wangeweka na option ya kupiga kura za dislikes

Hapo ndio angepata jibu la moja kwa moja ni kiasi gani watu tuko siriasi.
 
Tena hao BET ingependeza wangeweka na option ya kupiga kura za dislikes

Hapo ndio angepata jibu la moja kwa moja ni kiasi gani watu tuko siriasi.
Serious kwa kelele za mitandaoni, yaani lile vibe la Lissu utafikiri atakuwa rais, matokeo yake kaambulia kura milioni 1, nyie kelele zenu kama Nzi
 
Kuhamasishana ili watu wasimpgie kura mtu kutokana na itikadi yake ya kisiasa huo ni uadui. Hauna tofauti na magu alivyokuwa anawaweka ndani wapinzani. Na huenda kama wangekuwa na madaraka nao wangefanya kama magu
Chief naona umesahau makonda alivoenda kuvamia studio za clouds na watu wengi kulaani lile tukio, diamond akalikoroga kwa kutoa nyimbo kumtetea makonda licha ya kuonekana wazi alichofanya ni makosa...mi binafsi tatizo na diamond lilianzia hapa! Licha ya hilo pia kipindi serikali ya magufuli uko kwenye pick ya kuwafanyia watu ukatili akatoe nyimbo nyingine kumsifu magufuli, sasa kwa situation km hii unaanza vipi kuwalaumu watu walionyanyasika kipindi cha utawala wa magu kutomsapoti diamond?
 
Mkuu mbona Ata Konde boy alitoa nyimbo tamuu ya kumsifia Magufuli, vile vile amechora tattoo ya Magufuli mguu, vile vile alilia Instagram live, au mna muacha kwanza mpaka apate nomination BET ndio hasira zenu zinakuja?
 
Serious kwa kelele za mitandaoni, yaani lile vibe la Lissu utafikiri atakuwa rais, matokeo yake kaambulia kura milioni 1, nyie kelele zenu kama Nzi
We unafikiri BET ni sawa na NEC ya mahera ambayo inafata meza yenye bia nyingi ya kumlamba boss miguu?
 
Uislamu unanasibishwa na ugaidi dunia nzima...je inafaa kuwaita waumini wote kuwa ni magaidi kwa kuwa wamechagua kuwa waislamu........??
Tatizo lilianzia kwenye wimbo 'acha nikae kimya' na likaishia kwenye wimbo 'magufuli baba lao' hakuna haja ya kupigizana kelele kila mtu akale alipopeleka mboga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…