kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Magufuli hakukosea kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya chadema kwa sababu haikua na tija ila kuleta vurugu tu. Ilikua fujo tu kupinga kila kitu hadi serikali ilioko madarakani wanapata shida kutekeleza ilani yao.Kwa kweli sielewi kabisa misimamo ya wana-ccm, wakati ule mara tu alipoingia madarakani mwaka 2016, Rais wa wakati huo, Hayati Magufuli, alipopiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, huku akijua wazi kuwa anaisigina Katiba ya nchi, walijitokeza wana-ccm kibao, waliopongeza hatua hiyo na kuiita ya kishujaa na kuvisihi vyama vya upinzani, vikachape kazi, Kwa kuwa muda wa kufanya siasa ulikuwa umekwisha!
Nimeshangazwa pia safari hii, wakati Rais wa awamu ya 6, Samia Suluhu Hassan, alipoiruhusu mikutano hiyo na akaeleza wazi kuwa ni ukiukwaji wa Katiba kuipiga marufuku mikutano hiyo, Kwa kuwa ni haki yao kikatiba, vyama hivyo kuifanya mikutano hiyo na wao kama Serikali, Kwa kutumia Jeshi lake la Polisi, wajibu wao mkubwa, ni kuilinda mikutano hiyo, Ili ifanyike Kwa njia ya amani na utulivu.
Nimeshangazwa pia kuwaona wana-ccm wale wale, wakitoa pongezi nyingi Kwa Rais Samia na kusema kuwa huyu mama ni mwana-demokrasia, Kwa hiyo anapaswa kupewa pongezi nyingi Sana!😎
Ndipo hapo ninapojiuliza hivi Hawa wana-ccm wanajielewwa kweli?
Ni kwanini wakati ule Mwenyekiti wao wa CCM, ambaye pia alikuwa ndiye Rais wa nchi, alipopiga marufuku mikutano hiyo, hawakuweza kumuhoji kuwa kitendo anachofanya, ni Cha kukiuka waziwazi Sheria za vyama vya kisiasa vya upinzani, ambao wamepewa haki hiyo kstika Sheria za vyama vya kisiasa nchini?
Tabia hii ya ukinyonga na unafiki inayofanywa na viongozi wa CCM, ambao wanashindwa kuwa na msimamo mmoja, ndiyo inayoweza kuliangamiza Taifa letu!
Mungu ibariki Tanzania
Jpm alisema na kwa usahihi siasa baada ya uchaguzi zihamie bungeni na kwenye mabaraza ya madiwani.
Sasa hivi chadema wameishilia kutokana na itikadi na sera yao isiyofaa kwa wananchi. Hata wakifanya mikutano ya hadhara itawalazimu kufuata utaratibu na kuacha uchochezi. Hayo ndio masharti yametolewa kwa wapinzani.