Siwezi kuandamana hata siku Moja ni ujinga

Tusameheni watoto na wajukuu zetu. Tumewaangusha sana. Wenzenu huko USA,UK,UAE,China etc wamekuta nchi imejengwa na wazee wao. Lakini sisi tumewaachia uozo mtupu, yaani tulikuwa tunashindana kuiba mali na rasilimali za taifa. Lakini mwisho wa siku msipochukua hatua nyinyi ndio mtateseka sana sisi tumebakisha muda mfupi sana hapa duniani halafu tushajilimbikizia mali za wizi za kutosha. Tusameheni vijana wetu. KOMBOENI NCHI YENU THE FUTURE LOOKS BLEAK.
 
Utaandamana wewe Sina huo ujinga mimi
Wanaoandamana siyo wajinga tumia lugha nzuri! Watakaposikilizwa au shinikizo lao litakapokuwa na nguvu serikali ikatekeleza kutenda mema utasimama Kifua na mstari wa mbele kufurahia. Swala ni katiba inasemaje? Waandamanaji wanafikisha ujumbe bila vurugu? Waliopelekewa ujumbe wanachukia hatua gani? Watawala wengi Wana dharau sana Kwa sababu ya kulindwa na dola zao. Hatimaye watu wanakasirika.
 
Umeongea kitu cha dhahabu!
Watz tunaonekana ni wazembe hatupendi kufanya kazi ndio maana tunalia njaa lakini sio kweli!
Kwa mfumo tulionao hata mtu anayepambana kwa nguvu zake zote hawezi kupata return sawasawa na nguvu zake
Ndio maana matajiri wetu wengi ukichunguza wana kitu fishy wanafanya chini ya kapeti.
 
Siwezi kufanya huo ujinga acha tuteseke Kila mtu na kaburi lake
 
Ni wajinga tu yaani unaandamana unakufa unazikwa unaoza halafu wenzio wanakula keki ya taifa mda huo wewe umeshakua mchanga kama unabisha sio ujinga mfano waliokufa kwenye maandamano Kenya wafufuliwe halafu waulizwe ni ujinga au ujanja amini nakuambia watasema walikua wajinga sana
 
SIKU WAKIKUBAKA UKAKOSA HAKI YAKO UTUJULISHE
 
Unaandamana ili mbowe na lisu wakakae kwenye kiyoyozi na apewe maximum security kama Rais watoto wao waishi vizuri alafu we uendelee kula dagaa na ugali kama ngumi
 
Kila mtu huwa ana play part yake, wewe huenda ukatumia njia nyingine tofauti na kuandamana, lakini mwingine akaandamana na wote mkatangeneza kitu kikubwa katika nchi au jamii kwa ujumla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…