Siwezi kulea Mtoto ambae Wazazi wake wako hai na afya zao

Siwezi kulea Mtoto ambae Wazazi wake wako hai na afya zao

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
12,312
Reaction score
18,194
Utakuta mtu anakuletea mtoto wake ati ukae nae yeye kamshindwa tabia, sasa umemshindwa wewe uliyemzaa nitamuweza mimi ambaye sijui uchungu wa huyu mwana?

Ati anakuletea ukae naye kisa maisha magumu hivyo msaidie kulea, kwani akikaa huko huko na wewe mzazi wake alafu mimi nikawa namsaidia akiwa hapo kwenu kuna tatizo gani wakati msaada ndo ule ule?

Sikatazi watoto waje kunitembelea hapana, ila kuja moja kwa moja kukaa na kuwalea lazima kuwa na masharti ya kutosha tu.

Dunia ya sasa huwezi kukaa na mtoto wa mtu wakati wazazi wake wanatanua tu au wanasingizia maisha magumu.

Kaa na umlee mwanao kama maisha magumu na yeye ayaone ili baadae akitoboa awakumbuke wazazi namna mlivyoishi kwa tabu.

Mtoto analelewa na mjomba wake anayejiweza akija kuwa mkubwa haoni uchungu wa wazazi wala hakumbuki mambo ya njaa kwa sababu wakati wazazi mna njaa hamkuwahi kukaa nae pamoja.

Ni hayo tu.
 
fanya kile kitu roho inapenda ila kuna wengine wana shida kweli!
Msaidie mtoto akiwa kwao na wazazi wake.

Kama ishu ni kusaidia basi unaweza kumsaidia hata akiwa kwao.

Sasa hivi watu wanachofanya ni kusaidiana kulea huku wakidhani wanasaidia au kusaidiwa mahitaji ama huduma.

Utakuta mtoto hana malezi ya wazazi wake kabisa.
 
Kuna rafk angu yeye anasema kuna mtoto wa shemeji yake anataka kuletewa alafu huyo mwenye mtoto anatamba mjini anakula vizuri tu na life linaenda lakini kwa kigezo ati mtoto hana adabu hivyo anambadilisha mazingira.

Si ujinga huu
Hana adabu aliye mfundisha kutokuwa na adabu si yeye kwahyo anataka ampeleke KWA jamaa Ili akawaambukize na watoto wa jamaa kutokuwa na adabu sometimes sisi watu weusi tunashndwa kupata maendeleo KWA kujibebesha mzigo isiyotuhusu,. Mimi Kama namsaidia mtoto wa mtu mpaka niione kwel haina namna ama wazazi wake wamefariki
 
 
Back
Top Bottom