Kwa mimi niliyelelewa na wasiokuwa wazazi wangu, ingawa wazazi walikuwa hai(bado wapo hai). Nitalea nikipata hiyo nafasi ya kulea.
Nimejifunza mengi sana mazuri na mabaya kukulia mikononi mwa walezi, hilo ni somo tosha sina budi kuliishi nikipata hiyo nafasi!
Hapa naona unafanana na mimi mkuu.Mimi wazazi wangu walikuwa na uwezo tena sana ila nimelelewa na familia isiyo na uwezo kabisa kwa mapenzi ya wazazi wangu na wao sijui walitendeana mema kiasi gani siku za nyuma ila na mimi nilikuwa na mapenzi ya dhati kabisa na familia iliyokuwa inanilea.
Ajabu sasa wazazi wangu walifariki miaka20 iliyopita kwa utu uzima ajabu sasa hii familia iliyonilea ndio mimi ni kama mtoto wao wa damu kabisa katika familia hii naweza kusema mimi ndio niko vizuri kidogo kielimu na kikipato kuliko watoto wao kwa kweli nina mapenzi nao kabisa mimi ni mtoto wao wa damu na tuko pamoja.
Hii familia hawakujaliwa mtoto wa kiume mimi ndio kaka yao wa kiume wakipekee na bahati mbaya baba aliyenilea naye akaja kutangulia mbele mimi ndio msimamizi wa kila kitu cha mirathi na mali japo za kawaida kwenye hii familia.
Nimeona nitoe kisa hiki nikiwa na maana kila jambo mungu anapopanga anakuwa na makusudi yake maaluma ambaye kwa binadamu wa kawaida hawezi kujua fumbo la mbele.
Kisa flani huyu Jef Bezos tajiri namba moja wa dunia mama yake aliolewa na baba mmoja alikuwa mlevi kupindukia ambaye ndio alikuwa baba yake Jef sasa.Ilifikia hatua yule mama akapewa talaka na yule mlevi mlevi akamuambia ondoka na takataka yako yaani yule mwanawe wa kiume yaani Jef.
Yule mama baadae akaja pata bwana mwingine akamuoa akampenda yule mama na mtoto wake.Akamuasili kisheria kuwa mwanae kabisa ikabidi aasili na jina la ubin wake mtoto akaitwa Jef Bezos.
Baada ya miaka kadhaa huyu mtoto akaja kuwa tajiri sana wa dunia siku moja kuna mwana historia alitaka kuandika historia ya Jef Bezos akagundua baba yake bado yupo akamfuata.Akamuuliza unamkumbuka kuna mama ulimuacha na mtoto wa kiume yule mlevi akasema hivi yule kijana bado yuko hai?
Yule muandishi akamuambia umeshawahi sikia tajiri wa dunia anaitwa Bezos akasema ndio akamuambia basi ndio yule mwanao uliyemkataa kwa sasa anaitwa Jef Bezos.Yule mzee aliumia sana akawa anamuandikia barua nyingi mwanaye kumlilia shida mbali mbali na kumtambulisha kuwa yeye baba yake bado yupo hai Jef Bezos hajawahi kabisa kumjibu huyo baba yake akaja kufariki kwa kihoro sana.
Siandiki haya kushabikia kulea watoto wasio na mpango ambao mtu unatupitwa mzigo wakati wazazi wao bado wapo wanatanua tu ila nia yangu ni kusema tu kila kitu mungu ana mpango wake.
Wako watoto ambao unawalea kutokana na kuwa ni yatima baba yao na mama amefariki.Na pia wako watoto ambao ni wa ndugu yako unawalea sababu either wazazi wao hawana uwezo kabisa ni mafukara wa kupindukia au wazazi wote ndio wamezaa lakini mmoja wa wazazi au wote wamepatwa na ugonjwa wa akili.
Pia ukifuata msemo unasema ukipenda boga penda na ua lake unaweza lea mtoto wa mke uliyempenda sana ila akaja na mwanaye. Natoa mifano ya watoto walioasiliwa na kusomeshwa na familia ambazo sio zao
Jef Bezos-tajiri namba moja wa Marekani
Steve Job-mwanzilishi tajiri wa Apple alikuwa mtoto aliyeasiliwa
Eleanor Roosevelt-Alikuja kuwa first lady wa raisi wa marekani.Na alikuja kuwa mjumbe kwenye baraza umoja wa mataifa
Nelson Mandela-baba yake alifariki akiwa na miaka9 tu akarithiwa na chief wa kabila lake ndio aliyemsomesha.
Nancy Reagan-alikuja kuwa first lady wa Marekani.
Bill Clinton-alikuja kuwa raisi wa marekani