Siwezi kulea Mtoto ambae Wazazi wake wako hai na afya zao

Kwa mimi niliyelelewa na wasiokuwa wazazi wangu, ingawa wazazi walikuwa hai(bado wapo hai). Nitalea nikipata hiyo nafasi ya kulea.

Nimejifunza mengi sana mazuri na mabaya kukulia mikononi mwa walezi, hilo ni somo tosha sina budi kuliishi nikipata hiyo nafasi!
 
Bao apige mwingine alafu niteseke mimi? Hiyo haipo..
Nisipolisema Hili Hapa Morogoro Halafu Nikaondoka Nitakuwa Ni Mnafki.
Nasema Uongo Ndugu Zangu
😀😁😂🤣😃😄😅😄🤣😂😁😀
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Umeletewa Jiko hulitaki mkuu
 
Hapa naona unafanana na mimi mkuu.Mimi wazazi wangu walikuwa na uwezo tena sana ila nimelelewa na familia isiyo na uwezo kabisa kwa mapenzi ya wazazi wangu na wao sijui walitendeana mema kiasi gani siku za nyuma ila na mimi nilikuwa na mapenzi ya dhati kabisa na familia iliyokuwa inanilea.
Ajabu sasa wazazi wangu walifariki miaka20 iliyopita kwa utu uzima ajabu sasa hii familia iliyonilea ndio mimi ni kama mtoto wao wa damu kabisa katika familia hii naweza kusema mimi ndio niko vizuri kidogo kielimu na kikipato kuliko watoto wao kwa kweli nina mapenzi nao kabisa mimi ni mtoto wao wa damu na tuko pamoja.
Hii familia hawakujaliwa mtoto wa kiume mimi ndio kaka yao wa kiume wakipekee na bahati mbaya baba aliyenilea naye akaja kutangulia mbele mimi ndio msimamizi wa kila kitu cha mirathi na mali japo za kawaida kwenye hii familia.
Nimeona nitoe kisa hiki nikiwa na maana kila jambo mungu anapopanga anakuwa na makusudi yake maaluma ambaye kwa binadamu wa kawaida hawezi kujua fumbo la mbele.
Kisa flani huyu Jef Bezos tajiri namba moja wa dunia mama yake aliolewa na baba mmoja alikuwa mlevi kupindukia ambaye ndio alikuwa baba yake Jef sasa.Ilifikia hatua yule mama akapewa talaka na yule mlevi mlevi akamuambia ondoka na takataka yako yaani yule mwanawe wa kiume yaani Jef.
Yule mama baadae akaja pata bwana mwingine akamuoa akampenda yule mama na mtoto wake.Akamuasili kisheria kuwa mwanae kabisa ikabidi aasili na jina la ubin wake mtoto akaitwa Jef Bezos.
Baada ya miaka kadhaa huyu mtoto akaja kuwa tajiri sana wa dunia siku moja kuna mwana historia alitaka kuandika historia ya Jef Bezos akagundua baba yake bado yupo akamfuata.Akamuuliza unamkumbuka kuna mama ulimuacha na mtoto wa kiume yule mlevi akasema hivi yule kijana bado yuko hai?
Yule muandishi akamuambia umeshawahi sikia tajiri wa dunia anaitwa Bezos akasema ndio akamuambia basi ndio yule mwanao uliyemkataa kwa sasa anaitwa Jef Bezos.Yule mzee aliumia sana akawa anamuandikia barua nyingi mwanaye kumlilia shida mbali mbali na kumtambulisha kuwa yeye baba yake bado yupo hai Jef Bezos hajawahi kabisa kumjibu huyo baba yake akaja kufariki kwa kihoro sana.
Siandiki haya kushabikia kulea watoto wasio na mpango ambao mtu unatupitwa mzigo wakati wazazi wao bado wapo wanatanua tu ila nia yangu ni kusema tu kila kitu mungu ana mpango wake.
Wako watoto ambao unawalea kutokana na kuwa ni yatima baba yao na mama amefariki.Na pia wako watoto ambao ni wa ndugu yako unawalea sababu either wazazi wao hawana uwezo kabisa ni mafukara wa kupindukia au wazazi wote ndio wamezaa lakini mmoja wa wazazi au wote wamepatwa na ugonjwa wa akili.
Pia ukifuata msemo unasema ukipenda boga penda na ua lake unaweza lea mtoto wa mke uliyempenda sana ila akaja na mwanaye. Natoa mifano ya watoto walioasiliwa na kusomeshwa na familia ambazo sio zao
Jef Bezos-tajiri namba moja wa Marekani
Steve Job-mwanzilishi tajiri wa Apple alikuwa mtoto aliyeasiliwa
Eleanor Roosevelt-Alikuja kuwa first lady wa raisi wa marekani.Na alikuja kuwa mjumbe kwenye baraza umoja wa mataifa
Nelson Mandela-baba yake alifariki akiwa na miaka9 tu akarithiwa na chief wa kabila lake ndio aliyemsomesha.
Nancy Reagan-alikuja kuwa first lady wa Marekani.
Bill Clinton-alikuja kuwa raisi wa marekani
 
Ahsante mkuu kwa kutilia mkazo hili jambo
 
Acha kulea mtoto wa mtu ambaye wazazi wake wapo hai. Mimi sintolea hata mtoto wa Dada ama kaka yangu au eti mtoto sijui wa Shangazi waje kusomea kwangu. Nitapambana na famili ambao ni watoto wangu. Huu ndio msimamo wangu wa kutokaa na single Mama.
 
Hujafa hujaumbika mkuu omba mungu sana hivyo vijisenti usijione umefika kuna Leo na kesho acha roho mbaya
Kuna wakati nilisaidia mtoto Kwenye familia ya watoto 4, nikawa namnunulia mahitaji ya shule yote. Baadae mama Yake akasema niwe Nampa hela anunue yeye kumbe aliona watoto wake wengine wanaanza kumchukia mdogo wao kwanini ananunuliwa yeye tu.
Dawa ni kumchukia umsaidie akiwa kwako Kama unaweza.
 
Jana tu mtoto wa shemeji yangu kafika mjini bila taarifa,nakuta dogo yupo na hapohapo anasema begi na vitu vyake vyote kaporwa alivyoshuka Stendi.Wazazi wake wote wawili wapo na wanna nguvu zote.
 
Mliokuwa mnauliza baadhi ya ngozi nyeupe kuweza kuishi extended family huku sisi ngozi nyeusi tukishindwa

Majibu yapo kwenye comments
 
Tatizo linaletwa na masingo maza, watoto wale hawana pa kwenda maana mamayao tu na yeye analelewa.
 
Sijui ni kitabu gani nilisoma kuna hii quote "life is a learning process" mleta mada sikulaumu bado hujapitia baadhi ya life process.
Kuna watoto wamezaliwa na wazazi wenye fedha, uwezo, status kuliko wewe lakini mtoto yupo kwenye mazingira hatarishi na mateso makali, baba au mama au wote ni "hell", njia pekee ya kumuokoa ni kumtoa huyu mtoto kwa wazazi/mzazi wake aishi na mtu mwingine. Unafikiri watoto wanaoishi na babu/bibi zao wanaishi kwa kupenda au wazazi wao hawana uwezo? au wanaoishi kwenye vituo vya kulelea yatima na watoto wa mitaani hawana wazazi wenye uwezo?
Kuna tabia za wazazi wanaowabaka na kuwanajisi watoto wao wa kuzaa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…