Siwezi kulea Mtoto ambae Wazazi wake wako hai na afya zao

Kwa kesi kama hizo nakubali.

Ninachozungumzia ni mzazi kumgawa mtoto kwa kesi ya kuwa ati maisha magumu.

Na kesi ya kuwa mtoto kashindikana.

Hizi kesi ndo zipo mtaani ndizo ambazo nimegusia kwenye uzi wangu lichs ya kuwa bandiko liko katika ujumla.
 
Kuna wazaz haswaa wababa si salama kwa watoto zao..
 
Aisee.😀😀,inaonekana mleta mada kaletewa watoto wandugu awalee.sasa kashindwa kukataa so kaamua hasira zake aje kuzimalizia JF😀,

au nasema uwongo jamani!
 
Yapo makabila ambayo yanatabia ya kushadidia sana extended family bila aibu lakini ukiangalia kiundani ni shauri ya kukosa elimu na umasikini.Unakuta baba na mama ameshajua tu mtoto amepata kazi yuko mjini baba na mama wanasafiri kwenda kwa mtoto na wanao uwezo wanalima kijijini sio watu wa kufa njaa.
Ukweli unabaki pale pale extended family inarudisha nyuma maendeleo ila kuna situation flani inabidi uwe nayo mfano mtoto wazazi wake wote wamefariki labda kwa ajali mtoto yuko std1 je utasema hukai na mtoto wa hivyo?.Unakuta mtoto amezaliwa mama yake ana ugonjwa wa akili na baba yake hajulikani na huyo mtoto ni wa dada yako utaacha kumsaidia au kukaa naye kisa hupendi extended family?.Sisi waafrica wengi in one way or another tumeshaishi ki extended family hatujafikia hatua ya wazungu.Mfano hata ukiwa unasoma secondary mikoa ya mbali ni baba yako anakusomesha lakini likizo za midterm zote huwezi toka Songea hadi Bukoba wakati una baba yako mdogo yuko Songea utakaa ile wiki itaishi ni short lived tu lakini kwa kile kipindi kifupi utakuwa ume disturb system za watu.
This is Africa.Huwezi mpeleka mama yako na baba yako nyumba ya kulea wazee kisa wewe unaishi maisha ya matawi ya juu wakati walikuhangaikia ukafika ulipo.Kila race wana culture yao tusijifanye kuiga ya wazungu kwanza wenzetu wazee wanapewa allowance na serikali hadi mwisho wa maisha yao ukileta hayo Africa haiwezi ku work out.
Mandela asingechukuliwa na chief wa kabila lao baada ya baba yake kufariki akiwa na miaka9 tu mwaka1927 tusingekuwa na kiongozi maarufu duniani.Mtoa mada pengine watu watafikiria umetoa mada una ubinafsi umeongea ukweli ila na wewe nikuulize je toka uzaliwe hujawahi wakati unasoma hata likizo ukaenda kwa mjomba au ndugu yako?.Tayari hiyo ni extended family hata kama ni muda mfupi watu weupe wao hawana kitu nakwenda kwa dada kwanza ukifika tu unaulizwa utaondoka lini je una mpango wa kula mchana ukisema ndio siku hiyo inakuwa zamu yako kupika na kuosha viombo.Hii niliiona wingereza jiji la Bath county ya Somerset nilikwenda kama family friend kutembelea family flani nikakuta hayo ila nilishaambiwa mapema kabisa ila nilichoshangaa hata mnyama paka ni part of family na ana sahani yake unaosha pamoja na sahani zingine hiyo ni kazi ya mgeni siku ya kwanza.
Narudia tena in everything GOD HAS SOME REASONS Yusuf aliishi misri utumwani kwa kulelewa na Farao lakini akaja kuwa mkombozi wa watu wa taifa lake.
EXTENDED FAMILY IS NUISANCE IF THERE IS NO SUBSTANTIAL REASON TO HAVE IT
 
Wenzio wazungu wanatamani extended Family!
Mnashirikiana Umaskinj na Utajiri pamoja kama Familia!
[emoji116][emoji116]
RUM. 12:15 furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.
 
Wazazi wangu wote wako hai. Nimelelewa na mjomba wangu na alihakikisha napata elimu nzuri na nimekua baraka sana kwake na kwa ukoo wetu mzima.

Wakati mwingine its not about the parents, bali huyo mtoto. Kama unaweza kurescue future yake kwa faida yake ni bora kuliko kumuacha na kuendeleza chain ya umasikini.
 
Kuwa na ukwasi au kuishi maisha ya luxury wewe ishi tu huko mbeleni Lakin kulea mtoto wa mtu ni kazi kubwa sana

Sent from my F3111 using JamiiForums mobile app
 
Kama umetaka mwenyewe kulea watoto wa wengine hakuna tatizo.

Lakini suala la mtu snakuja kukuambia kuwa umlee mwanae kisa anatabia mbovu mtoto ama eti kuna huduma fulani haziipati hilo naon halijakaa sawa.

Msaada atasaidiwa akiwa kwao tu
 
Kuna watu nadhani aidha ni utindio wa ubongo, au walizaliwa na sehemu za akili zikiwa damaged.

Unapata mtoto kwa hiyari yako mwenyewe then ghafla bin vuuu unamletea mtu majukumu yako, it doesn't make any sense. Huwa nashangaa sana.
 
Kama una shida si inabidi upewe msaada, sasa kwenda kumbwagia mtu watoto wakati mzazi/ wazazi mpo hai mnakula bata na kutanua tu si sawa
 
Wanavyozaana wanasemaga tuzae tu kila mtoto uja na rizki yake alafu wakiwashindwa wanawapa mizigo ndugu zao, kila mtu aubebe mzigo wake.
 
Shida ni familia yenu mmelelewa vipi mzee. Kama hukufundishwa upendo na wazazi wako lazma uone mzigo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…