Siyatambui mapinduzi Guinea, Rais Conde namtambua kama Rais bado waliomteka nyara wamrudishe upesi

Siyatambui mapinduzi Guinea, Rais Conde namtambua kama Rais bado waliomteka nyara wamrudishe upesi

Kwa siku moja tu !!. Lazima mazingira ya kuirudisha serikali kwa raia yaandaliwe . Ikiwemo na hilo Bunge lililofanya mambo haramu lazima liondolewe .
Wangetaka kuachia madaraka tungeona hata dalili wakitamka wana lengo la kuitisha uchaguzi ndani ya muda fulani. Historia ya mapinduzi mengi yanayofanyika Afrika wanajeshi huwa hawatoki kwahiyo raia mnakuwa mmeondoa tatizo mmeingiza tatizo na wanajeshi huwa hawana uwezo wa kuongoza nchi.
 
Bunge la Guinea kwa Vikao vyake halali kabisa lilijiongezea posho na kupitisha kuwa Raisi aliyepo Raisi aliyepo ruksa kugombea tena

Kikosi kimoja cha makomandoo bila kushirikisha vikosi vingine vya jeshi wakaenda kumteka Raisi Condé na kumficha wanakojua wao.

Mimi bado namtambua Rais Conde kama Rais halali wa Guinea na nautaka umoja wa Afrika usimtambue huyo jambazi Mamady Doumbouya na Kikosi chake cha majambazi makomandoo waliomteka Rais halali na kujitia eti wamempindua.

Vikosi vingine nendeni mkalipindue hilo jangili. Mamady Doumbouya arudishwe Rais Conde

Naitaka jumuiya ya kimataifa ilaani huo utekaji nyara na hilo Jambazi linalojiita limepindua liuawe chap chap

Kwa mujibu wa katiba ya Guinea hakuna njia ya Jeshi ya kumuondoa Raisi aliyepo madarakani. Jambazi Mamady Doumbouya kavunja katiba
Hicho ndicho mtachofanyiwa maccm
 
Kwa siku moja tu !!. Lazima mazingira ya kuirudisha serikali kwa raia yaandaliwe . Ikiwemo na hilo Bunge lililofanya mambo haramu lazima liondolewe .
Inategemea na mpinduaji ana malengo yapi . Tumemshuhudia Jerry Rawlings akiifanya Ghana kuwa democratic country in Africa .

Kuna wale wenye tamaa sawa na hao wanaowaondoa madarakakani. Tulimshuhudia colonel Muamar Gaddafi akimpindua mfalme Idris na baadaye naye kung'ang'ania madarakani . So it depends . Ni sawa na Asp/Ccm ilifanya mapinduzi na leo wameng'ang'ania madarakani hata pale wanaposhindwa uchaguzi dhahiri .
 
Wangetaka kuachia madaraka tungeona hata dalili wakitamka wana lengo la kuitisha uchaguzi ndani ya muda fulani. Historia ya mapinduzi mengi yanayofanyika Afrika wanajeshi huwa hawatoki kwahiyo raia mnakuwa mmeondoa tatizo mmeingiza tatizo na wanajeshi huwa hawana uwezo wa kuongoza nchi.
Hawa ccm walioshindwa kuendesha nchi hapa nao ni wanajeshi.
 
Nchi hii mtu akishakuwa mwanachama wa ccm anajiona ANATAWALA ULIMWENGU MZIMA mtu mjumbe wa mkutano mkuu was kata wa ccm unatoa tamko la kuishurutisha nchi nyingine

Vituko Kama hivi utavikuta kwa wanachama wa CCM TU

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
YEHODAYA unaweza ukawa nani kwenye hii safu ya majambazi ccm?. Naona mapinduzi ya wananchi wa Guinea yamekutia tumbo joto kwamba yataambukiza mpaka huku
 
Mimi uzuri huwa post zangu sipost kutafuta likes ! !! ! Hii mada iko juu mno ya uwezo wako hii ni ya kimataifa sio ya ndani ya hoja ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi mada ambazo wewe unaziweza kidogo! ! ! Hapa niko anga za kimataifa
Hivi njemba Kama huyo wa Guinea inapo fanya Jambo Kama Hilo hufuata katiba????
Kule kwa kwa hayati Mugabe walifata katiba?
Je Yale yaliyokuwa yakifanyika Nigeria miaka ya 80-90 yalifuata katiba?????
Ya Liberia, Upper Volta kwa Sasa Ni Burkinafaso,Burundi n.k miaka ile pia yalifuata katiba????
Japo tukio la Guinea halipendezi ila Mleta mada umezidi ukali!!!
 
Hakuna kitu kibaya kama kunywa uji wa mapumba ya mahindi na chumvi kama chakula kikuu cha siku.

Ukute mtoa mada ni muhitimu wa chuo fulani tangu 2013 hana ajira, kakaa kwa shemeji imeshindikana akajiunga na forever living anatembea na vipeperushi kila siku kazi kuhudhuria mikutano ya motivational speakers tu kila alhamisi na anasali kwa Gwajima. Unaweza kuelewa ni mtu wa aina gani
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi ni mmojawapo nitakayesaidia kuwezesha hilo Jambazi Mamady Doumbouya kuondoka madarakani wewe subiria hapo hapo utaona
Ungekua na uwezo huo si ungezui kifo cha mbaguzi,mwonevu na dhulumati aliekwenda zake? Lofa kabisa weweeeee!!
 
Ungekua na uwezo huo si ungezui kifo cha mbaguzi,mwonevu na dhulumati aliekwenda zake? Lofa kabisa weweeeee!!
Kifo hajizuiliki ndio maana kinachosubiriwa ni hilo Jambazi Mamady Doumbouya kuuawa
Sasa hivi linaishi kwa kujificha ficha saa yeyote litalambwa shaba
 
Kifo hajizuiliki ndio maana kinachosubiriwa ni hilo Jambazi Mamady Doumbouya kuuawa
Sasa hivi linaishi kwa kujificha ficha saa yeyote litalambwa shaba
Kumbe unajua kifo hakizuiliki ndio maana kuna jambazi lilidondoshwa vilevile Kwa ukatili na uhayawani wake.

Mamedy akidondoshwa Kwa kuuawa au vinginevyo atakua amemwondosha dikiteta la CCM B kule.
 
Sasa kipi bora waongoze wanajeshi au chama tofauti na ccm? Sio kazi ya jeshi kuongoza nchi hilo ni jukumu la raia.
Sasa huko Guinea huyo rais Conde ndio hivyo tena kishashindwa kajiongezea muda kinyume cha katiba na udikteta juu.

Sasa kwa jeshi linalojitambua na lenye uzalendo na nchi yao hawawezi kuwaacha wananchi wao wateseke na ndio maana hata baada ya hayo mapinduzi kufanyika kuna raia wengi wamethubutu hata kuwabusu wanajeshi kama ishara ya kuonyesha uungwaji wao mkono wa tukio la mapinduzi.
 
Kifo hajizuiliki ndio maana kinachosubiriwa ni hilo Jambazi Mamady Doumbouya kuuawa
Sasa hivi linaishi kwa kujificha ficha saa yeyote litalambwa shaba
Eti linaishi kwa kujificha...!!! Wewe utapata stroke bure, shauri yako 🤣

Guinea jeshi linalinda demokrasia sio watawala wa kibabe. Conde urais ndio basi tena.
 
Eti linaishi kwa kujificha...!!! Wewe utapata stroke bure, shauri yako 🤣

Guinea jeshi linalinda demokrasia sio watawala wa kibabe. Conde urais ndio basi tena.
Mamady Doumbouya anaishi kama panya kujificha

Kafanya vizuri sana kuifuta katiba ya Guinea sababu ile ilikuwa in Linda Rais Sasa sababu kuifuta kuua Rais ruksa sababu hana katiba in atommlinda asishitakiwe au kupinduliwa kwa kuuuwa
 
Back
Top Bottom