Haya mapinduzi yanaweza kuonekana yana nia njema hasa baada ya Rais kusigina katiba lakini kwa asilimia kubwa yatakuwa na matokeo hasi kwa wananchi wanaoshangilia leo.
Matatizo waliyoyataja yapo Afrika nzima na historia haioneshi kama wanajeshi huwa wanaleta demokrasia na hali bora ya maisha (isipokuwa Jerry Rawlings tu). Wangeweza kumtoa Rais na kuitisha uchaguzi lakini ndio kwanza wanateua wakuu wa mikoa hiyo si dalili nzuri.
Misri, Sudan na Mali wanajeshi walifanya mapinduzi na hadi leo bado wapo madarakani hawataki kuwaachia raia serikali, na wananchi wakiandamana kuwapinga wanapigwa risasi za moto. Huyu Mamady Doumbouya na Assimi Goita wa Mali walikuwa darasa moja kwenye mafunzo yanayoongozwa na Marekani na Ufaransa.
Marekani, Australia na Ufaransa wameshirikiana kumtoa Rais madarakani kwa maslahi yao na kuondoa ushawishi wa China katika nchi hiyo. Australia ndio muuzaji mkubwa wa iron ore kwa China na tangu mwaka juzi China amekuwa akitishia kuacha kununua madini hayo baada ya kuingia mkataba wa trilion 14 na Guinea ambayo ina madini hayo mengi na bora kuliko ya Australia. Sasa hivi kwa kuwa Rais hayupo China ataendelea kuwa mteja wa Australia. Marekani na Ufaransa hawataki China awe na ushawishi kwenye nchi zote zenye rasilimali Afrika. Kwa sasa utaona mikataba ya madini watapewa makampuni ya kwenye nchi hizo mbili.