Siyatambui mapinduzi Guinea, Rais Conde namtambua kama Rais bado waliomteka nyara wamrudishe upesi

Siyatambui mapinduzi Guinea, Rais Conde namtambua kama Rais bado waliomteka nyara wamrudishe upesi

Mbona naona Wananchi wa Guinea Conakry 🇬🇳 wanafuraha tu
Maigizo tu hayo

Guinea ina miji Mingi sio Conakry tu

Wamekusanya mateja na wahuni wa Conakry mji mkuu kuonyesha wananchi wana wa support

Kama wana support ya wananchi Conakry mbona wamepiga marufuku wananchi wasithubutu kuwa mtaani usiku? Wanaogopa nini wakati wana support?

Hilo Jambazi Mamady Doumbouya lazima lifungashwe virago
 
Hii mada kaa nayo mbali iko juu ya uwezo wako wa akili
Ok ok ok!! Sawa sawa!! Tumekusikia,na baada ya kutafakari kwa muda tumeamua kukuunga mkono,teh teh teh teh, tena usipiteze muda, kamfurushe huyo mamady doumbouya kutoka huko ikuluni kwao haraka,mtu yeyote akikuuliza kwa nini unawafurusha makomandoo wetu mjibu kuwa sisi kama kamati kuu ya ccm tumekutuma,wakileta ujuaji utuambie tumwambie jaji mitungi awafutie usajili haraka sana!
 
Maigizo tu hayo

Guinea ina miji Mingi sio Conakry tu

Wamekusanya mateja na wahuni wa Conakry mji mkuu kuonyesha wananchi wana wa support

Kama wana support ya wananchi Conakry mbona wamepiga marufuku wananchi wasithubutu kuwa mtaani usiku? Wanaogopa nini wakati wana support?

Hilo Jambazi Mamady Doumbouya lazima lifungashwe virago
Hebu niambie alichokifanya Konde ni sahihi?
Amepitisha mwenyewe katiba ya two terms, halafu anaivunja mwenyewe tena
 
Hebu niambie alichokifanya Konde ni sahihi?
Amepitisha mwenyewe katiba ya two terms, halafu anaivunja mwenyewe tena
Conde hajavunja katiba bunge ambalo lina wawakilishi wa wananchi toka kona zote za nchi ndio waliopitisha sio Raisi Conde yeye haingii bungeni na sio mpira kura bungeni. Huyu Jambazi Mamady Doumbouya anadharau wabunge waliochaguliwa na wananchi wote wa Guinea kuwa wajinga yeye ndie ana akili kuliko wawakilishi wa wananchi walioamua hilo kwa mujibu wa mamlaka waliyopewa na katiba.

Mfano hapo Rwanda Raisi Kagame katiba ilibadilishwa aendelee wakati kabla ilitoa ukomo bunge likaongeza muda huwezi sema ohhh Kagame kajiongezea muda aondoke yeye sio bunge na haingii bungeni yeye nani akatae kusaini wish ya wabunge waliochaguliwa na wananchi kutoka Rwanda nzima? Hakuwachagua yeye

Conde pia same case ulitaka asi sign apingane na wawakilishi wa wananchi wabunge waliowachagua?

Alichofanya sio sahihi huyo jambazi Mamady Doumbouya
 
Bunge la Guinea kwa Vikao vyake halali kabisa lilijiongezea posho na kupitisha kuwa Raisi aliyepo Raisi aliyepo ruksa kugombea tena

Kikosi kimoja cha makomandoo bila kushirikisha vikosi vingine vya jeshi wakaenda kumteka Raisi Condé na kumficha wanakojua wao.

Mimi bado namtambua Rais Conde kama Rais halali wa Guinea na nautaka umoja wa Afrika usimtambue huyo jambazi Mamady Doumbouya na Kikosi chake cha majambazi makomandoo waliomteka Rais halali na kujitia eti wamempindua.

Vikosi vingine nendeni mkalipindue hilo jangili. Mamady Doumbouya arudishwe Rais Conde

Naitaka jumuiya ya kimataifa ilaani huo utekaji nyara na hilo Jambazi linalojiita limepindua liuawe chap chap

Kwa mujibu wa katiba ya Guinea hakuna njia ya Jeshi ya kumuondoa Raisi aliyepo madarakani. Jambazi Mamady Doumbouya kavunja katiba
Haya ni maneno yako au unaota tu
 
Hakuna kitu kibaya kama kunywa uji wa mapumba ya mahindi na chumvi kama chakula kikuu cha siku.

Ukute mtoa mada ni muhitimu wa chuo fulani tangu 2013 hana ajira, kakaa kwa shemeji imeshindikana akajiunga na forever living anatembea na vipeperushi kila siku kazi kuhudhuria mikutano ya motivational speakers tu kila alhamisi na anasali kwa Gwajima. Unaweza kuelewa ni mtu wa aina gani
Unajua umenichekesha sana bahati nzuri hapo nilipo nipo peke yangu vinginevyo ningeonekana mwehu kwa kucheka peke yangu.
 
Conde hajavunja katiba bunge ambalo lina wawakilishi wa wananchi toka kona zote za nchi ndio waliopitisha sio Raisi Conde yeye haingii bungeni na sio mpira kura bungeni. Huyu Jambazi Mamady Doumbouya anadharau wabunge waliochaguliwa na wananchi wote wa Guinea kuwa wajinga yeye ndie ana akili kuliko wawakilishi wa wananchi walioamua hilo kwa mujibu wa mamlaka waliyopewa na katiba.

Mfano hapo Rwanda Raisi Kagame katiba ilibadilishwa aendelee wakati kabla ilitoa ukomo bunge likaongeza muda huwezi sema ohhh Kagame kajiongezea muda aondoke yeye sio bunge na haingii bungeni yeye nani akatae kusaini wish ya wabunge waliochaguliwa na wananchi kutoka Rwanda nzima? Hakuwachagua yeye

Conde pia same case ulitaka asi sign apingane na wawakilishi wa wananchi wabunge waliowachagua?

Alichofanya sio sahihi huyo jambazi Mamady Doumbouya
Ndiyo maana kila kitu kimesimamishwa ila kuanza upya.........Alpha ndiyo alitumia nechoro resosesi kuwalaghai hao waganga njaa bungeni.........
 
Condeboy kashakubali yaishe na Douboya kashatangaza kwenye TV kwamba nchi ipo chini ya jeshi.

Sasa wewe unamkosoa Conde kama nani?
 
Ndiyo maana kila kitu kimesimamishwa ila kuanza upya.........Alpha ndiyo alitumia nechoro resosesi kuwalaghai hao waganga njaa bungeni.........
Sawa awe alilaghai au kutumia ushawahi wowote or whatever lakini alikuwa ndani ya katiba framework ya Guinea inachotaka

Hili Jambazi Mamady Doumbouya limetokea wapi wakati katiba halitambuliki?
 
Condeboy kashakubali yaishe na Douboya kashatangaza kwenye TV kwamba nchi ipo chini ya jeshi.

Sasa wewe unamkosoa Conde kama nani?
TV sio katiba hata Itangaze vipi

Uingiaji kwenye uraisi wa hilo Jambazi Mamady Doumbouya hauko kwenye katiba ya Guinea

TV hazimsaidii ku legitimize kuwa yeye Raisi ataishia tu kuuza sura kwenye TV lakini si Raisi ni jambazi tu
 
Bunge la Tanzania liitake serikali itoe tamko kuhusu kilichotokea Guinea na nini msimamo wa serikali

Mbunge yeyote asimame amhoji waziri mkuu kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo au ahoji Waziri wa Mambo ya nje kipindi cha maswali na majibu

Bunge wake up
 
Wakizalisha wakimbizi watatusumbua. Guinea ilishazalisha wakimbizi wakaja Tanzania ndio maana tuna hadi mtaa wa Guinea uliokuwa Zaman umejaa wakimbizi wa Guinea. hatutaki historia ijirudie hilo Jambazi Mamady Doumbouya lifungashwe virago
Unavyoandika kama mtu mwenye maamuzi flani kwenye hii nchi au Guinea [emoji1787][emoji1787]

Watu Guinea wenyewe wanashangilia we hapa unaleta porojo zakoView attachment 1927799
 
Yale ni maigizo kama maigizo mengine. wanashangilia kuvunjwa katiba ya Guinea?

Katiba inatamka wazi kuwa katika njia za kumuondoa Raisi madarakani hiyo ya mapinduzi haimo kwenye katiba

Raisi Conde ni Raisi halali wa Guinea hadi saa hii kwa mujibu wa katiba ya Guinea siyo hilo Jambazi Mamady Doumbouya
Kajavunja katiba bali kaitupilia mbali kwa sababu haina msaada, wanataka waje na katiba itakayomfunga raisi na wabunge mikono. Katiba inatoka kwa wananchi hivyo wananchi wana mamlaka hata kupita katiba yenyewe. Kwa sasa wameamua kumtimua raisi na genge lake
 
Kwenye katiba ya Guinea hiyo statement haimo. jeshi halitajwi kama njia mojawapo ya kumuondoa Raisi madarakani. hilo Jambazi Mamady Doumbouya lazima lifungashwe virago
Imetoka hiyo, ni zamu ya madikteta wengine kufuata.
 
Bunge la Guinea kwa Vikao vyake halali kabisa lilijiongezea posho na kupitisha kuwa Raisi aliyepo Raisi aliyepo ruksa kugombea tena

Kikosi kimoja cha makomandoo bila kushirikisha vikosi vingine vya jeshi wakaenda kumteka Raisi Condé na kumficha wanakojua wao.

Mimi bado namtambua Rais Conde kama Rais halali wa Guinea na nautaka umoja wa Afrika usimtambue huyo jambazi Mamady Doumbouya na Kikosi chake cha majambazi makomandoo waliomteka Rais halali na kujitia eti wamempindua.

Vikosi vingine nendeni mkalipindue hilo jangili. Mamady Doumbouya arudishwe Rais Conde

Naitaka jumuiya ya kimataifa ilaani huo utekaji nyara na hilo Jambazi linalojiita limepindua liuawe chap chap

Kwa mujibu wa katiba ya Guinea hakuna njia ya Jeshi ya kumuondoa Raisi aliyepo madarakani. Jambazi Mamady Doumbouya kavunja katiba
Viongozi wakiwa katika harakati za kujiongezea muhula na kuvunja katiba hamjitokezi kukemea au kuomba jumuiya zikemee huo uhuni. Wakipinduliwa mnajitokeza kupinga. Huo ni UNAFIKI
 
Back
Top Bottom