Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Nafikiri sasa tutaongea lugha moja ya kwamba yanga kucheza michezo 44 bila kufungwa sio jambo jepesi kama wanavyodhani wale mbumbumbu, unatakiwa uwe na kikosi cha maana na kipana kufikia iyo rekodi.
Tumeona leo wazee wa pira litembee walivyoangukia pua mbele ya azam, baada ya kulegezwa na derby ya kariakoo uku wenzao jana wakifanya rotation ya kikosi na kuibuka na ushindi wa kibabe wao wazee wa pira litembee wakaona ufinyu wa kikosi chao isingekuwa rahisi kuzipumzisha bunduki zao na wakatoka salama wakaona waingie nazo hivyo hivyo na wakapasuka.
Tunaposema upana wa kikosi atumaanishi kuwa na rundo la wachezaji bali kuwa na wachezaji wanaoweza kufanya kile wanachofanya wale wanaoanza, Simba leo walitakiwa wafanye rotation ya wachezaji kutokana na energy kubwa waliyotumia kwenye derby lakini wameshindwa kufanya hivyo kutokana na kikosi finyu walichonacho.
Uchovu kwa wachezaji wao umeonekana dhahiri na Azam walitakiwa waondoke na goli si chini ya 3 kama sio kukosa umakini, Sasa yanga kakaa kileleni rasmi kuwatoa pale kwa gape la point 3 kwenye hii ligi ngumu labda liletwe tingatinga vinginevyo safari ndo imeanza rasmi ya kuretain ubingwa wao kwa mara nyingine, Taratibu gadiora mnene ataanza kutupiwa mawe