Nakumbuka wakati niko shule nilizushiwaga nadate na mwalimu wa physics ile skendo ilinitesaga sana nilifikia hatua hadi nikawa najifelisha makusudi maana nilikua nikifaulu tu watu wanasema nimevujishiwa paper,, toka nimeenda shule msosi wa shule nilikua sili ila ikafikia hatua ilibidi nianze kula tu hatakama situmii malage na sipendi kande maana ilikua nikinunua hata chips wanasema hela nimehongwa na mwalimu, nilikuaga kiongozi lakini ikabidi nijiudhuru tu maana ilikua nikisimama assembly hata kutangaza naona kama shule nzima inanizomea[emoji2356][emoji2356]...iliniumiza na kunitesa sana kisaikolojia ukizingatia na mwalimu mwenyewe alikua mkali hata kuanza kumuuliza naogopa naanzia wapi,, nilimwomba mzee anihamishe shule alikataa hadi nikatamani nitoroke[emoji23][emoji23][emoji23].. Nilikuja kujifunza baadae sana kwamba inabidi uishi tu maisha ya kawaida ambayo almost kila mtu anaishi maana ukijiweka tofauti tu watu wanaanza kufanya assumptions za kipuuzi