Sleeper Agent: Mbinu ya kupandikiza jasusi mahali atakayetumika siku za baadaye

Sleeper Agent: Mbinu ya kupandikiza jasusi mahali atakayetumika siku za baadaye

Namtafuta aliyenidanganya kuwa Tanzania ni ya Tatu kwa ubora kwenye ulimwengu wa ushushu.
Vichaa Tanzania ni mashushushu
wapiga debe mashushushu
yaani kila MTU shushushu na ushushu hawaujui

Kuna kichaa mmoja mwanamke alikua anajua kalenda hatari, anakuuliza ijumaa mwezi wa 7 itakua tarehe ngapi na hapo upo mwezi wa 3, ukikosea tu anakwambia anapiga hesabu anapatia kabisa, wakaanza kusema usalama usalama, dah yule mama alipoteaga gafla tu
 
Huu uzi ni kama umeclick kwa mind yangu!
Namkumbuka chalii mmoja tulisoma nae chuo, huyu hakika alikuwa ni sleeper agent wa TUTSI EMPIRE dogo kainflitiate hadi jeshini na sahivi ni mgavi huko jeshini na ana nyota3!
Dada zake na nduguze wote wako na nyadhifa huko kwa Kagame!!


Daaaahhhh aseee na mimi pia kuna jamaa mmoja mganda yupo chuo flani yaani HAKIKA yule jamaa katumwa umenikumbusha kitu asee,
 
Naona mfano mzuri wa sleeper agent ni bwana 'tribe' Rais wa nchi jirani yetu, aliingia kwenye Familia kwa Muda mrefu akatulia akaja kukamilisha mission baada ya Muda kufika.... Asante kwa somo la leo
 
Ndio maana siku zote nina wasiwasi na DIASPORA ambao baadae huja na kupewa nafasi za juu kisa tu elimu zao
 
mweeeeeeh akili kumkichwaaa....wacha mi nijilimie nyanya zangu tu
 
Namtafuta aliyenidanganya kuwa Tanzania ni ya Tatu kwa ubora kwenye ulimwengu wa ushushu.
Vichaa Tanzania ni mashushushu
wapiga debe mashushushu
yaani kila MTU shushushu na ushushu hawaujui

Bujibuji tuheshimiane, acha kuwadharau vichaa wetu. Wamejitolea kuishi kama vicha kwa maslahi taifa. Were huoni hao vichaa jinsi walivyo, nguo chafu, mwili mchafu, nywele chafu lakini visigino havina hata Magamba.
 
'Sleeper agents' wetu wapo busy kugawa pesa za kununua viongozi wa upinzani, huku wengine wakiwa busy kujua mikutano ya vyama vya siasa itafanyika lini na wapi.
 
Basi Tanzania kulikukuwa na kuna Sleeper agents wengi sana, maana hata kabla na baada ya uhuru tumekuwa ni nchi ya almost everybody from anywhere in the world kiasi kwamba wengine walipewa ajira kwenye taasisi za umma na wengine kushika madaraka ya juu ndani ya serikali.

Labda ndio maana nchi hii imekwama pamoja na kuwa na utajiri wote huu.
 
Kiongozi, hongera sana Umetoa Elimu ya maana sana. Ila kitu cha pekee ni raia kuwa na uzalendo kwa Taifa lako
Kitu pekee ambacho hupelekea mataifa wanaotumia Sleeper Agent ku fail ni Uzalendo.
kwa mfano mtu katoka Tz kwa scholarship akarudi nchini tayari kashapandikizwa, kunachangamoto kubwa sana mtu huyu kwa sababu za kiubinadamu kuja kuwasaliti ndugu zake Kaka,dada,mama, baba (Taifa lake)

Sijawahi kufanyakazi ktk idara nyeti za kiusalama ila kunawakati napata maswali mengi sana kwa baadhi ya mambo ninapo yaona au kusikia...naamini wengi wetu mtakuwa mshashuhudia unapita mjini au mitaani unakuta Raia wa kigeni wapo huru kabisa wanapiga picha maeneo yetu, watu, nk. Je umehijiuliza kwa nin wanapiga? na hizo picha zinaenda kutumika wapi?

Kuna story moja alinisimulia mzee mmoja kuna raia wa kigeni walikuja miaka hiyo kama watu wa dini, siku moja wakaenda kutembea milimani wakiwa na wenzake kilichomshangaza ni huyo raia kuwa na Tatoo mgongo wote (ukristo hauruhusu kujichora) kumbe Tatoo hizo ni ramani ambayo inawaelekeza mahali ambapo kunamakaburi, na hayo makaburi kumbe sio ya watu bali ni mahali wakoloni inasemekana walizika mali...

Ni vizuri kuwa na uzalendo na Taifa letu ili sisi na ndugu zetu na mali zetu tuwe salama, kuna mbinu nyingi zilikuwepo, na zina zidi kuongezeka kutokana na maendeleo ya kitecknolojia kuhakikisha mbinu za kijasusi zinakuwa juu sana ndani na nje ya kila Taifa

Uzalendo unatakiwa uanzie kwa wanasiasa na watawala,huwenzi kulazimisha/kumfanya mtu kuwa mzalendo kwa maneno matupu,uzalendo sehemu yake kubwa ni matendo. Bahati mbaya nchi hii imekosa watu wa kuigwa kwa uzalendo wao,baada ya Sokoine na Mwalimu Nyerere hakuna zaidi ya hapo,yaani waliobaki wote hawana sifa ya uzalendo,si mkubwa wala mdogo kila mtu anapambana na maisha yake.

Kuwafanya wananchi wako kuwa wazalendo ni lazima uwaunganishe pamoja nao wananchi waamini hivyo kwamba wako pamoja na wote ni sawa. Lakini kwa wakati huu tuliopo tutaimba sana kuhusu uzalendo na wala hatutafanikiwa,sababu kubwa ni kwamba watawala wametugawa sana kimatabaka.
 
Back
Top Bottom