Kwa maono yangu, upinzani tz kumejaa sleeper agents wa kutosha, kamwe hautokuja shamiri.
Angalia Dr. Slaa alivyoaminiwa na Chadema, plus watanzania kwa ujumla, ule wakati ameishaiva na yupo tayari kwa mapambano ya kinyang'anyiro cha uraisi, akashiriki kumleta Lowasa, yeye akachapa lapa. hapa kuna namna ukizingatia alitokea CCM huko nyuma.
From no where Mbatia akapewa Ubunge wa kuteuliwa, kwa siasa za Tanzania ni kitendawili ilitokea tokea vipi, in no time ukawa ukaundwa akiwa mwenyekiti mwenza, leo ukawa ni kama imepotea sababu za ukawa kufifia hata hazionekani.
Kuna mtu anaitwa Lipumba, yani muda ukawa imeshika hatamu, akajirudisha uenyekiti CUF, hadi leo CUF haisomeki.
Kuna mtu anaitwa maalim Seif, aliwaigi kuwa kindakindaki kwenye ujana wake, it makes no sense kuasi ujana wake.
nnawashuku wengi, mwisho hapa nimuweke babu yangu Kingunge, kabisaa huyu babu amekunywa maji ya kijani kilichoiva, eti kirahisi rahisi tu hivyo aondoke CCM.
Kama ulidhani tz kuna upinzani, mpinzani ni wewe.
Nyerere was very genius, akaona hawa watu wanataka vyama vingi, kura hazijajitosheleza hivyo wataendelea kusumbua, ruksa wape vyama vingi, ila penyeza kote watu wako, na ikawa hivyo, CCM itaendelea dumu milele na milele.