Sleeper Agent: Mbinu ya kupandikiza jasusi mahali atakayetumika siku za baadaye

Namtafuta aliyenidanganya kuwa Tanzania ni ya Tatu kwa ubora kwenye ulimwengu wa ushushu.
Vichaa Tanzania ni mashushushu
wapiga debe mashushushu
yaani kila MTU shushushu na ushushu hawaujui

Kuna kichaa mmoja mwanamke alikua anajua kalenda hatari, anakuuliza ijumaa mwezi wa 7 itakua tarehe ngapi na hapo upo mwezi wa 3, ukikosea tu anakwambia anapiga hesabu anapatia kabisa, wakaanza kusema usalama usalama, dah yule mama alipoteaga gafla tu
 


Daaaahhhh aseee na mimi pia kuna jamaa mmoja mganda yupo chuo flani yaani HAKIKA yule jamaa katumwa umenikumbusha kitu asee,
 
Naona mfano mzuri wa sleeper agent ni bwana 'tribe' Rais wa nchi jirani yetu, aliingia kwenye Familia kwa Muda mrefu akatulia akaja kukamilisha mission baada ya Muda kufika.... Asante kwa somo la leo
 
Ndio maana siku zote nina wasiwasi na DIASPORA ambao baadae huja na kupewa nafasi za juu kisa tu elimu zao
 
mweeeeeeh akili kumkichwaaa....wacha mi nijilimie nyanya zangu tu
 
Namtafuta aliyenidanganya kuwa Tanzania ni ya Tatu kwa ubora kwenye ulimwengu wa ushushu.
Vichaa Tanzania ni mashushushu
wapiga debe mashushushu
yaani kila MTU shushushu na ushushu hawaujui

Bujibuji tuheshimiane, acha kuwadharau vichaa wetu. Wamejitolea kuishi kama vicha kwa maslahi taifa. Were huoni hao vichaa jinsi walivyo, nguo chafu, mwili mchafu, nywele chafu lakini visigino havina hata Magamba.
 
'Sleeper agents' wetu wapo busy kugawa pesa za kununua viongozi wa upinzani, huku wengine wakiwa busy kujua mikutano ya vyama vya siasa itafanyika lini na wapi.
 
Basi Tanzania kulikukuwa na kuna Sleeper agents wengi sana, maana hata kabla na baada ya uhuru tumekuwa ni nchi ya almost everybody from anywhere in the world kiasi kwamba wengine walipewa ajira kwenye taasisi za umma na wengine kushika madaraka ya juu ndani ya serikali.

Labda ndio maana nchi hii imekwama pamoja na kuwa na utajiri wote huu.
 

Uzalendo unatakiwa uanzie kwa wanasiasa na watawala,huwenzi kulazimisha/kumfanya mtu kuwa mzalendo kwa maneno matupu,uzalendo sehemu yake kubwa ni matendo. Bahati mbaya nchi hii imekosa watu wa kuigwa kwa uzalendo wao,baada ya Sokoine na Mwalimu Nyerere hakuna zaidi ya hapo,yaani waliobaki wote hawana sifa ya uzalendo,si mkubwa wala mdogo kila mtu anapambana na maisha yake.

Kuwafanya wananchi wako kuwa wazalendo ni lazima uwaunganishe pamoja nao wananchi waamini hivyo kwamba wako pamoja na wote ni sawa. Lakini kwa wakati huu tuliopo tutaimba sana kuhusu uzalendo na wala hatutafanikiwa,sababu kubwa ni kwamba watawala wametugawa sana kimatabaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…