Soko la Kariakoo lateketea kwa moto

Soko la Kariakoo lateketea kwa moto

Mkuu si unawajua hao? Wana vifaa chakavu na mara nyingi hawana hata tone la maji.
Fire si wapo mita 1000 tu toka hapo au na leo hawana maji
Hawana maji. Ningekuwa Rais wa nchi ningeanza kumtumbua Mkuu wa jeshi la zimamoto na viongozi wote wakubwa katika vituo vya zimamoto

Kwanini magari ya uokozi yakose maji??

Wao wanafanya nini? Au ndio kufanya kazi kwa mazoea

Hii nchi hii...HOVYO KWELI.
 
Hawana maji. Ningekuwa Rais wa nchi ningeanza kumtumbua Mkuu wa jeshi la zimamoto na viongozi wote wakubwa katika vituo vya zimamoto

Kwanini magari ya uokozi yakose maji??

Wao wanafanya nini? Au ndio kufanya kazi kwa mazoea

Hii nchi hii...HOVYO KWELI.
Labda wanahusika kwenye hujuma
 
Miaka yote fire bongo yanakujaga bila maji.
Sijawai kusikia uzembe huu mahali popote.
Tulipewa Semina Na Hao Hao Fire..Wanadai Huwa Wanakuja Kuangalia Sababu ya Moto ili Wajue Waje na Type Gani ya Fire Extiguisher..Cjui walitupiga Fix
 
Shule ya sekondari ya at taun ya kiislamu morogoro eneo la mji mpya nayo imewaka Moto leo usiku.
 
kulala MO kuamka MUDI ndo haya sasaaa... ishakuwa noma pole sana kwa wale waliokopaa mabank Mungu awatie nguvu maana umaskini sio kitu chema.
Ukweli ndio huo, Muumba awape nguvu
 
Tulipewa Semina Na Hao Hao Fire..Wanadai Huwa Wanakuja Kuangalia Sababu ya Moto ili Wajue Waje na Type Gani ya Fire Extiguisher..Cjui walitupiga Fix
Kujua class ya moto ni muhimu, inaonesha hawa wanategemea sana maji nakati maji yanazima aina moja tu ya moto,
Dry Powder ndio Universal, inazima almost classes zote za fire..

Nakumbuka mwaka juzi kule Simiyu, eti gari la zimamoto limeenda site kufika site out of nowhere likaanguka maji yakamwagika, ikabidi watu waanze kuchota maji kwa ndoo, gari limetulia pembeni, Mwaka mmoja baadae maeneo ya Coco Beach tukio kama hilo hilo
Screenshot_2021_0711_081820.png
Screenshot_2021_0711_081215.png

Sikutaka kuamini ila ndio futuhi hii.
 
Mi binafsi kuna mdau alileta uzi umu nafikiri ni majuzi kwamba moto unawaka kariakoo kitu ambacho akikua kweli,baada ya muda ule uzi ukafutwa

Swali ni sisi kujiuliza yule mtoa uzi alikua na lengo lipi au aliwasha moto ikashindika iyo juzi? Leo hii ndio umefanikiwa ? Au unabii wa jf najiuliza apa sipati jibu?
Moderator wanachakujifunza badala y kufuta wawe wanaficha nyuzi au kufanya namna yoyote kopi ibaki
 
Pole sana kwa wahanga wote walioathiriwa na moto huo , hapa sasa ndipo umuhimu wa bima unapokuja ili wapate fidia...

Naona watu wengi wanatupia lawama jeshi la zimamoto (Fire rescue), Magari ya zimamoto hua yana Tank dogo sana almost litre 10,000 ambayo kwa dakika 15 tuu maji yanakua yameisha,
Hivyo majengo kama hayo hayana budi kuwekwa smoke detector, fire horse reel na fire hydrant ili maji yakiisha kwenye gari la fire basi watape hapo kwenye fire hydrant,
Kutoa lawama nyingi kwa watu wa fire wakati majengo hayakidhi viwango ni kuwaonea,
Soko linachukua ushuru wangechimba underground water tank then wanakusanya maji ya mvua na Dawasa, wananunua na pump kubwa haizidi 15m linapotokea tukio kama hilo fire kazi yao inakua nyepesi,
Sasa gari limefika likiishiwa maji linaenda kufuata maji mpaka wakirudi moto unazidi kuteketea...
Poleni sana
 
Kulikuwaga na sehemu kuliwekwa mabomba maalum ambayo fire walikuwa wanaunganisha
Mipira yao wapate maji wakati wa dharula
Hiyo miundo mboni yote tushaiuaaa

Ova
 
Back
Top Bottom