Soko la Karume limeungua moto

"TBL fire brigade walijaribu kutaka kuzima moto kwani uko karibu na depot yao wakakatazwa, kwamba waangalie moto usivuke kwenda kwenye depot yao na kwa wananchi ila mengine hayawahusu".

Mleta mada nimekuelewa mno mno kwa hayo maneno yako niliyoweka katika quoate. Mungu ndiye hakimu mtoa adhabu stahiki.
 
Mkuu hii ni awamu ya wanyonge kutubu😂 zamu ya matajiri na mafisadi kuwahenyesha maskini!

Sasa mtachagua kama muendelee nae au mchague mwengine ~ Job Ndugai
 
Moto wa mchongo 😂😂😂 aliskika mnyonge mmoja
Inaumiza sana ila kama kuna mtu anahusika na hili Mungu ampe mwisho mbaya afee kifoo kibaya maana hajui watu wanaumiza sana vichwa kukuza vimtaji vyao na kama nitasikia serikali inataka kumpa mwekezaji ndo tutajua kumbe ni moto wa mchongo
 
Halafu wiki hii ndiyo shule zinafunguliwa. Kuna Mali nyingi Sana. Tena kuna zile zinaitwa mbegu zikikusanywa baada ya muhula wa shule kuhitimishwa na kuja kuuzwa mhula mpya ukianza. Yaani mabeji kama yote brand, viatu, nguo za shule n.k.. . Kama kuna hujuma Mungu wapige upanga wa Moto wote waliohusika.. . Kifupi Machinga complex hakufai kabisa kuwa a business centre. Ni kuchafu, ujenzi wa hovyo. Yaani hakuna hadhi ya kumpeleka mnunuzi Kule.
 
Sasa kama ni jukumu la kila mmoja mbona inaonekana hao wamachinga ndio wanaopaswa kuandama kuliko wengine?
 
Ni maandishi tu ila hayapatikani bila kula kipigo cha polis ccm😅😅😅 lazma mpambane na kipigo mpaka umoja wa mataifa uingilie kati ndio mpewe hio katiba😅!

Hamna ambaye hajui kuwa katiba ni haki ila tunatambuwa uwepo wa kipigo cha polisi form 4 failure hiko ndio wananchi hawakitaki ndio maana wanavumilia kama makondoo
 
Ww ndio umepotea KABISA na hamjitambui.. mnamsifia tu JPM kila siku.. si mkamfufue sasa?? Mtu aliharibu sana hii nchi na inaendelea kuharibika sababu yake..
Aliharubu nchi kimpango gani? Hebu acha ushamba bana wewe! Huyu mama alichofanya cha maana kipi mpaka sasa kama sio kuhenyesha maskini tu? Au sababu hamdu shaka ami yako kapewa uwenezi?
 
Utawala dhalimu una halalisha uhalifu, dhuluma, wizi, rushwa na ufisadi
Safi sana mama anaupiga mwingi mno! Kazi iendelee tukitoka hapo tuhamie la Ilala Boma pale napo tuwaunguzie!

Wamachinga wanachafua sasa jiji watalii wanaona uchafu umezidi, waende kitunda huko au chamazi wakauze bidhaa zao!

Magufuli yeye alikuwa anatetea wanyonge ni fala tu kama ambavyo tulimsindikiza na vibwagizo hivyo mwezi march mpaka septemba😅 wacha twende na mama!
 
Tatizo unaongea hivyo halafu usikute upo nje ya nchi huko au yakipangwa hata maandamano tu wewe unaishia humu JF kuangalia itakuaje huingii road halafu unawaita wenzako huku wajinga.
 
Safi sana mama anaupiga mwingi mno! Kazi iendelee tukitoka hapo tuhamie la Ilala Boma pale napo tuwaunguzie!

Wamachinga wanachafua sasa jiji watalii wanaona uchafu umezidi, waende kitunda huko au chamazi wakauze bidhaa zao!
Kitunda ndege zikiwa zinatua na watalii, Wamachinga wataonekana. Itafaa wamachinga wote nchini wahamishiwe Nkasi Rukwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…