Soko la Karume limeungua moto

Soko la Karume limeungua moto

Lakini ndo wakome maana yaliitishwa maandamo wakajifanya wako bize na mambo yao na vitambulisho feki,haya sasa wakale walipopeleka mboga...

Watz hawasikii mpaka wapigwe nyundo km hizi
Tatizo hapo ni kudhani kwamba wao hawana la maana la kufanya ndio maana unaona kuwa wao walipaswa kuingia barabarani kuandamana tofauti wengine ambao wapo maofisini tena ya serikali hiyo hiyo.
 
Naomba nikuulize CCM imevunja katiba kuwabakiza wabunge walifukuzwa CHADEMA. Mbona hamna hatua yoyote iliyochukuliwa? Mimi nimekuwa nikidai katiba mpya muda mrefu lakini nimegundua kuna tatizo kubwa sana kwetu, tunaogopa kudai haki zetu. Katiba ni maandishi tu, ni jukumu letu kuhakikisha inatekelezwa. Tunataka maandishi lakini tunaogopa kutekeleza.

Kwasasa, Ukitaka Kudai utaulizwa kwa Sheria ipi na Kwa Katiba Ipi. Tunaanza na Katiba ambayo itasema kuhusu viongozi Kuwajibishwa then kutokea Pale Sisi tutasimama Kudai haya. Na huu ni Utanzania Tuuu wa kutaka Mwenye shida au uhitaji Akunyenyekee hadi pale utakapo amua kumpa.

Nikupe mfano, Mwezi uliopita Rais Wa Marekani alitoka Hadharani na kutaka Wananchi wawe wanavaa Barakoa muda wote, Wachanje kwa lazima na iwe lazima Kupima Kupima Covid-19 kila Wiki. Lakini Kabla hata Wananchi Hawajalalamika, Mahakama Ilijitokeza kwa Mamlaka Iliyo nayo KIKATIBA, ikapinga na kuzuia Tamko, la Rais Wa Marekani. Wana nafasi Hiyo Kikatiba.

Ingekuwa Tanzania Jaji Mkuu angekuwa anaandika Barua Ya Kujiuzulu sahizi. Tunataka Katiba Mpya Kwasababu Katiba ya sasa Haiwawajibishi Viongozi wetu, Rais Ndio Kila Kitu mwisho wa Siku Ugomvi wao kama Viongozi wakuu, Unatutesa Wananchi wa Hali ya Chini.
 
Umeongea kinyume.Watu ndiyo hawana huruma na maisha yao kwa kuruhusu kutawaliwa na mbwa-CCM.
Kutupia kila lawama kuwa ni kwa sababu ya ccm kuwa madarakani sidhani kama ni sahihi kwa sababu kwa sababu hata kikija chama kingine kutawala haina maana hakitafanya makosa, kwa hivyo kama yanatokea makosa na hatuna cha kufanya zaidi ya kufikiria kukiondoa chama tawala madarakani basi hilo ni tatizo kubwa maana hakutakuja kutokea chama ambacho kitakuwa ni kikamilifu.
 
Noma sana tulipofika yani... daah wanangu waiza viatu pale wedata mzigo wote umeisha hawajui wanaanzia wapi

Af ukute wahuni waliochoma wako zao bar sa izi wanakula monde tu
 
Kutupia kila lawama kuwa ni kwa sababu ya ccm kuwa madarakani sidhani kama ni sahihi kwa sababu kwa sababu hata kikija chama kingine kutawala haina maana hakitafanya makosa, kwa hivyo kama yanatokea makosa na hatuna cha kufanya zaidi ya kufikiria kukiondoa chama tawala madarakani basi hilo ni tatizo kubwa maana hakutakuja kutokea chama ambacho kitakuwa ni kikamilifu.
CCM wanapaswa kulaumiwa kwa kuwa ndiyo wanachoma haya masoko na kuhamasisha ufisadi.

Kusema kuwa hakitakuja kutokea chama ambacho ni kikamilifu siyo sahihi kwa sababu hatuna ushahidi na hilo.

Lakini kuwaita CCM kuwa ni mashetani na waharibifu wa nchi hii ni sahihi kabisa kwa sababu tuna ushahidi wa wazi kabisa wakihamasisha ufisadi katika nchi hii.
 
Soma upya.Nimeandika "kuruhusu CCM kushika dola" na wala siyo CCM kushinda chaguzi kama unavyodai.
Sasa utasemaje wao ndio wameruhusu ikiwa wao wanapiga kura ili kuwaondoa ccm ila ccm inatumia mabavu ya jeshi kuendelea kukaa?
 
Amosi Makala, Ni mkuu wa Mkoa, Ni kiongozi wa Usalama Katika Mkoa wa Dar Es Salaam, Hata Aki GUGU majukumu yake ataona JUKUMU kubwa alilo nalo Ni Kusimamia Usalama wa Mkoa Wa Dar Es Salaam. Na Usalama Wa Kumkoa Wa Dar Es Salaam ni Neno pana Ikiwa ni pamoja na Kuhakikisha Kuwa Majanga Kama Haya Hayatokei, Na Hata Yakitokea basi Aweze Ku GUGU na Kunapata Majibu ya Nani Anahusika na nini Kifanyike, Na Hatua Gani Zichukuliwe, Chanzo Chochote kile cha Moto kina Mtu nyuma Anaye Husika, Iwe kwa Bahati Mbaya au kwa Kukusudia Chanzo Chochote Kile lazima Kiwe na Muhusika, na Kanuni za FORENSIC zinasema, Tukio lolote lile linapotokea basi Lazima Huwa kuna Alama 1 au 2 zitakazo kukusaidia kukupa Crue na Kujua Nini Kinaendelea.

Nitoe Mfano Kuna Mwaka Nigeria, Ulitokea Mripo Mkubwa Sana karibu Na Shule ya Kanisa, Siku ya Jumapili wanafunzi wakiwa wanasali. Katika mripuko ule Watu Takriban 23 walifariki, watu wa NPCS walitokeza wakasema hawajui chanzo huenda ni bomba la Gesi lilipuka. Lakini ilifanyika Forensic investigation ilikuja kuonekana ni UZEMBE wa Viongozi wa NPCS na Uzembe ule ulionesha watu wanaoishi maeneo ya Karibu na Zilipo pita njia za Mafuta na Gesi walipata miripuko zaidi Ya 3 maeneo tofauti tofauti. Watu waliwajibishwa hadi Leo miripuko ya kizembe iliyo kuwa inatokea ni historia.

Amosi Makala, Masoko karibi 4 yameungua Dar Es Salaam, Lakini bado wanachekeana na Rais Wake na Kupongezana kwa kazi Nzuri like Seriously? Wakati watu wanapoteza mali zao? Matukio ya Ujambazi kipindi hiki cha Makala Ndio Usiseme sasa Anafanya nini? Kungekuwa na Katiba inayo muwajibisha sahizi makala Kwa Tukio la Kariakoo, Au Mwenge Ilitakiwa Tusiwe Naye ameshindwa. Hivi ni Nani Alipaswa Kuondoka Kati ya Ndugai Na Makala? Makala Anaacha Kusimamia Usalaama Anaenda Kushadadia Mikopo na Ku GUGU.

Watanzania Tuamke
 
Hii trend ya kuunguza masoko bado haijaisha tu?

Naambiwa soko la Karume limeungua lote na hakuna kilichobaki.

Hivi karibuni kumeibuka mtindo wa kuunguza masoko ya machinga maeneo mbali mbali nchini ikiwa na lengo moja la kuwaondoa machinga.

Najiuliza, mbona karume watu walikua tayari organized, shida ni nini? Mnalazimisha watu wakapange kwenye vizimba machinga complex ambavyo tayari mlishajimilikisha ili mpate pesa ya kula.

TBL fire brigade walijaribu kutaka kuzima moto kwani uko karibu na depot yao wakakatazwa, kwamba waangalie moto usivuke kwenda kwenye depot yao na kwa wananchi ila mengine hayawahusu.

Ipo siku hawa mnaowaonea itafika siku watachoka.

View attachment 2083158
Apa kwa Mungu kuwa ulikuwepo na ulisikia wakati wanakatazwa.
 
Huyu Makala bado anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa masoko yanaungua kila siku na hakuna hatua zozote zinachukuliwa??
 
Tatizo hapo ni kudhani kwamba wao hawana la maana la kufanya ndio maana unaona kuwa wao walipaswa kuingia barabarani kuandamana tofauti wengine ambao wapo maofisini tena ya serikali hiyo hiyo.
Wewe kwa akili yako unafikiri mtu alieajiriwa serikali ofisini ataandamana!?

Ata ivyo kuandamana ni kujitolea muda na wala sio kukosa shughuli ya kufanya,ni jukumu la kila mmoja kwa ukombozi kamili vinginevyo kila siku majanga ya kila aina yanaongezeka
 
Back
Top Bottom