Soko la Vetenari lililoko maeneo ya TAZARA linateketea kwa moto, Chanzo Hitilafu ya umeme

Hivi kuna MCHONGO wowote kutokana na haya masoko kuungua??!!
 
Duh juzi nmetoka kununua machungwa hapo bei poa sana shiling 60/= kila chungwa
 
Duuu yaani mie naendaga pale nanunua ndizi za 3000 lundo watoto wanakula mpaka basi
 
Wafanyabiashara hasa wengi jambo la kukatia bima shughuli zao wanalionaga kama upuuzi fulani hapa UK bima hukatwa kwanza na ndiyo licence hutolewa.

N. B, BIMA ILIVYO YA LAZIMA KWENYE MAGARI NA KWENYE BIASHARA UWEPO ULAZIMA HUO.
Suala la bima kwa Watanzania wengi bado sana inabidi juhudi za ziada za uhamisishaji na elimu ya bima itolewe kwa jamii labda kutakuwa na mwamko wa kukata bima za aina mbalimbali
 
Tuache kuwatupia lawama wasiostahili. Masoko yetu kwanza ni machafuuuuuuu, vyupa vya mikojo, maji machafu kila kona, tope, pili tunaendesha shughuli mseto ambazo kwa kiasi kikubwa hazikupaswa kufanyika ndani ya eneo moja yaaaani wachomelea vyuma, mama ntilie na majiko yao ya mkaa, Wauza Gesi wako eneo moja na muuuza ndizi na matikiti maji anayeizia chini kwenye nyasi kavu. Just imagine nyasi na moto wa mkaa wa mama ntilie?
Fire ilipoyaka kuboreshwa inunuliwe mitambo ya uhakika na vitendeakazi vinginevyo KANGI LUGORA akaonekana hafai, Watanzania mkapiga kelele TUMBUAAAAAAAAAAAAA Mzee akafanya yake.
Sasa ngoja mtumbuliwe nyie na moto
 
Huwa ninaamini tatizo la waafrica sio viongozi bali ni wananchi. Na hata hapa kwetu tatizo sio la viongozi bali ni sisi wananchi, mfano ona hii akili iliyotumika hapa kuandika comment
 
Kwa mujibu wa Kamanda wa Zimamoto mkoa wa kizimamoto Temeke Mrakibu Msaidizi Michael Bachubira amesema Hadi sasa Jeshi linaendelea kuuzima moto huo na kudhibiti usisambae maeneo mengine na kwamba wanaendelea kuchunguza chanzo cha moto huo.
Haya matukio yalihusishwa na mwanasiasa mmoja ni kama yana uweli vile ukitazama historia ya alikopitapita
 
Ndio ukae chonjo nenda kakate bima aisee hii kitu imeshakuwa kwenye masoko yote yajiandae na haya majanga.
Hata ukate bima hulipwi soko likiunguzwa, uchunguzi utasema Wenye bima ndo mmechoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…