Sokomoko la zawadi ya gari ya Rais mstaafu Mwinyi

Tuwe na roho ya utu, huruma na upendo.
Mzee Mwinyi amefanya mangapi kwa watanzania? Leo tunahoji mzee Mwinyi kupewa gari ambalo anaweza kupanda na kushuka vzr sawa na umri wake wa miaka 96?

Tukumbuke kuwa wanae hawajashindwa kununua Benzi kwa ajili ya Baba yao.

Na Serikali isingeshindwa kununua/kugawa gari kimya kimya, limefanyika kwa uwazi kwa sbb si la nia ovu.

Suala la kumpatia mzee Mwinyi gari halina lengo baya ni kuzidi kutambua mchango katika uongozi wake.
 
Kuna wazee wastaafu wengi tu wanapata shida kwenye usafiri wa umma mara mia ya anavyopata Mwinyi kupanda "vieite" lake.

Naishauri serikali iwape msamaha wa kodi wastaafu wote kwenye kuagiza gari at least moja.

Hii nchi ni yetu sote!
Mkuu Kame, ebu fafanua vizuri huu ushauri wako "Serikali iwape msamaha wa kodi wastaafu WOTE kwenye kuagiza gari at least moja" ushauri huu unawahusu Marais wastaafu au na wastaafu wa Umaa.
 
Anaanza kutumia madaraka yake vibaya, Mwinyi anashindwa kunua gari kwa hela yake ? Au kuna utakatishaji hapa ? Umzaniae sie kumbe ndie ,ya Mungu ni mengi ,tokea aache uraisi ni miaka mingapi,pensheni anapokea ,ukisikia ubazirifu na huu nao upo kwenye aina fulani.
 
Tatizo ni kuwa, bimkubwa juzi tu kawaambia wazee wa dar kuwa hakuna fedha ya kuwapa walau 30,000 kwa mwezi. Jana amemtunuku mzee Mwinyi Benz, watu wanamaind hilo pia.

Tujue tu kuwa mwenye nacho anaongezewa, Hussein angeweza kumnunulia mzee wake hiyo Benz coz hashindwi, mzee anapata pensheni nono kila mwezi....
 
Mkuu Kame, ebu fafanua vizuri huu ushauri wako "Serikali iwape msamaha wa kodi wastaafu WOTE kwenye kuagiza gari at least moja" ushauri huu unawahusu Marais wastaafu au na wastaafu wa Umaa.
Watumishi wote wa umma wastaafu wawe wanapewa msamaha wa kodi ili kwa watakaoamua kumiliki usafiri wapate ahueni ya gharama.
 
Zawadi ya gari ina ubaya gani?
Hapo sasa, na hicho kitu kingine wanataka kiwe nini? Naamini hata hicho kitu kingine wakuhoji wangehoji tu. Ni nani chini ya jua anaweza kufanya kitu kila mtu akaridhika?
 
Kwa hela walizo nazo hawa wazee hapakua na u muhimu wa kununua gari la bei ivyo ili hali nchi yenyew ndo kama hivi
Halijanunuliwa wamelitoa bohari na bado yapo meng tu kuanzia mavieite mabenz km LA Babu manisan km ya mwendazake makosta wameyaweka kule kwa ajili ya kwao wao Bi Mkubwa tangu aingie bado hajanunua anatumia oda ya mwendazake.
 
Hii hii benz ni miongoni mwa benzi 20 zilizoletwa na Mfalme wa Morocco King Hasssan VI, as a gift ambapo Mwendazake alijimilikisha kama mali yake binafsi. Kugawanywa leo kwa Kiongozi mstaafu nahisi zimeshataifishwa, na ni sahihi!
 
Afrika insu ni kuupata huo Urais ,ila ukifanikiwa inakuwa Mungu wa Nchi
 
Aliyekuwa anauza jogoo alikuwa ni kuongozi wa kitaifa?
Lakini pia alinunua hakutoa zawad,

Sasa.mwinyi kapewa gari, je yeye katoa mikioni mia saba ilintuone kazidisha bei ya gari?
Alitumia pesa ya jamhuri au ya kwake binafs!!?? Lkn sidhan km wanaweza weka maten pasent ktk dili km hili LA laki
 
Watumishi wote wa umma wastaafu wawe wanapewa msamaha wa kodi ili kwa watakaoamua kumiliki usafiri wapate ahueni ya gharama.
Mkuu ushauri wako uko vizuri, maana akisitafuu amekuwa amechoka tayari.. Yah ushauri poa.
 
Akiba ya fedha za kigeni baada ya Vita vya Uganda iliteremka, nchi ilikuwa haikopesheki na maahirika ya fedha kimataifa, Watanzania walikuwa wanakula mchele wa msaada wa kitumbo, unga wa yanga. Halafu vyote hivyo unavipata kwa foleni. Huko Mtwara wananchi walikuwa wanavaa mifuko ya visulphate kama mashati.

Mwinyi ndiye aliyeruhusu biashara huria, kuanzishwa kwa daladala, kuingizwa kwa mitumba kutoka Ulaya. Akaruhusu watu wafanye biashara mbali mbali. Hata kitimoto kwa wakristu kuliwa openly kwenye mabaa kilianza wakati wake.

Hata privatization ya maahirika Kama TBL na TCC ilianzia kipindi chake na uanzishwai wa TRA.

Muache babu afaidi nchi aliyosaidia kuijenga
 
Mbona nasikia Samia ni mtoto wa nje wa mzee Mwinyi.Samia Hassan .Ahaaa.Mechi imehahirishwa.
LUPEM umepotea kwa hiyo assumption yako. Binti mkubwa wa Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye ni mkubwa kuliko Dr Hussein, na anazaliwa na mama tofauti anaitwa Fatma mke wa Kagasheki na kasoma IDM Mzumbe mwaka 1989. Suluhu naye kasoma IDM Mzumbe mwaka 1986. Hicho ndiyo kinawachanganya

Nimesoma nao wote wawili na ninawafahamu
 
Kama yepi?
1. Kwenye uongozi wao walichukua Chao mapema, (ni matajiri)
2. Magu aliwajengea mahekalu.
Leo mtu anapewa zawadi ya kuzaliwa gari ya mamilioni
Huku wazee wetu wa mitaani wanaomba hisani ya kutibiwa bure kutoka na umri wao, hata ivo hawapati
INAKERA.
 
Hakujenga pekee yake, yeye anakila kitu wakati waliomsaidia wengi wao hawana kitu. Tuache kuwatukuza hawa viongozi!!! This thinking hautifikishi kokote inaturudisha nyuma sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…