Sokomoko la zawadi ya gari ya Rais mstaafu Mwinyi

Sokomoko la zawadi ya gari ya Rais mstaafu Mwinyi

Jana Rais Samia kwenye uzinduzi wa kitabu cha Rais mstaafu Mwinyi, alitangaza kuwa katika pia kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Rais wetu huyo wa zamani aliyetimiza miaka 96, serikali imempatia gari [jipya?] aina ya Mercedes Benz iliyo chini [sedan] kwa sababu aliyokuwa akiitumia [nadhani ni SUV] ilikuwa inampa shida kuipanda na kushuka kutokana na umri wake mkubwa kwa sasa pamoja na kimo chake [hapa nahisi Rais Samia alisema kwa utani].

Tangazo hilo la Rais Samia limezua sokomoko kubwa, hususan mitandaoni.

Mimi sina tatizo na ‘zawadi’ hiyo kwa Rais wetu huyo mstaafu. Kwa maelezo machache aliyoyatoa Rais, sina pingamizi lolote lile.

Ila kuna wengine hawakufurahishwa na jambo hilo. Wamehoji kwamba iweje mtu kama Rais Mwinyi, ambaye katumikia taifa kwa muda mrefu na katika nafasi za juu kabisa, mtu mwenye istihaki nyingi hivyo, ashindwe kujinunulia gari linalomfaa kwa matumizi yake.

Rais Mwinyi keshawahi kuwa waziri. Keshawahi kuwa Rais wa Zanzibar. Na alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Sina hakika kama pia huwa anapata marupurupu ya utumishi wake kama Rais wa Zanzibar au la. Naamini ya urais wa Jamhuri ya Muungano anayapata.

Sasa mimi nina maswali kadhaa:

1. Je, hilo gari alilopewa hivi sasa ni la kwake? Limesajiriwa kwa jina lake? Yeye ndo analilipia bima?
Mimi muda wote huu nimekuwa nikidhani kuwa marais wastaafu huwa wanapewa gari ya matumizi na serikali na kwamba magari hayo huwa ni mali ya serikali.
Yaani, Rais mstaafu huwa anapewa gari, ofisi, watumishi wa ofisi, walinzi, na kadhalika.

2. Kama hivyo ni ndivyo, ni kapewa au wamembadilishia tu gari ya matumizi na siku atayoacha kuitumia itarudishwa ilikotoka?

3. Kama wamembadilishia tu gari, Rais angesema ‘tumembadilishia’ gari la matumizi kuliko kusema ‘tumempa’ gari jipya kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa, ingekuwa ni bora zaidi na isingezua sokomoko?

Tatizo nilionalo hapa ni kuhusu timing, optics, na word choice tu.

Zaidi ya hapo kelele zilizopigwa sizioni kama ni hoja zilizo compelling.

Rais Mwinyi siyo raia wa kawaida. Hawezi kulinganishwa na wazee wengine ambao hawajawahi kuwa marais.

Rais Samia kusema ile majuzi kuwa serikali haina hela za kutosha kuwapa posho wazee, hiyo haina maana serikali haina hela za kuwatunza marais wa zamani.

So this is much ado about nothing.

Go ahead and click that ‘Like’ button if you agree with me. Even if you don’t agree but you appreciate the content, go ahead and smash that button.

Happy Sunday and most importantly, have a very happy Mother’s Day!
Kumbuka kwamba anapokea kama pensheni, 80% ya mshahara wa rais aliyepo madarakani kila mwezi!
Hii ni kwa mujibu wa Sheria Na. 2 ya 1999 aliyojitungia B. W. Mkapa.
Kwa mujibu wa Sheria hiyo kila baada ya miaka 5 lazima bunge liipitie upya "kwa madhumuni ya kuiongeza".
 
Kwenye hili sakata nimegundua watu wanaomchukia Mother wapo wa makundi 3:
1. Wasiotaka Rais mwanamke, hawa ni jamaa wasiotaka kukubali kuwa dunia imebadilika sana
2. Watanganyika wanaochukia kutawaliwa na Mzanzibari, hawa ni wengi zaidi
3. Wakristo wasiopenda kutawaliwa na mwislamu, hawa wengi vile vile.
Sababu zingine ndogo ndogo na ni wachache ni vyama vya upinzani na watu walioumizwa sana na kifo cha JPM
Inawezekana maana hoja za wanaopinga mzee kupewa kabenzi ni nyepesi mno.
 
Sasa 450 m mbona unaziona si mali kitu wakati 38 m zilikuuma!? Au matumizi ya 38 m yalifanya jambo lisilo na manufaa kwa taifa lakini 450 zimefanya jambo muhimu, zito, la lazima na manufaa kwa taifa!?
Hivi hiyo Milioni 450 mmeipata wapi? Maana mnajibu tuu kama kasuku kila mtu 450 mia nne hamsini. Kama ni mtihani wote si mtakuwa mmefeli?
 
Mbona hukuhoji pale Mwendazake alivyonunua jogoo kwa laki moja? Mbona hukuhoji source ya hela ambazo Mwendazake alikuwa anatapanya hovyo kwa kuwazawadia watu mikutanoni?
Vitu kama si vyote alivyofanya Mwendazake Kama hivi hukutia neno na ulipotaka kusema ulileta ki complicated English ili ku blur intention 😃😃
Mtulie, rais Samia ametoa kwa niaba yetu zawadi kwa rais mstaafu. Ulitaka akodishiwe gari na serikali aliyoitumikia kwa 10 years kama kiongozi mkuu.
MATAGA kubalini bhasi
Unauhakika watanzania hawakuhoji? Au genye zimekujaa... watu walipiga kelele kuwa ni rushwa na tena aliendelea hadi uchaguzi ulipokuwa unakaribia jiwe anamwaga tu pesa barabarani wapinzani walipiga kelele... hivi mlikuwa wapi hadi muongee as if watu kuwa walikaa kimya watu hawakumuogopa Meco japo alikuwa anapoteza watu mashujaa walikomaa tu... ukifanya upuuzi mbele za watu utapondwa tu... naomba unyamaze kitendo cha jana ni upuuzi wa kutia hasira.. kama huna pesa fanya yasiyo gharama na kama pesa ipo toa kwa wote
 
Zawadi ya gari ina ubaya gani?
Ingekuwa ya bei rahisi sawa... kumbuka sheria inasemaje kuhusu thamani ya zawadi kwa mtumishi au mtu anayepokea mshahara kutoka serikalini... kuna thamani ikizidi unaikabidhi serikali ukiibeba zako inakuwa Rushwa.
 
Tatizo ni kuwa, bimkubwa juzi tu kawaambia wazee wa dar kuwa hakuna fedha ya kuwapa walau 30,000 kwa mwezi. Jana amemtunuku mzee Mwinyi Benz, watu wanamaind hilo pia.

Tujue tu kuwa mwenye nacho anaongezewa, Hussein angeweza kumnunulia mzee wake hiyo Benz coz hashindwi, mzee anapata pensheni nono kila mwezi....
Kwahiyo kila mzee wa dar ni Rais mstaafu wa Tanzania?
 
Mbona magufuli aliwajengea Nyumba wastaafu lakini hakuna aliehoji kama pesa imetoka wapi
 
Uzanzibari tu zamani hatukujua kabisa BIRTHDAY ya mwinyi
 
Ona sasa badala ya kujibu swali langu unakuja na mambo ya u team. Pole umeishiwa
Najibu vipi swali lisilokuwa na mantiki yoyote, hilo swali una majibu yake. Kwamba kila mzee wa Dar ni raisi, are you outta mind mkuu? Siku nyingine njoo na swali...utajibiwa!!
 
Yaan mambo mengine yana umiza mioyo ya wananchi ila basi tu.
Fanyen kazi,somesheni watoto zenu waje kula cake ya Taifa, porojo zingine hazina msingi, milion 450 kwa serikali ni sawa na buku jero tu kumnunulia zawadi mzee wetu mwinyi
 
Mbona leo sisikii ooh MATAGA
Hili MATAGA wanalifurahia kwa vile limeudhi wengi.
Kwao ni kama kumsukuma mlevi!

Its shocking jinsi wandaaji wa shughuli ya Mwinyi , Ofisi ya Ikulu pamoja na Wizara ya Michezo wasivyiweza kuona the bigger picture.
 
Najibu vipi swali lisilokuwa na mantiki yoyote, hilo swali una majibu yake. Kwamba kila mzee wa Dar ni raisi, are you outta mind mkuu? Siku nyingine njoo na swali...utajibiwa!!
Sasa mnakosea mnapomlinganisha mzee mwinyi na kila mzee wa dar. Hilo swali nilikuuliza ili kichwa chako kifunguke uweze kuelewa hoja yangu.
 
Sasa mnakosea mnapomlinganisha mzee mwinyi na kila mzee wa dar. Hilo swali nilikuuliza ili kichwa chako kifunguke uweze kuelewa hoja yangu.
@Waterloo,
Nakuheshimu sana mkuu, Ila hapo hakuna hoja. Jaribu kufikiria tena kwamba je, mzee Mwinyi kweli alihitaji hiyo zawadi wakati tunaambiwa taifa linapitia kipindi kigumu hata kushindwa kuongeza watu mishahara?
 
Back
Top Bottom