Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Hapo kuna vitu viwili
1. Zawadi
2. Stahiki
Hatuna Shida na namba 2, Kama ni Stahiki yake basi atwambie kuwa kampa stahiki yake. Na pia tunataka tujue, Stahiki yake ina ukomo upi, Je anaweza kumpa chochote kile anachoona kinafaa? —Yaani akijisikia kumpa hata private Jet anaweza ili kumrahisishia kumove around?, Je Mwinyi aliandika barua kuomba stahiki hiyo?
Kama ni zawadi tunataka kujua, Je Kodi za wananchi na mali ya Umma inaweza kugaiwa tu kama zawadi tu kwa mtu kujisikia?, Yaani rais anaweza kuamka asubuhi akachukua mali ya umma na kumpa mtu kama pipi?, Kama ana power hizo, vipi let say akiamua kumgawia mtu Kiwanda cha umma kama zawadi au what if kama akiamua kutwaa donge kubwa la mabilioni la dhahabu lililo benki kuu na kumgawia mtu?. Je kuna sheria ya Zawadi?.
Bwana Ngabu, Hii nchi ilipotoka enzi za Nyerere tulijifunza mambo ya cheo ni dhamana sitotumia cheo changu kwa manufaa binafsi, Sasa hawa akina Mzee Mwinyi enzi za ujana wao ndo walikuwa wakiimba Slogan hii kama Kasuku, Sasa Leo hii kastaafu, haipaswi atumie cheo chake cha zamani kwa manufaa binafsi, maana kapewa gari hilo kwa kofia kuwa "aliwahi kuwa rais".
Mwisho niseme, Mwinyi anao uwezo wa kujinunulia gari analohitaji, kwa sababu ana majumba, ana pensheni, ana ardhi, kiufupi hata kukopesheka anakopesheka, Kwa hiyo kutwaa mali ya umma na kumpa eti zawadi ni kutapanya kiduchu ambacho tunakihitaji kuondoa umasikini wa watu wetu wetu.
Ila kama ni Stahiki yake basi tusiambiwe kuwa ni Zawadi.