mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 88,759
- 123,368
Sawa....nini mnataka kifanyikeMimi naona huku ni kudhalilishana kweli. Hawa ni watu walioomba wenyewe hiyo kazi, hawakutufanyia favour kwamba alikuwa mahali tukamuomba aje atusaidie. Huyu aliwatumikia raia wa nchi hiyo kwa utashi wake. Sasa haya ya shukrani zilizopitiliza zinatoka wapi?
Hakuna Rais mstaafu ambae hakuna nyumba yake binafsi ( wengine zaidi ya moja). Hamna Rais mstaafu asie na uwezo wa kujinunulia gari anayoitaka kutokana tu na posho yake ambayo ni asilimia 80 ya mshahara wa Rais aliyekuwepo. Rais mstaafu anapewa magari mawili na yanabadilishwa kila baada ya miaka mitano. Analipiwa mpaka dobi. Yote hayo bado tunaona ana shida sana kiasi cha kutaka waboreshewe mafao yao! Kusema leo tunamjengea nyumba Rais mstaafu na kumnunulia gari ni kumdhalilisha kuwa ni maskini kiasi hicho.
Kwa wenzetu Marekani Rais mstaafu anajinunulia nyumba. Sijasikia waziri mkuu wa uingereza au India wakipewa nyumba au magari baada ya kustaafu. Wao kama ilivyo kwa watumishi wengine wa umma wanatarajiwa kuwa wamejipanga kwa ajili ya maisha ya ustaafu.
Mimi ningeunga serikali kama ingetenga fungu ( milioni 500) ambazo mstaafu ataweza kutumia kujenga kitu chenye faida kwa jamii kama kumbukumbu yake, vitu kama maktaba, sehemu ya utafiti n.k.
Haya ya nyumba na magari ni kuwafedhehesha tu. Aidha, itaonekana kama Rais aliyepo anayapigia debe kwa vile anajua yeye pia atanufaika.
Amandla....
Kuondoa mambo haya
Ova