Soma hapa kabla ya kuchapisha andiko lako katika Jukwaa la Stories of Change

Soma hapa kabla ya kuchapisha andiko lako katika Jukwaa la Stories of Change

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
Kwa wote wanaotaka kushiriki shindano la Stories of Change Tafadhali someni kwa makini vigezo hivi. Hakikisha andiko lako limekidhi kabla ya kutaka kuchapisha.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:
  1. Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.
  2. Andiko liwe kwa Kiswahili lenye maneno yasiyopungua 800 na yasiyozidi 1000.
  3. Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism (Wizi wa machapisho mengine) haitaruhusiwa.
  4. Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa taarifa binafsi (jina) endapo ataibuka mshindi.
  5. Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
  6. Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.
 
Upvote 73
Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.

Swali langu hapa Ni je Ni lazima andiko lihusishe mambo yote hayo au moja katika hayo mfano naweza andika andiko kuhusu elimu tu?
 
Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.

Swali langu hapa Ni je Ni lazima andiko lihusishe mambo yote hayo au moja katika hayo mfano naweza andika andiko kuhusu elimu tu?
Andiko lako linaweza kujikita kwenye jambo moja au zaidi katika hayo yaliyoorodheshwa
 
Kwa wote wanaotaka kushiriki shindano la Stories of Change Tafadhali someni kwa makini vigezo hivi. Hakikisha andiko lako limekidhi kabla ya kutaka kuchapisha.

Vigezo na masharti ya kushiriki katika shindano hili:
  1. Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.
  2. Andiko liwe kwa Kiswahili lenye maneno 800 hadi 1000.
  3. Makala zinatakiwa kuwa habari au makala halisi zisizowahi kuchapishwa sehemu nyingine yoyote. Plagiarism (Wizi wa machapisho mengine) haitaruhusiwa.
  4. Mshiriki anaweza kutumia jina la kubuni ‘pseudonym’ lakini atatakiwa kutoa taarifa binafsi (jina) endapo ataibuka mshindi.
  5. Matumizi ya picha au video yanaruhusiwa ili kushibisha andiko. Endapo picha na video sio za mshiriki, atalazimika kutaja chanzo.
  6. Watendaji wa Jamii Forums na ndugu zao wa karibu hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano hili.
Thank you
 
Mshiriki anatakiwa kutayarisha andiko linalochochea mabadiliko kwenye nyanja za Elimu, Uchumi, Kilimo, Utawala, Afya, Sayansi na Teknolojia.

Swali langu hapa Ni je Ni lazima andiko lihusishe mambo yote hayo au moja katika hayo mfano naweza andika andiko kuhusu elimu tu?
napenda kuuliza andiko hili tunaliandikia sehemu gan hum au tunaandika kwenye karatasi kwanza then tunalituma?
 
MAENDELEO NA KAGERA
Dhana ya maendeleo watu wengi huitafakari tofauti kabisa.
Wataalamu wengi husema maendeleo ni ile hali ya kutoka kwenye hali duni kwenda kwenye hali bora( hali yenye unafuu kuliko ya awali)
Watu wengine hudhani maendeleo ni mfano kupatikana kwa umeme, barabara safi tena za lami, upatikanaji wa maji safi na salama hasahasa yale maji ya bomba,hospitali nzuri n.k
Wote wako sahihi.
lakini leo ebu kidogo tujikite kidogo kwenye maendeleo yahusuyo kipato cha mtu mmoja mmoja yaani maendeleo ya kiuchumi tuaachane kidogo na maendeleo ya kijamii. Mimi naamini zaidi sana mtu akiniambia sehemu fulani imeendelea asinionyeshe majengo mazuri,barabara,hospitali tu bali twende zaidi katika kuangalia maendeleo ya mtu mmoja mmoja hasa kiuchumi(economic development).
Mkoa wa Kagera ni kati ya mikoa mitatu duni zaidi kwa mujibu wa ripoti ya serikali ya mwaka 2016, japokuwa mwaka 2018 ripoti hiyo iliusogeza mbele kidogo.
Nimekuwa nikifatilia kwa karibu maisha ya watu,mienendo,tamaduni nimegundua kuna vitu ambavyo vinachangia mkoa huu kuwa nyuma na pia kuendelea kurudi nyuma siku zinavyosonga.
Sababu hizo ni kama ifuatavyo

1.ARDHI.
Swala la umilikaji Ardhi mkoani Kagera ni kizungumkuti.Tokea enzi na enzi mkoa huu umekuwa chini ya Nyarubanja. Hii system ya kiuchumi imepitwa na wakati na haifai kuendelea kutumika kwa sasa.
Mfumo huu huusisha mzee wa ukoo kumilika ardhi ambayo uwagawia wanae wote, baadae wanae pia upata watoto na kuwagawia pia,baadae uenda hivo mpaka vitukuu.
Mfano fikilia mzee wa ukoo labda alimiliki hekari 20 ,akazaa watoto 20,kila mtoto atapata takribani hekari moja, na haohao watoto wakipata watoto wao ,ebu tuseme kila mmoja apate watano,ataendelea kuwagawia hekari moja ileile na baadae hao watoto wataigawa tena kwa watoto wao tena.
Inawezekana mzee aliyekuwa na hekari 20,saa hizi kitukuu atamiliki kitaru tu

Nini kifanyike
Kutokana kwa mkoa wa Kagera bado takribani asilimia 80 ya ardhi yake haijakaliwa na watu ni bora serikali za vijiji kwa mamlaka zilizopewa kupitia wafikilie uwezekano wa aidha kuwauzia watu ardhi,kukodisha au kuwagawia kulingana na sheria ya ardhi inavyodai.
Hapa simaanisha wauze au wagawe maeneo yote hapana maana kuna ardhi inabidi ibaki kwa vizazi vijavyo
Lakini pia pesa itakayopatikana kutokana na uuzaji au ukodeshaji wa ardhi itumike kuendeleza huduma za kijamii.

2.Kilimo
Ni ukweli usiopingika kwamba staili ya kilimo inayotumika mkoani kagera hasahasa Missenyi,Bukoba,Biharamulo na Muleba imepitwa na wakati, hapa sijaitaja Karagwe kwasababu angalau Karagwe wanajitahidi kidogo.
Miaka ya 90 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000,kilimo kilikuwa bora mkoani Kagera lakini baada ya kuingia mnyauko wa migomba pamoja na magonjwa ya kahawa kwa sasa kagera imefeli vibaya katika nyanja za kilimo.
Mwanzoni mwa miaka ya 2000,watu walilima kwa trekta hasahasa zile za KCU leo hii watu wamerudi kwenye kilimo cha jembe la mkono, maeneo yakulima vimekuwa vibustani kutokana na mfumo wa nyarubanja.

Nini kifanyike

Mapendekezo namba moja hapo juu
Pili ziwepo tafiti za kilimo kuhusu kahawa na migomba
Tatu, NGOs zijikite zaidi ktk kuelimisha juu ya mbinu bora za kitaalamu za kilimo biashara.

3.USAFIRI NA USAFIRISHAJI
Kagera inaitaji barabara za lami,meli,viwanja vya ndege. Mpango wa Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa sio wa kuachwa.
Kubwa kuliko Kagera inaitaji usafiri wa reli/treni.
Usafiri wa reli/treni ndio usafiri bora zaidi na wa uwakika kwa nchi zetu hizi duni

Naweza kueleweka vibaya nikisema bora meliisiwepo,uwanja wa ndege usiwepo ila kukawepo na reli
naamini wengi hawatanielewa ila kusafirisha mzigo kwa reli kutoka dar es salaam mpaka bukoba inaweza kuwa sh10000 kwa mzigo ambao mtu atasafirisha kwa laki moja kwa bus. Lakini pia usafiri wa meli unaunganisha mkoa wa Kagera na Mwanza tu wakati Kagera inatakiwa kuungwa na mikoa mingine zaidi.
Usafiri wa meli ni wa bei rahisi kweli lakini kwa treni ni bei rahisi zaidi uenda ata nauli ya kutoka bukoba mpaka Mwanza inaweza kuwa elfu 9 mpaka 10.

4.UHAMAJI WA WATU
Mkoa wa kagera ni mkoa unaoandamwa na watu wanaoamia mikoa mingine kila uchao.Hii inapunguza nguvu kazi.
Watu wanaenda mikoa mingine kutafuta mahitaji ya kijamii. Nahisi ni bora kuangalia uwezekanao wa kusogeza mahitaji hayo karibu.

5.KAHAWA NA MAZAO MBADALA
Kahawa naiongelea mara mbili hapa .Nimeisha iongelea kwenye swala la kilimo. Kahawa ilikuwa kama madini kwa kagera. Lakini kwa sasa kilimo hiki kimekufa.

NINI KIFANYIKE
napendekeza zifanyike tafiti za kutosha juu ya zao hili
pili wananchi wafundishwe juu ya kilimo cha kisasa
tatu,watafiti waje na mbege bora zinazoendana na mabadiliko ya tabia ya nchi
nne, yawepo mazao mbadala yanayoendana na hali ya Kagera.
Napendekeza mazao yafuatayo
1.KATANI
hali ya hewa ya mkoa Kagera haipishani sana na Tanga na Morogoro, kwa iyo zao la katani linaweza kustawi kwa wingi mkoani Kagera na kuchangia katika maendeleo ya mkoa.
2.ALIZETI
licha ya kwamba zao la Arizeti ulimwa sehemu zenye upungufu wa mvua ila sio kwamba halistawi kwenye maeneo yenye mvua .Mfano zao hili linalimwa Moshi,Kilimanjaro japokuwa kwa uchache.
3.PAMBA
4.UFUTA
5KARAFUU n.k

6.BEI ZA BIDHAA
Mkoani Kagera ni dhairi kwamba bei za bidhaa zipo juu sana.

NINI kifanyike
Ujenzi wa reli utasaidia gharama za usafirishaji kuwa ndogo hivo bei zitashuka
pili,Serikali iharakishe ushirikiano wa jumuiya ya africa mashariki ili biashara uria ifanyike kati ya Kagera na Uganda.

7.BEI YA PETROLI NA DIZEL
Ni ukweli kwamba mkoani Kagera bei ya mafuta hiko juu sana.Bei ya mafuta ndo utabiri gharama za maisha ziwe juu au chini.

nini kifanyike
ujenzi wa reli
pili ifanyike tathimini tena ili bei ya bidhaa hii adimu iwe chini kiasi

8.UWEKEZAJI
uwekezaji ktk mkoa kagera bado uko chini licha ya kuwepo rasilimali nyingi

nini kifanyike
zitatuliwe changamoto zoto nilizozielezea hapo juu ili kuvutia wawekezaji

9.UVUVI
Hii ni kazi nyingine muhimu mkoani Kagera laikin bado uvuvi uko chini sana ukilinganisha na Mwanza.

nini kifanyike
Taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali ziwaelimishe wqananchi juu ya uvuvi wa kisasa.
Pia changamoto za usafiri na usafirishaji zitatuliwe

10.SIASA
Mkoa kagera ni mkoa uliotawaliwa na siasa za kijani ukiachana na jimbo la bukoba mjini.
Niliwahi kusema kwamba ili mkoa wa KAGERA uendelee hauitaji CCM wala CHADEMA. Nikaenda zaidi nikasema kuwa si CCM wala CHADEMA zitakazoleta maendeleo kwa Kagera.

Lakini siku zote mkoa ukiwa chini ya chama kimoja uwa unasahauliwa kwaiyo nishauri kwamba kwa kuwa mkoa huu umekuwa chini ya kijani na bado unarudi nyuma kimaendeleo basi ni bora kuwaajibisha hawa kijani ili wajifunze wananchi wanataka nini.

ahsante
 
Vipi unaweza kuandika kwa mfumo wa shairi, tenzi, ngonjra au lazima liwe kwenye mfumo mmoja wa makala tu
 
Back
Top Bottom