Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Waislamu wengi wa kiafrika hawajui Quran kwasababu ya lugha.
Huyu mifano yote ameitoa kwenye biblia. Angeaonyesha kwa mifano kuwa kwenye Quran hakuna jambo hilo, Ningemuelewa sana.
Huwa napata wakati mgumu sana kujua hawa watu kama wanaelewa Quran vilivyo.
Hata maandiko yao hapa JF utayakuta yale ya Rest in peace, najuni sijui nini lkn mambo mengine kuhusu yaliyoandikwa kwenye Quran hakuna.
Wewe ungekuwa mjumbe mzuri sana kwa kuelezea Quran ilivyokuwa nzuri lkn umeishia kwenye Biblia.
Cha ajabu na kinachosikitisha huyu Yesu ambaye humtambui lkn Quran inamtabua kama nabii issa lkn kwa sababu hamjui lugha mnafikiri Yesu wa kwenye Biblia na kwenye Quran ni yule yule.
Muislamu ukimwambia mimi ni mkristo nihubirie ili nisilimu. Hapo ataanza kuikosoa Biblia, atatoa mifano mingi ya kwenye Biblia 99% na Quran 1% anamalizia kukuambia ni dini ya haki. Unashangaa hawa watu wanaelewa au wamekaririshwa?
Hongera sana kwa kuisoma Biblia, hii inaonesha unaisoma na kuikubali sana Biblia kuliko Quran. Kinachokufanya usiisome Quran ni kwasababu huijui lugha ya kiarabu. Bila kujua lugha ya Kiarabu huwezi kusali wala kwenda peponi lakini kwetu Mungu wetu anajua lugha zote.
Kuna njia mbili zinazoweza kupitiwa ili kuufikia utambulisho wa Yesu Kristo na yaliyomo katika ujumbe wake.
Ya kwanza inaangazia makusanyo ya rekodi za kihistoria za wanahistoria wa kisasa kutoka katika maandiko na masalio ya kipindi hicho na ya pili inaangazia ripoti zilizomo katika Maandiko ya ufunuo.
Kwa ukweli, kuna ushahidi mchache mno unaotufahamisha kuwa Yesu alikuwa ni nani, au unaobainisha ujumbe wake ulikuwa ni nini.
Nyaraka rasmi za kihistoria za kipindi hicho kwa hakika hazina rekodi yoyote juu ya Yesu.
Msomi wa Biblia, R.T. France, anaandika,
"Hakuna andiko lolote la karne ya kwanza linalomtaja Yesu na hakuna kitu chochote au jengo lolote lililobakia na ambalo lina uhusiano naye."
Ukweli huu umewafanya baadhi ya wanahistoria wa Kimagharibi kukosea na kudai eti Yesu Kristo wa hakika hajapatapo kuwepo.
Kwa hiyo, kimsingi, utafiti lazima uegemee maandiko matakatifu yanayoeleza haiba na kazi za Yesu Kristo.
Maandiko matakatifu yatakayoulizwa ni yale yanayotambulikana kirasmi na dini zote mbili Ukristo na Uislamu.
Hata hivyo, kuchambua barabara, maelezo yaliyomo katika maandiko ya kidini, ni jambo la msingi kuanzia na kupima usahihi wa maandiko hayo.
Je, vitabu vya dini ni vyanzo vya kuaminika kuwa nyaraka za ushahidi, au ni ubunifu wa simulizi za kibinadamu na visa asili, au ni mchanganyiko wa yote mawili?
Je, Biblia, Agano la kale na Jipya ni maandiko ya ufunuo wa Mungu?
Je, Quran (Kurani) ni sahihi?
Nitaendelea