Somo la 'Historia ya Tanzania' alilotaka Magufuli lasitishwa

Somo la 'Historia ya Tanzania' alilotaka Magufuli lasitishwa

Magufuli alikuwa sawa, achaneni kupinga kila jambo:
Tuachane na mtaala wa kikoloni tufundishe watoto wetu historia yetu na ya mababu zetu, tamaduni zetu, mila zetu, ili tukuze uzalendo kwa vizazi vya sasa na vijavyo
Hakuna haja ya kufundisha historia kwa Kiingereza,
Magufuli alikuwa sawa, ProfesaNdalichako harakisheni huo mtaala mpya
Teh teh teh ndio imeisha hiyo..
 
Hilo SoMo halina umuhimu wowote kwa sababu sioni utofati wake na historia inayosomwa shule ya msingi, zaidi sana ni kuongezea watoto wetu mzigo wa masomo yasiyo na ulazima. Nilichogundua hiyo historia ya Tanzania ulikua imelenga kuwasifu viongozi wa fisiemu na si vinginvyo.
Wanataka kutengeneza kizazi cha kuwachukia mabeberu.

Kizazi ambacho wanasiasa watakitumia kama kichaka kutupia sababu za kushindwa kutekeleza majukumu yao.
 
Ni maagizo ya kipumbavu.

Lazima yatupiliwe mbali.
Kujifunza na kufundisha vijana wetu na kizazi kijacho historia ya nchi yetu ni maagizo ya kipumbaavu? Mpumbavu ni wewe uliyepofuliwa na chuki mpaka hutambui jema na la manufaa kwako na kizazi chako ni nini!
 
Mtaala hatengenezwi na mtu mmoja, inapitishwa na jopo la watu mbalimbali. Hii hofu ya siasa itatukwamisha hata kwenye mambo ya msingi
Hivi vile vitabu ndalichako alivyosema wameshaandaa SoMo lianze kufundisha mwezi wa Saba Ile haraka ilikua ya nini?

Hatua zote zilifiatwa kweli? Ndalichako alituangusha sana kwenye hili kuweka taaluma pembeni na kuingiza siasa.
 
Magufuli alikuwa sawa, achaneni kupinga kila jambo:
Tuachane na mtaala wa kikoloni tufundishe watoto wetu historia yetu na ya mababu zetu, tamaduni zetu, mila zetu, ili tukuze uzalendo kwa vizazi vya sasa na vijavyo
Hakuna haja ya kufundisha historia kwa Kiingereza,
Magufuli alikuwa sawa, ProfesaNdalichako harakisheni huo mtaala mpya
Ni kipi ambacho kinakosekana kwenye somo la historia la sasa?
 
Yaani hadi Professor Ndelichako anamsaliti Magufuli? Kweli?
Ni Magufuli aliyemuinua Professor Ndelichako kutokea benchi, akampa ubunge wa bure na zawadi ya uwaziri, leo hii bila aibu anaizika legacy ya Magufuli kirahisi.

Nimeamini adui wa mtu ni watu wa karibu yake. Magufuli alizungukwa na wanafiki watupu, akawakumbatia huku akiwaangamiza wapinzani.
Profesa anafanya mambo yenye manufaa kwa nchi siyo kulipa fadhila kwa aliyemteua
 
Huo mtaala unamsaidia nini kijana baada ya kumaliza elimu yake?

Tafuteni mmabo ya muhimu hata fani za ufundi ndio ziwe za lazima katika ulimwengu huu historia inamchango mdogo sana kwenye maisha ya kila siku.

Kuna SoMo la historia shuleni bado mnatka kulazimisha kuongeza na lingine kwanini msiboreshe hilohilo lililopo mashuleni ikawa mwaka mzima au miwili mtu anasoma historia ya Tanzania kwanini iwe mtu anasoma miaka yote ya shule kwa content ipi ya hiyo historia yetu na itasaidia nini mtu kujikwamua kwenye hili tatizo la ukosefu wa ajira?

Pia hao wataalamu wa kufundisha hiyo historia ya Tanzania mmewaandaa? Swala la mtaala Lina taratibu zake yaani mnataka hiyo historia ifundshwe na watu amabao hat Wao hawajaijua hiyo historia?
Kila somo lina sehemu yake kwenye maisha hata kama sio sehemu ya taaluma ya baadaye ya muhusika

Mentality na mitizamo yetu inajengwa na jinsi tulivyokuzwa na kufundishwa

Ukimfundisha mtoto takata atakuja kuwa takataka

Ukimfundisha mtoto bangi, atakuja kuwa bangi tu

Historia iliyobuniwa vizuri inawajengea watoto positive mentality na patriotisms hata wakiwa wakubwa na viongozi kwenye jamii bila kujali taaluma
 
Magufuli alikuwa sawa, achaneni kupinga kila jambo:
Tuachane na mtaala wa kikoloni tufundishe watoto wetu historia yetu na ya mababu zetu, tamaduni zetu, mila zetu, ili tukuze uzalendo kwa vizazi vya sasa na vijavyo
Hakuna haja ya kufundisha historia kwa Kiingereza,
Magufuli alikuwa sawa, ProfesaNdalichako harakisheni huo mtaala mpya
Kwamba wafundishe kuhusu mizimu ya mababu zetu?
 
Back
Top Bottom